STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 9, 2014

Msafara wa viongozi CHADEMA watekwa nyara

http://www.gumzolajiji.com/wp-content/uploads/2014/09/SAM_7117.jpg
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama, Juma Protas
MSAFARA wa viongozi na wanachama wa chama Demokrasia na Maendeleo Chadema wa Kanda ya ziwa Magharibi wametekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wakitoka kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za serikali za Mitaa kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama, Juma Protas alisema tukio hilo lilitokea  juzi katikati ya Kijiji cha  Kalagwe kata ya Ntobo na Kijiji cha Nyambula  Kata ya Ngongwa majira ya Saa 3:30 Usiku wakati wakitoka kwenye Kampeni  Kijiji cha Kakola.
Akizungumzia tukio hilo Protas alisema walipofika eneo la Daraja walikuta magari matatu  yamesimama pembeni ambayo ni Basi la Jordan ambalo lilikuwa linatoka mkoani Geita kuelekea Kahama,Roli aina ya Fuso na Gari ndogo inayomilikiwa na Kampuni ya TBL kupitia bia ya Balimi ambayo nayo yalikuwa yametekwa.
Alisema wakati wanajaribu kuyapita magari hayo ghafla waliona Mawe na Miti ambayo ilikuwa imetandazwa barabarani  na ndipo majambazi hao waliamuru Msafara huo ambao ulikuwa na magari mawili wenye watu 10 wasimame na watoe simu na fedha walizokuwa nazo.
“Tulisikia sauti  wakisema zimeni  taa za gari na muziki na hatuwezi kuwadhuru nyinyi Makamanda ila tunataka fedha na simu, na tupo kazini mnatakiwa kuwalaumu viongozi waliokula Pesa za Escrow  bila hiyo tusingefanya haya mnayoyaona”alifafanua Protas.
Aliwataja waliokuwemo kwenye msafara huo kuwa ni mratibu wa Kanda ya ziwa mashariki Renatus  Mzemo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimali Kanda ya ziwa Magharibi, Emmanuel Mbise na Mwenyekiti wa Kamati ya Uenezi wa chama hicho Kanda hiyo Juma Protas ambaye ndiye Mwenyeki wa Chadema.
Viongozi hao  wa Chadema walikuwa wamepanda gari aina ya Toyota  Prado yenye no. T 707  BBP ambayo hata hivyo ilivunjwa baadhi ya vioo.
“Tuliibiwa fedha  tathimini zaidi ya shilingi laki tisa pamoja na simu 11 ambazo hazikufahamika mara moja thamani yake na gari yetu moja ambayo ni ya mdau alyejitolea kutusaidia ilivunjwa vioo na ile ya M4C yenyewe walisema hawawezi kuivunja maana ni wananchi walichanga kuinunua”,aliongeza Protas
“Kulikuwa na magari mengi tuliyoyakuta yametekwa na abiria walinyang’anywa simu na fedha zao, pia kulikuwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Lunguya ambaye alitekwa akiwa na pikipiki na wakamfunga  Kwenye mti pamoja na ddugu yake  na baada ya kuchukua fedha walitoweka kusikujulikana”,AliongozeaMwenyekiti huyo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi wilayani Kahama lilifika eneo hilo   baada ya kupewa taarifa na abiria waliokuwa kwenye basi ambalo lilitekwa  na kukuta majambazi hayo yakiwa yametokomea kusikojulikana  na kutoa msaada wa kiusalama kwa magari  yote na abiria waliotekwa.
MALUNDE

Simba yamalizana na beki wa Gor Mahia

OWINO (KUSHOTO) AKIWA KAZINI NA GOR MAHIA.
KLABU ya Simba imemalizana na beki David Owino wa Gor Mahia.
Uongozi wa Simba kupitia kamati yake ya usajili, imefanya mazungumzo na beki huyo na kumalizana naye, kilichobaki ni suala la kuanguka saini tu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe amesema wanachosubiri ni kumuona na kumalizana naye katika usajili.
"Kweli mazungumzo yamekwenda vizuri na Gor Mahia pia wamekubali, suala ni kukutana naye na kujua nini cha kufanya," alisema Hans Poppe.

