STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 9, 2014

Platini asema ni muda muafaka Blatter kuondoka FIFA

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02785/PlatBlat_2785870b.jpg
Mzee muda wa kuondoka FIFA, umewadia au we unaonaje? Platini (kushoto) akiteta jambo la Sepp Blatter wa FIFA
RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya, UEFA, Michel Platini amekataa kumuunga mkono Sepp Blatter au mpinzani wake Jerome Champagne katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Duniani,FIFA utakaofanyika mwakani.
Platini amedai kuwa anatumaini ataibuka mgombea mwingine wa tatu katika kinyang’anyiro hicho, ambaye huenda akamuunga mkono. 
Akihojiwa na rekodi moja nchini Ufaransa, Platini amesema anadhani muda umefika kwa Blatter ambaye anagombea kwa kipindi cha tano toka ateuliwe kwa mara ya kwanza mwaka 1998, kuondoka. 
Platini amesema alimuunga mkono Blatter mwaka 1998 kwa sababu alifikiri ni mtu sahihi kwa muda ule lakini baada ya vipindi vitano alivyoongoza anadhani ni muda muafaka wa kuleta mtu mwingine katika nafasi hiyo. 
Rais huyo wa UEFA aliendelea kudai kuwa taswira ya FIFA hivi sasa imeharibika vibaya kutokana na kshafa mbalimbali ndio maana anaona itakuwa vizuri kwa Blatter kuondoka lakini hadhani kama yeye mwenyewe anahitaji kuondoka. 
Akiulizwa nani atamuunga mkono katika uchaguzi huo, Platini amesema hana chaguo kwa wagombea wote wawili waliochaguliwa na akitegemea kujitokeza kwa mgombea mwingine katia uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment