STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 9, 2014

Maromboso atoa kilio chake kwa serikaliMaromboso katika pozi tofauti
MUIMBAJI anayekuja juu nchini anayefanya kazi katika kundi la Yamoto Band, Mbwana Yusuf Kilangi 'Maromboso', ameiomba serikali na mamlaka nyingine zinazosimamia fani ya sanaa kuwashughulikia wezi wa kazi zao.
Maromboso alisema miongoni mwa wezi wanaopaswa kushughulikiwa ni wale wanaoedesha shughuli za kuchoma (burn) CD na kuingiza nyimbo za wasanii kwenye simu na vifaa vingine kwani wanawakosesha wasanii mapato.
"Tunaibiwa na wezi wamekuwa wakiachwa mitaani wakifanya shughuli hizo bila vyombo husika kuwachukulia hatua, hawa ni wezi na wanapaswa kushughulikiwa wanatunyima mapato," alisema.
Alisema wakati msanii au kundi likitumia gharama kubwa kurekodi kazi zao, wanaochoma CD na kuingiza nyimbo katika simu mitaani wanaifanya bila kulipa kodi wala gharama nyingine na kudai hiyo siyo haki.
"Watu hawa ndiyo wanaowafanya mashabiki wasisumbuke kwa sasa kununua kazi zetu kwa vile wanajua wataenda kutumia fedha kidogo tu kupoata kazi nyingi kwa mkupuo, Inauma sana," alisema.
Maromboso ni mmoja wa waimbaji wanne wanaounda kundi la Yamoto Band linalotamba na nyiumbo kama Yamoto, Nitajuta, Niseme, Inno na nyingine zinazotamba nchini wakiwa chini ya Mkubwa na Wanae.

No comments:

Post a Comment