SALEHJEMBE

Platini asema ni muda muafaka Blatter kuondoka FIFA

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02785/PlatBlat_2785870b.jpg
Mzee muda wa kuondoka FIFA, umewadia au we unaonaje? Platini (kushoto) akiteta jambo la Sepp Blatter wa FIFA
RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya, UEFA, Michel Platini amekataa kumuunga mkono Sepp Blatter au mpinzani wake Jerome Champagne katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Duniani,FIFA utakaofanyika mwakani.
Platini amedai kuwa anatumaini ataibuka mgombea mwingine wa tatu katika kinyang’anyiro hicho, ambaye huenda akamuunga mkono. 
Akihojiwa na rekodi moja nchini Ufaransa, Platini amesema anadhani muda umefika kwa Blatter ambaye anagombea kwa kipindi cha tano toka ateuliwe kwa mara ya kwanza mwaka 1998, kuondoka. 
Platini amesema alimuunga mkono Blatter mwaka 1998 kwa sababu alifikiri ni mtu sahihi kwa muda ule lakini baada ya vipindi vitano alivyoongoza anadhani ni muda muafaka wa kuleta mtu mwingine katika nafasi hiyo. 
Rais huyo wa UEFA aliendelea kudai kuwa taswira ya FIFA hivi sasa imeharibika vibaya kutokana na kshafa mbalimbali ndio maana anaona itakuwa vizuri kwa Blatter kuondoka lakini hadhani kama yeye mwenyewe anahitaji kuondoka. 
Akiulizwa nani atamuunga mkono katika uchaguzi huo, Platini amesema hana chaguo kwa wagombea wote wawili waliochaguliwa na akitegemea kujitokeza kwa mgombea mwingine katia uchaguzi huo.

Hatimaye Pele atoka Hospitalini

http://www.bnci.com.br/blog/images/2014/03/pele-esteira-4.jpg
Pele
GWIJI wa zamani wa soka duniani, Mbrazil Pele ameruhusiwa kutoka hospitali leo baada ya kupona maambukizi ya mkojo aliyopata kutokana na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe katika figo wiki tatu zilizopita. 
Katika taarifa yao madaktari wa hospitali ya Albert Einstein iliyopo jijini Sao Paulo wamedai kuwa nguli huyo kwasasa yuko hali njema hivyo hakuna umuhimu wa kuendelea kumuweka hapo. 
Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe katika figo yake Novemba 13 mwaka huu lakini alilazwa tena hospitalini hapo siku 10 baadae baada ya kupata maambukizi katika njia ya mkojo. 
Nguli huyo mwenye umri wa miaka 74 aliwahakikishia mashabiki wake kwamba bado yuko fiti katika picha ya video iliyotolewa Ijumaa iliyopita ikimuonyesha kitabasamu huku akipiga gitaa akiwa amezungukwa na familia yake.

Breaking News! Vurugu kubwa Dumila, kadhaa wajeruhiwa


Na Dunstan Shekidele, MOROGORO
WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni hii huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizo.
Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.
Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya wafugaji wa eneo hilo.
Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma matairi.
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji eneo hilo na kufanya uharibifu.
Majeruhi katika vurugu hizo wamepelekwa hospitali kwa huduma ya kwanza.
GPL

Stars Maboresho yanyolewa 2-1 Taifa


Furaha ya kupata bao la kuongoza
hekaheka katika lango la Burundi
Kosakosa langoni mwa vijana wa Intamba Murugamba
Burundi wakiwakimbiza Stars Maboresho
Stars wakiokoa hatari langoni mwao
KIKOSI cha timu ya Taifa Stars Maboresho kimeendeleza unyonge wa Tanzania mbele ya Burundi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika pambano la kirafiki na kimataifa lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa kama sehemu ya kusherehekea siku ya Uhuru wa Tanganyika.Stars Maboresho walianza kuandika bao dakika ya 11 kupitia Yusuf Rashid kabla ya Burundi kucharuka na kurejesha bao hilo dakika ya 25 kupitia Fabrice Mimimahanzwe na kwenda mapumziko wakiwa 1-1 na kipindi cha pili kuruhusu wageni kupata bao la ushindi lililovuruga 'pilau' la Uhuru.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Nassor Niyonkulu aliyemalizia krosi pasi ya kutoka kushoto mwa uwanja na kupiga mpira uliosindikizwa wavuni na kipa Aishi Manula.

