STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 9, 2014

Shamsa Ford: 2014 ulikuwa mwaka wangu


WAKATI akitarajiwa kuuza sura kwenye filamu nyingine mpya iitwayo 'Chale Mvuvi', muigizaji Shamsa Ford amefichua kuwa alikuwa na mwaka mzuri wa 2014 kiasi cha kumshukuru Mungu.
Akizungumza na MICHARAZO, Shamsa alisema hakuna mwaka aliofurahia fani yake ya uigizaji kama mwaka huu wa 2014 kutokana na kupata mafanikio makubwa kiasi cha kujivunia.
"Siyo Siri namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa na mwaka mzuri na tarajio langu ataniwezesha mwaka ujao uwe kama huu," alisema.
Shamsa alidokeza kuwa anatarajiwa kuonekana kwenye filamu mpya iitwayo 'Chale Mvuvi' aliyoigiza na wasanii kadhaa wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema mbali na yeye na Baba Haji, filamu hiyo imewashirikisha pia, Haji Kanuti na Mzee Kombora na ni filamu ya kijamii yenye mafunzo makubwa na ambayo imewaunganisha wasanii wa pande mbili za Muungano.
"Hii siyo filamu yangu, lakini nimeishiriki na Baba Haji na tumeigizia visiwani Zanzibar, siyo ya kuikosa kwani ina mafunzo makubwa kwa jamii," alisema Shamsa.

No comments:

Post a Comment