STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 6, 2017

Chelsea haitaki mchezo, yanasa kinda la zamani la Everton

Baadhi ya Wachezaji wa Chelsea
MNAHESABU lakini? Klabu ya Chelsea imeanza hesabu zake za kuimarisha kikosi chao, ikiwa ni siku chache tangu watunguliwe mabao 2-0 na Tottenham Hotspur kwa kumsainisha beki kinda wa zamani wa timu ya vijana ya  Everton, Kyle Jameson.
Kwa mujibu wa duru za kispoti zinasema Jameson, 18, amejiunga na Chelsea kama mchezaji huru kwa mkataba wa soka la kulipwa utakaoishia msimu wa 2017/18.
Beki huyo wa kati Chipukizi huyo aliwahi kushiriki Ligi ya Vijana akiwa na klabu ya Southport alianza kucheza soka katika klabu hiyo ya Merseyside kabla ya kwenda kwenye klabu za chini.
Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Chjelsea umeandika; "Mipango yetu ya kuboresha kikosi chetu tumemsainisha Kyle Jameson. Beki huyo wa kati mwenye miaka 18 hakuwa amesajiliwa kokote na amesaini nasi mkataba wa soka la kulipwa utakaoisha mwishoni mwa msimu ujao."
Jameson ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa Stamford Bridge wakati dirisha la usajili wa Januari likiwa limefunguliwa mapema wiki hii.

No comments:

Post a Comment