Arsenal v Hull City, City wapewa kibonde FA Cup

The FA Cup third-round draw was made on Monday evening and produced some brilliant tiesRATIBA ya Rasundi ya Tatu ya michuano ya Kombe la FA nchini Uingereza imetoka kwa Arsenal kupangiwa Hully City wakati Manchester City wakipewa kibonde Sheffield Wednesday.
Mechi ra raundi zitaanza kuchezwa kati ya Januari 3 na 5 mwakani na ratiba kamili ni kama ifuatavyo;

Maromboso atoa kilio chake kwa serikaliMaromboso katika pozi tofauti
MUIMBAJI anayekuja juu nchini anayefanya kazi katika kundi la Yamoto Band, Mbwana Yusuf Kilangi 'Maromboso', ameiomba serikali na mamlaka nyingine zinazosimamia fani ya sanaa kuwashughulikia wezi wa kazi zao.
Maromboso alisema miongoni mwa wezi wanaopaswa kushughulikiwa ni wale wanaoedesha shughuli za kuchoma (burn) CD na kuingiza nyimbo za wasanii kwenye simu na vifaa vingine kwani wanawakosesha wasanii mapato.
"Tunaibiwa na wezi wamekuwa wakiachwa mitaani wakifanya shughuli hizo bila vyombo husika kuwachukulia hatua, hawa ni wezi na wanapaswa kushughulikiwa wanatunyima mapato," alisema.
Alisema wakati msanii au kundi likitumia gharama kubwa kurekodi kazi zao, wanaochoma CD na kuingiza nyimbo katika simu mitaani wanaifanya bila kulipa kodi wala gharama nyingine na kudai hiyo siyo haki.
"Watu hawa ndiyo wanaowafanya mashabiki wasisumbuke kwa sasa kununua kazi zetu kwa vile wanajua wataenda kutumia fedha kidogo tu kupoata kazi nyingi kwa mkupuo, Inauma sana," alisema.
Maromboso ni mmoja wa waimbaji wanne wanaounda kundi la Yamoto Band linalotamba na nyiumbo kama Yamoto, Nitajuta, Niseme, Inno na nyingine zinazotamba nchini wakiwa chini ya Mkubwa na Wanae.

Shamsa Ford: 2014 ulikuwa mwaka wangu


WAKATI akitarajiwa kuuza sura kwenye filamu nyingine mpya iitwayo 'Chale Mvuvi', muigizaji Shamsa Ford amefichua kuwa alikuwa na mwaka mzuri wa 2014 kiasi cha kumshukuru Mungu.
Akizungumza na MICHARAZO, Shamsa alisema hakuna mwaka aliofurahia fani yake ya uigizaji kama mwaka huu wa 2014 kutokana na kupata mafanikio makubwa kiasi cha kujivunia.
"Siyo Siri namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa na mwaka mzuri na tarajio langu ataniwezesha mwaka ujao uwe kama huu," alisema.
Shamsa alidokeza kuwa anatarajiwa kuonekana kwenye filamu mpya iitwayo 'Chale Mvuvi' aliyoigiza na wasanii kadhaa wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema mbali na yeye na Baba Haji, filamu hiyo imewashirikisha pia, Haji Kanuti na Mzee Kombora na ni filamu ya kijamii yenye mafunzo makubwa na ambayo imewaunganisha wasanii wa pande mbili za Muungano.
"Hii siyo filamu yangu, lakini nimeishiriki na Baba Haji na tumeigizia visiwani Zanzibar, siyo ya kuikosa kwani ina mafunzo makubwa kwa jamii," alisema Shamsa.

