STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 22, 2016

TFF mnatania au mnawataka ubaya Wekundu wa Msimbazi?!

http://www.timesfm.co.tz/wp-content/uploads/2016/04/Alfred-Lucas.png
Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEguD-aZGG5X59TJ_U5wBcN4j_dmq1GHSge94N-6O3EvLKtFeSYpVKM2frwbCVbwcv0jznXiFEatblJrg-Z12VhIt6yK2CbIpq0_jojZb5CdYPWrHCiCJMnlQSiO1lCdWepV75H9GbZSbkk/s1600/MMG25686.jpg
Mashabiki wa Al Ahly wakipewa sapoti na mashabiki wa Simba wakati wa mechi baina ya Wamisri hao na Yanga lililochezwa Uwanja wa Taifa hivi karibuni
BILA shaka Simba watakuwa wanacheka huko walipo, baada ya kulisikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwaangukia na kuwataka wawe na uzalendo kwa kuishangilia Yanga itakapokuwa ikiumana na TP Mazembe Jumatano ijayo.
Simba na Yanga kwa miaka mingi zimekuwa zikishindwa kupigana tafu kwenye mechi zao za kimataifa, kwa tabia yao ya kushangilia wageni na kufikia hatua ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayocheza na mmoja wao, lakini TFF kupitia Afisa Habari wake, Alfred Lucas imewaomba mashabiki kuwa wazalendo kuisapoti Yanga.
Lucas alisema TFF inawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushangilia kwani wanaamini mashabiki ni mchezaji wa 12 na uwepo wao utaongeza ari ya ushindi.
"Tunafahamu mchezo wa Yanga utakuwa na changamoto zake kwa vile  wameanza kwa kufungwa na TP Mazembe wanaongoza kundi lakini tunaamini watafanya vizuri kwani inachezwa kwa mtindo wa ligi hivyo mashabiki waje kushangilia timu zetu.", alisema Lucas.
Yanga itacheza na Mazembe Juni 29 kwenye mchezo wa Kundi A ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kusisitiza kuwa mafanikio ya Yanga ni faida kwa soka la Tanzania na kuomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono kama ambavyo anataka wajitokeze Jumapili kuishangilia Serengeti Boys itakayocheza na  Shelisheli mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Vijana U17 Afrika.

Tayari mashabiki wa Simba wameshaanza kununua jezi za Mazembe ili kuwaunga mkono katika mechi hiyo na iwapo watasikia ombi hilo la TFF lazima wataumia mbavu kwa kucheka kwani ni jambo lisilowezekana kwao kama ambavyo kigogo wa klabu hiyo, Zakaria Hanspoppe aliwahi kukaririwa akisema huwa anahisi kichefuchefu akitajiwa jina la Yanga.

No comments:

Post a Comment