STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 9, 2014

Hatimaye Pele atoka Hospitalini

http://www.bnci.com.br/blog/images/2014/03/pele-esteira-4.jpg
Pele
GWIJI wa zamani wa soka duniani, Mbrazil Pele ameruhusiwa kutoka hospitali leo baada ya kupona maambukizi ya mkojo aliyopata kutokana na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe katika figo wiki tatu zilizopita. 
Katika taarifa yao madaktari wa hospitali ya Albert Einstein iliyopo jijini Sao Paulo wamedai kuwa nguli huyo kwasasa yuko hali njema hivyo hakuna umuhimu wa kuendelea kumuweka hapo. 
Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe katika figo yake Novemba 13 mwaka huu lakini alilazwa tena hospitalini hapo siku 10 baadae baada ya kupata maambukizi katika njia ya mkojo. 
Nguli huyo mwenye umri wa miaka 74 aliwahakikishia mashabiki wake kwamba bado yuko fiti katika picha ya video iliyotolewa Ijumaa iliyopita ikimuonyesha kitabasamu huku akipiga gitaa akiwa amezungukwa na familia yake.

No comments:

Post a Comment