Rais Jamali Malinzi kushuhudia Fainali za Kawambwa Cup 2014

http://4.bp.blogspot.com/-Z7fNwhVuwXI/UmjeW6wwceI/AAAAAAAAO3k/pDgs26pY9EI/s1600/016.JPGRAIS wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Fainali za Mashindano ya Kombe la Kawambwa 2014 itakayochezwa Desemba 20 mjini Bagamoyo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa michuano hiyo, Masau Bwire michezo ya nusu fainali za michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kuanzia Ijumaa kwa kuzikutanisha timu za Zing Zong na Mwambao.
Pambano la pili la nusu fainali za michuano hiyo itazikutanisha timu za Mapinga heroes dhidi ya New Stars na mechi zote zitakchezwa kwenye uwanja wa Mwanakalenge mjini Bagamoyo.
Bwire alisema washindi wa mechi hizo za nusua fainali watakutana kwenye fainali itakayochezwa Desemba 20 na mgeni rasmi atakuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Alisema kuwa mbali na Malinzi pia fainali hizo zinatarajiwa kuhudhuria na viongozi wengine mbalimbali walioalikwa  na kutakuwa na michezo mimngine ya kusisimua katika kupamba fainali hizo.
Miongoni mwa michezo itakayochezwa siku hiyo ni pamoja na ile ya kuvuta kamba kwa wazee, kukimbiza kuku na kina mama kukimbia kwenye magunia mbali na burudani ya ngoma na Bongofleva.
Mshindi wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa atanyakua Kombe kubwa na zawadi wa Pikipiki huku timu nyingine zikipata vikombe na zawadi nyingine ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya michuano hiyo.

Taifa Stars, Intamba Murugamba leo Taifa

http://3.bp.blogspot.com/-w-EdmksecnQ/VHx1J8I48NI/AAAAAAAG0m4/WFsKKJIhHxw/s1600/Staz.jpg
Kikosi hiki cha Taifa Stars Maboresho kilinyukwa mabao 3-0 na Burundi katika sherehe kama hizi za Uhuru mwaka jana
KIKOSI  cha Taifa Stars Maboresho kimerejea Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa leo. Timu hiyo ambayo jana asubuhi ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) juzi kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma. Nayo timu ya Taifa ya Burundi ilitua nchini jana saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni. Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.
Katika mechi mbili zilizopita baina ya timu hiyo kwenye michezo ya kirafiki ya kimataifa Stars imeshindwa kufurukuta baada ya awali kupigwa 3-0 uwanja wa Taifa kwenye sherehe kama hizi za Uhuru kupitia Maboresho na kisha 2-0 Stars yenyewe mjini BUnjumbura, Burundi.
Je, Stars Maboresho imeimarika kuweza kulipa kisasi kwa Intamba Murugamba? Tusubiri!

Arsene Wenger apata mtetezi Arsenal

http://i3.mirror.co.uk/incoming/article4568785.ece/alternates/s615/Arsenal-v-Anderlecht.jpg
NYOTA wa zamani wa Uingereza, Gary Lineker amewaponda mashabiki wa Arsenal ambao wanamzomea meneja wa timu hiyo Arsene Wenger.
Kuna picha za video zilizotoka zikionyesha Wenger mwenye umri wa miaka 65 akizomewa na mashabiki wakati akipanga treni kufuatia Arsenal kuchapwa mabao 3-2 na Stoke City Jumamosi iliyopita.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa Mfrungaji Bora wa Kombe la Dunia, ambaye kwasasa ni mtangazaji wa michezo wa BBC aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akiwaponda mashabiki hao kwa kukosa heshima pamoja na matokeo hayo baada ya kuona picha hizo za video.
Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Britania Arsenal walikuta wakiwa nyuma kwa mabao 3-0 mpaka kufikia muda wa mapumziko.
Kocha huyo pia alijikuta katika wakati mgumu mbele ya mashabiki wa Arsenal kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Robin van Persie aipeleka Man Utd katika 3 Bora

Kitu! Van Persie akifunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo
Vijana wa Van Gaal wakishangilia bao lao
Kuna maswali tena jamaniiiii!
Van Persie akifunga bao la kwanza
MSHAMBULIAJI wa Kiholanzi, Robin van Persie usiku wa jana aliiwezesha klabu yake ya Manchester United kukwea hadi nafasi ya tatu baada ya kuisambatarisha Southampton nyumbani kwao kwa kuwafunga mabao 2-1 katika Ligi Kuu ya England.
Van Persie aliandika mabao hayo katika dakika ya 12 na 71 na kuifanya Mashetani Wekundu hao kufikisha pointi 28 na kuziengua timu za Southampton na West Ham United na kuzipa presha Manchester City na Chelsea waliopo kileleni kwa sasa.
Bao la wenyeji liliwekwa kimiani na Pelle dakika ya 31 ambalo lilikuwa la kusawazisha kabla ya 'Vijana Watakatifu' kutepeta kipindi cha pili kwa bao la pili la van Persie.


