STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 22, 2016

Yanga yaamua kuwachezesha Mazembe usiku

Kikosi cha Yanga

Mashabiki watakaoishangilia timu yao usiku Uwanja wa Taifa
Baadhi ya nyota wa Yanga akiwamo Nahodha Nadir Haroub Cannavaro atakayekuwepo kuivaa Mazembe
IMEFAHAMIKA kuwa, pambano la Yanga dhidi ya TP Mazembe la Kundi A michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika litapigwa usiku wa Jumatano na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.
Kwa mujibu kutoka kwa Msemaji wa klabu hiyo, Jerry Muro, mechi yao itapigwa majira ya saa 1:30 usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Muro alisema wameamua kulipeleka pambano lao Jumatano usiku ili kutoa fursa ya mashabiki wengi kuhudhuria baada ya kutoka kazini na wakishakula futari ikizingatiwa kwa sasa waumini wa Kiislam wapo kwenye mfungo wa Ramadhani.
Msemaji huyo alisema maandalizi yao kuelekea kwenye mchezo huo yapo shwari na kwamba wana uhakika wa kuwatumia baadhi ya nyota wao wapya ambao wamewasajili hivi karibuni akiwamo Mzambia, Obrey Chirwa, licha ya kwamba kuna nyota wao wengine watawakosa kwa kasi za njano walizopewa Bejaia Algeria.
Yanga ilipoteza mchezo wao wa kwanza wa kundi hilo dhidi ya MO Bejaia kwa kulala bao 1-0, wakati Mazembe watakaotua nchini Jumapili hii wakitokea kwao Lubumbashi waliitambia Medeama ya Ghana kwa mabao 3-1 na kuongoza msimamo.

No comments:

Post a Comment