STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 22, 2016

Jose Mourinho kumvuta Matic Man United

Matic na Mourinho walipokuwa Chelsea
KOCHA Mpya wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anatarajiwa kumchukua nyota wake wa zamani aliyemnoa akiwa Chelsea kwa kubadilishana na Mchezaji wake mmoja kwa mujibu wa duru za kispoti za England.
Imeripotiwa kuwa wakati dirisha la usajili likitarajkiwa kufunguliwa Julai Mosi, Kocha Mourinho anatarajiwa kuitumia shauku ya Meneja mpya wa Chelsea kutoka Italy, Antonio Conte ya kumhusudu beki toka Italia, Matteo Darmian kwa kumtoa kama Ofa ya kumchukua kiungo wa Chelsea Nemanja Matic.
Tayari Mourinho ameshaanza kuisuka upya Man United kwa kumnunua beki wa kati kutoka Villareal, Eric Bailly na anatarajiwa kuongeza wapya wengine.
Matic, Mchezaji wa Kimataifa wa Serbia, alikuwa nyota wa kwanza kwa Mourinho kumnunua aliporudi Chelsea kwa mara ya pili kwa kumsaini mwaka 2014 kutoka Benfica na sasa inaelekea Mourinho anataka kuungana tena na Matic.
Chini ya Mourinho, Matic alikuwa na msimu mzuri wa kwanza huko Stamford Bridge na kuweza kutwaa Ubingwa wa England, lakini Msimu uliopita, hasa Mourinho alipotimuliwa Desemba mwaka jana, Matic hakuwa na namba mara kwa mara kikosini.
Haijulikani kama Matic atakuwa vipi chini ya Kocha Conte ambae bado hajatua rasmi huko Chelsea kwani yupo bado yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Italia katika fainali za Euro 2016 zinazoendelea Ufaransa.
Magazeti huko England yamedai Darmian yupo kwenye uhusiano mzuri na Conte katika timu ya Italia, kwani panga pangua hakosi namba na hilo limeleta imani kuwa anamtaka wawe wote Chelsea.
Darmian amekuwa na msimu mchanganyiko Man United ambako alitua mwaka jana kutoka Torino ya Italia na hilo, pengine ndio linamfanya Mourinho amtoe kafara ili amnase Matic ambae hucheza kwa kutumia nguvu katikati ili kuimarisha safu yake mpya.

No comments:

Post a Comment