Ruvu Shooting yanyakua kifaa cha zamani cha Yanga

http://1.bp.blogspot.com/-QTFqztjc5rE/UI6VApvFw1I/AAAAAAAAagM/X22S2PtY3LM/s1600/DSC_8206.JPG
Yahya Tumbo (kushoto) akichuana na beki wa Bnadari katika Ligi Kuu ya Zanzibar hivi karibuni. Mchezaji huyo ametua Ruvu Shooting akitokea Mtende Rangers
KLABU ya Ruvu Shooting  imefanikiwa kumsainisha mkataba wa miezi 18, Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Azam, Yahya Tumbo aliyekuwa akiichezea Mtende Rangers inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar.
Tumbo, anayeongoza orodha ya wafungaji bora katika ligi ya visiwa hivyo maarufu kama Grand Malta akiwa na mabao 7 alisaini mkataba huo na Ruvu Shooting jana Jumatatu ili kuitumikia katika Ligi Kuu Bara.
Ruvu imemsajili mchezaji huyo aliyekuwa na mkataba na klabu yake inayoongoza msimamo wa ligi ya visiwani baada ya kumalizana na klabu yake pamoja na Chama cha Soka za Zanzibar, ZFA.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire alisema kuwa, wamemnyakua mchezaji huyo ili kuimarisha kikosi chake baada ya awali kumdaka Betram Mombeki aliyewahi kuichezea Simba.
'Usajili wa Tumbo, mchezaji hatari katika kufumania nyavu ni ishara kwamba timu yetu imedhamiria kufanya vizuri ligi itakapoendelea katika msimu huu," alisema Bwire.
Bwire alisema anaimani na washambuliaji hao kuwa wataibeba Ruvu katika ligi hiyo iliyosimama tangu Novemba 9 na itakayoendelea tena Desemba 26.
Tumbo ametua Ruvu akitokea Mtende Rangers iliyopo kileleni kwa sasa wakati ligi ikiwa imesimama visiwani humo  ikiwa na pointi 19 ikifuatiwa na Zimamoto yenye pointi 18, huku mshambuliaji huyo akiwa kinara wa mabao 7 akifuariwa na Amour Janja wa JKU mwenye mabao matano.
Bwire aliongeza kuwa mbali na kuwasajili wachezaji wawili, yaani Mombeki na Tumbo, pia kuna wachezaji wanne wanaoendelea kufanyiwa majaribio katika timu yao na endapo viwango vyao vitamridhisha kocha Tom Oloba watasajili kuingozea nguvu Ruvu.
Ruvu Shooting imeenda mapumziko ikiwa katika nafasi ya 11 baada ya kukusanya jumla ya pointi saba baada ya kucheza mechi saba.

Zola D avunja ukimya na I Don't CareBAADA ya kimya cha muda mrefu, Mwanahip-hop, Zola D anajiandaa kuachia 'audio' na video ya kazi yake mpya iitwayo 'I Don't Care'.
Akizungumza na MICHARAZO hivi punde, Zola D ambaye pia ni Bondia wa ngumi za kulipwa uzito wa Juu, alisema wimbo huo ambao ni wa kigumu asilia, ameimba kwa kushirikiana na Ramso Latino.
Zola D alisema kuwa kazi hiyo ameitengeneza kwa Man DVD na video chini ya kampuni yake ya 'Under Films na itaachiwa muda wowote kuanza sasa.
Ila MICHARAZO inakupa nafasi ya kuusikiliza wimbo huo kwa mara ya kwanza hapo chini;

Zola D ft Latino - I Don Care.mp3