STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 6, 2017

Zimbabwe kakosekana Ngoma na Kamusoko tu!

Bruce Kangwa
Kikosi cha Zimbabwe 'Thje Might Warriors
HARARE, Zimbabwe
KWA mashabiki wa klabu za Simba na Yanga, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Methodi Mwanjali ni nyota wa aina yao, wanawategemea kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara. Sasa sikia hii. Wachezaji hao kwao wala si mali kitu, kwani kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe nchi wanayotokea imeita nyota wake kwa ajili ya Fainali za Afcon 2017, bila ya wachezaji hao.
Nyota Khama Billiat aliyeshika nafasi ya pili katika tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ya bara hilo, pamoja na kiungo mwenzake na nahodha Willard Katsande ni miongoni mwa wachezaji nane wanaocheza soka Afrika Kusini ambao wameitwa katika kikosi cha Zimbabwe.
Mchezaji Zimbabwe katika mashindano ya mwaka huu imepangwa katika Kundi B, ambapo watacheza na Mabingwa wa zamani Algeria na Tunisia na Senegal, wakati timu mbili za juu zitatinga robo fainali.
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Zimbabwe kushiriki fainali hizo, ambazo walitolewa katika raundi ya kwanza nchini Tunisia mwaka 2004 na kupata pigo kama hilo nchini Misri miaka miwili baadae.
Mshambuliaji wa pembeni Billiat alikuwa mchezaji muhimu aliyeisaidia timu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns wakati iliposhina taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka jana.
Pia mchezaji huyo alikuwa mmoja kati ya wachezaji watatu waliofikia hatua ya mwisho ya kumsaka mchezaji bora wa Afrika kwa timu za ndani iliyotwaliwa na kipa Mganda Dennis Onyango, akimtangulia pia Rainford Kalaba wa DR Congo.
Katsande kutoka klabu maarufu Soweto ya Kaizer Chiefs naye alifanya kazi kubwa, baada ya kujipanga mbele ya mabeki wakati katika ushambuliaji.

Kikosi Kamili cha Zimbabwe
Makipa: Donovan Bernard (How Mine), Takabva Mawaya (ZPC Kariba) na Tatenda Mkuruva (Dynamos).
Mabeki: Teenage Hadebe, Lawrence Mhlanga (wote kutoka Chicken Inn), Onismor Bhasera (SuperSport Utd/Afrika Kusini), Bruce Kangwa (Azam/Tanzania), Oscar Machapa (V Club/Ivory Coast), Elisha Muroiwa (Dynamos), Costa Nhamoinesu (Sparta Prague/CZE), Hardlife Zvirekwi (CAPS Utd).

Viungo: Kudakwashe Mahachi, Danny Phiri (wote wa Golden Arrows/Afrika Kusini), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns/Afrika Kusini), Willard Katsande (Kaizer Chiefs/Afrika Kusini,nahodha), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem/Uholanzi),

Washambuliaji: Tinotenda Kadewere (Djurgardens/Sweden), Cuthbert Malajila (Wits/Afrika Kusini), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang/China), Knowledge Musona (Ostend/Ubelgiji), Tendai Ndoro (Orlando Pirates/Afrika Kusini), Evans Rusike (Maritzburg/Afrika Kusini), Mathew Rusike (CS Sfaxien/Tunisia)
Kocha wa kikosi hicho ni Kallisto Pasuwa.

Real Madrid achana nayo, yamtumia Morata kama chambo Juventus

Alvaro Morata kama chambo kwa Juventus

Paulo Dyabala anayewindwa Real Madrid
SIO Mchezo! Klabu ya Real Madrid imepanga kumtumia Alvaro Morata kama chambo cha kuweza kumnasa nyota wa kimataifa wa Juventus, Paulo Dyabala.
Inadaiwa kuwa klabu hiyo imepanga kutoa kitita cha fedha pamoja na Morata ilimradi imbeba Dybala.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Madrid imetoa ofa ya Pauni Milioni 77 sambamba na straika wake mkali aliyewahi kuichezea Juventus kwa misimu miwili ya mkataba maalum, Alvaro Morata, ili imnase Muargentina huyo anayetisha kwa mabao Italia.
Hata hivyo mabosi wa Los Blancos wamefichua kuwa wapo tayari pia kuipa Juventus ama Toni Kroos ama Luca Modric, ili mradi dili la Dybala lijipe.
Mkuregenzi wa Juventus, Giuseppe Marotta amedaiwa kugomea mipango hiyo ya Mabingwa wa Dunia, akitaka kumbakisha nyota wao huyo mwenye miaka 23 aliyekuwa miongoni mwa waliokluwa wakiwania tuzo ya Ballon d'Or.
Licha ya msimamo huo wa Blanconeri, wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A, bado hawaaminiki kwa sababu ya kuwa na kauli za kisiasa, kwani kuna wakati wanadai hawauzi mchezaji, lakini ikiwa kama njaa ya kutaka kufanya biashara yenye faida. Hata kwa Paul Pogba walinukuliwa kutoa msimamo kama huo, lakini mwishowe walimuuza kwa Man United kwa kitita kinono kinachoshikilia rekodi kwa sasa barani Ulaya.

Chelsea haitaki mchezo, yanasa kinda la zamani la Everton

Baadhi ya Wachezaji wa Chelsea
MNAHESABU lakini? Klabu ya Chelsea imeanza hesabu zake za kuimarisha kikosi chao, ikiwa ni siku chache tangu watunguliwe mabao 2-0 na Tottenham Hotspur kwa kumsainisha beki kinda wa zamani wa timu ya vijana ya  Everton, Kyle Jameson.
Kwa mujibu wa duru za kispoti zinasema Jameson, 18, amejiunga na Chelsea kama mchezaji huru kwa mkataba wa soka la kulipwa utakaoishia msimu wa 2017/18.
Beki huyo wa kati Chipukizi huyo aliwahi kushiriki Ligi ya Vijana akiwa na klabu ya Southport alianza kucheza soka katika klabu hiyo ya Merseyside kabla ya kwenda kwenye klabu za chini.
Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Chjelsea umeandika; "Mipango yetu ya kuboresha kikosi chetu tumemsainisha Kyle Jameson. Beki huyo wa kati mwenye miaka 18 hakuwa amesajiliwa kokote na amesaini nasi mkataba wa soka la kulipwa utakaoisha mwishoni mwa msimu ujao."
Jameson ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa Stamford Bridge wakati dirisha la usajili wa Januari likiwa limefunguliwa mapema wiki hii.