STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 6, 2017

Zimbabwe kakosekana Ngoma na Kamusoko tu!

Bruce Kangwa
Kikosi cha Zimbabwe 'Thje Might Warriors
HARARE, Zimbabwe
KWA mashabiki wa klabu za Simba na Yanga, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Methodi Mwanjali ni nyota wa aina yao, wanawategemea kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara. Sasa sikia hii. Wachezaji hao kwao wala si mali kitu, kwani kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe nchi wanayotokea imeita nyota wake kwa ajili ya Fainali za Afcon 2017, bila ya wachezaji hao.
Nyota Khama Billiat aliyeshika nafasi ya pili katika tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ya bara hilo, pamoja na kiungo mwenzake na nahodha Willard Katsande ni miongoni mwa wachezaji nane wanaocheza soka Afrika Kusini ambao wameitwa katika kikosi cha Zimbabwe.
Mchezaji Zimbabwe katika mashindano ya mwaka huu imepangwa katika Kundi B, ambapo watacheza na Mabingwa wa zamani Algeria na Tunisia na Senegal, wakati timu mbili za juu zitatinga robo fainali.
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Zimbabwe kushiriki fainali hizo, ambazo walitolewa katika raundi ya kwanza nchini Tunisia mwaka 2004 na kupata pigo kama hilo nchini Misri miaka miwili baadae.
Mshambuliaji wa pembeni Billiat alikuwa mchezaji muhimu aliyeisaidia timu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns wakati iliposhina taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka jana.
Pia mchezaji huyo alikuwa mmoja kati ya wachezaji watatu waliofikia hatua ya mwisho ya kumsaka mchezaji bora wa Afrika kwa timu za ndani iliyotwaliwa na kipa Mganda Dennis Onyango, akimtangulia pia Rainford Kalaba wa DR Congo.
Katsande kutoka klabu maarufu Soweto ya Kaizer Chiefs naye alifanya kazi kubwa, baada ya kujipanga mbele ya mabeki wakati katika ushambuliaji.

Kikosi Kamili cha Zimbabwe
Makipa: Donovan Bernard (How Mine), Takabva Mawaya (ZPC Kariba) na Tatenda Mkuruva (Dynamos).
Mabeki: Teenage Hadebe, Lawrence Mhlanga (wote kutoka Chicken Inn), Onismor Bhasera (SuperSport Utd/Afrika Kusini), Bruce Kangwa (Azam/Tanzania), Oscar Machapa (V Club/Ivory Coast), Elisha Muroiwa (Dynamos), Costa Nhamoinesu (Sparta Prague/CZE), Hardlife Zvirekwi (CAPS Utd).

Viungo: Kudakwashe Mahachi, Danny Phiri (wote wa Golden Arrows/Afrika Kusini), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns/Afrika Kusini), Willard Katsande (Kaizer Chiefs/Afrika Kusini,nahodha), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem/Uholanzi),

Washambuliaji: Tinotenda Kadewere (Djurgardens/Sweden), Cuthbert Malajila (Wits/Afrika Kusini), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang/China), Knowledge Musona (Ostend/Ubelgiji), Tendai Ndoro (Orlando Pirates/Afrika Kusini), Evans Rusike (Maritzburg/Afrika Kusini), Mathew Rusike (CS Sfaxien/Tunisia)
Kocha wa kikosi hicho ni Kallisto Pasuwa.

No comments:

Post a Comment