STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 22, 2016

Shelisheli lazima wapigwe Taifa, kama unabisha subiri J'Pili


Wachezaji wa Serengeti Boys wakijifua mazoezi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Shelisheli
LAZIMA wapigwe! Kocha wa timu ya taifa ya Vijana ya Tanzania U17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amejigamba kuondoka na ushindi dhidi ya Shelisheli katika mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumapili hii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kocha Shime alisema timu yake ameiandaa vya kutosha ikiwa imepata mechi kadhaa za kimataifa za kirafiki hali iliyomwezesha kukisuka vema kikosi hicho.
“Naamini kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari ya kwenda Madgascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya”, alisema Shime.
Mchezo huo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa Vijana U17 utachezeshwa na waamuzi toka Ethiopia ambao ni Belay Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati na wasaidizi wake ni Tigle Belachew na Kinfe Yilma Kinfe huku mwamuzi wa akiba akiwa  ni Lemma Nigussie na Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys iliyoingia kambini  Juni 14, 2016 itarudiana na wapinzani wao  Julai 2, 2016, endapo itafuzu hatua hii itakutana na timu ya Vijana ya Afrika Kusini.
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba amesema wapo tayari kupambana na anaamini ushindi ni wao huku akiwataka mashabiki kuja kuwashangilia.

No comments:

Post a Comment