STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 22, 2016

Man City yakaribia kunasa kifaa kingine kipya

http://estaticos.marca.com/imagenes/2015/09/24/en/football/spanish_football/1443048045_extras_noticia_foton_7_0.jpgWANAMCHUKUA. Klabu ya Manchester City, ipo hatua ya mwisho kumnasa straika wa kimataifa wa Hispania, Nolito kutoka Celta Vigo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amethaminishwa kwa kiasi cha Euro Milioni 18 katika mkataba wake na Rais wa Celta Vigo, Carlos Mourino tayari ameshadokeza anategemea ataondoka dirisha hili la usajili.
Taarifa zilizotolewa na gazeti la Guardian la Uingereza zimedai kuwa, Man City ina uhakika wa kukamilisha dili hilo na kuongeza kuwa Nolito tayari ameshakubali mambo binafsi katika mkataba wa miaka mitatu atakaopewa wenye thamani ya Euro Milioni 4 kila msimu.
Straika huyo wa zamani wa Barcelona, aliyeichezea timu yake ya taifa ya Hispania katika mechi zote tatu za makundi ya michauno ya Euro 201, awali alikuwa akitajwa kuwindwa na timu yake ya zamani ya Barcelona iliyotaka kumrejesha kikosini.
Nyota huyo mwenye bao moja kwenye michuano hiyo ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa, aliondoka Nou Camp mwaka 2011 kwenda Ureno kujiunga na Benfica  kabla ya baadaye kutua Celta Vigo.

No comments:

Post a Comment