STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 9, 2014

Ruvu Shooting yanyakua kifaa cha zamani cha Yanga

http://1.bp.blogspot.com/-QTFqztjc5rE/UI6VApvFw1I/AAAAAAAAagM/X22S2PtY3LM/s1600/DSC_8206.JPG
Yahya Tumbo (kushoto) akichuana na beki wa Bnadari katika Ligi Kuu ya Zanzibar hivi karibuni. Mchezaji huyo ametua Ruvu Shooting akitokea Mtende Rangers
KLABU ya Ruvu Shooting  imefanikiwa kumsainisha mkataba wa miezi 18, Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Azam, Yahya Tumbo aliyekuwa akiichezea Mtende Rangers inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar.
Tumbo, anayeongoza orodha ya wafungaji bora katika ligi ya visiwa hivyo maarufu kama Grand Malta akiwa na mabao 7 alisaini mkataba huo na Ruvu Shooting jana Jumatatu ili kuitumikia katika Ligi Kuu Bara.
Ruvu imemsajili mchezaji huyo aliyekuwa na mkataba na klabu yake inayoongoza msimamo wa ligi ya visiwani baada ya kumalizana na klabu yake pamoja na Chama cha Soka za Zanzibar, ZFA.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire alisema kuwa, wamemnyakua mchezaji huyo ili kuimarisha kikosi chake baada ya awali kumdaka Betram Mombeki aliyewahi kuichezea Simba.
'Usajili wa Tumbo, mchezaji hatari katika kufumania nyavu ni ishara kwamba timu yetu imedhamiria kufanya vizuri ligi itakapoendelea katika msimu huu," alisema Bwire.
Bwire alisema anaimani na washambuliaji hao kuwa wataibeba Ruvu katika ligi hiyo iliyosimama tangu Novemba 9 na itakayoendelea tena Desemba 26.
Tumbo ametua Ruvu akitokea Mtende Rangers iliyopo kileleni kwa sasa wakati ligi ikiwa imesimama visiwani humo  ikiwa na pointi 19 ikifuatiwa na Zimamoto yenye pointi 18, huku mshambuliaji huyo akiwa kinara wa mabao 7 akifuariwa na Amour Janja wa JKU mwenye mabao matano.
Bwire aliongeza kuwa mbali na kuwasajili wachezaji wawili, yaani Mombeki na Tumbo, pia kuna wachezaji wanne wanaoendelea kufanyiwa majaribio katika timu yao na endapo viwango vyao vitamridhisha kocha Tom Oloba watasajili kuingozea nguvu Ruvu.
Ruvu Shooting imeenda mapumziko ikiwa katika nafasi ya 11 baada ya kukusanya jumla ya pointi saba baada ya kucheza mechi saba.

No comments:

Post a Comment