STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 3, 2015

Yanga yaenda Zimbabwe matumaini kibao, TFF yaitilia ubani

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/yanga1.jpg
Yanga Kila la Heri katika mechi yenu ya kesho dhidi ya FC Platinum
WAKATI Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi ikiwatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika, Yanga, kikosi cha timu hiyo kimeondoka leo nchini kuelekea Zimbabwe.
Yanga wameondoka leo majira ya asubuhi kuwahi pambano lao la kesho dhidi ya FC Platinum litakalochezwa kwenye Uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
Yanga wakiwa na ari kubwa wameondoka leo nchini na kuahidi kuendelea kuwapa raha watanzania kwa kupata ushindi ugenini mbele ya wachimba madini hao wa Bulawayo.
Yanga inahitaji sare ya aina yoyote na hata kama itapoteza mechi hiyo ya marudiano chini ya mabao manne inaweza kusonga mbele kwa ajili ya raundi ya pili.
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wameondoka wakisema wanaenda kupambana kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwepo miongoni mwa wawakilishi wa michuano ya kimataifa baada ya Azam, KMKM na Polisi kung'oka mapema.

Wenger, Giroud wang'ara England, watwaa tuzo

LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ametangazwa kuwa kocha wa mwezi wa Ligi Kuu ya England na mshambuliaji Olivier Giroud akiwa mchezaji wa mwezi.Gi

Arsenal ilishinda mecwon four successive Premier League ghi nne mfululizo za Ligi Kuu mwezi Machi, ikifunga mabao tisa na kufungwa mawili tu.

Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Giroud alifunga mara tano, wakati Newcastle ilipocheza dhidi ya Everton, QPR na  West Ham.

Hii ni mara ya 14 Wenger, mwenye umri wa miaka 65, kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi katika miaka yake 19 ya kuifundisha Arsenal.

Arsenal kwa sasa iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wakati zikiwa zimebaki mechi nane kabla ya ligi hiyo haijafikia mwisho.

Timu hiyo iko pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, ambao wana mchezo mmoja mkononi.

The Gunners itawakaribisha Liverpool iliyopo katika nafasi ya tano kwenye uwanja wa Jumamosi.

Mechi zilizobaki za Arsenal za nyumbani ni pamoja na ile dhidi ya Chelsea itakayofanyika Aprili 26 na safari ya Manchester United iliyopo katika nafasi ya nne Mei 17.

SPURS YAJIANDAA KUMTEMA ADEBAYOR

https://spursstatman.files.wordpress.com/2013/04/emmanuel-adebayor.jpgKLABU ya Tottenham Hotspurs inajipanga kumlipa Emmanuel Adebayor ili hatimaye waachane naye katika kipindi cha majira ya kiangazi. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Togo amekuwa hana namba katika kikosi cha kwanza cha Spurs, huku yeye pamoja na meneja wa timu hiyo Mauricio Pochettino wakifurahishwa na hatua hiyo pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa. 
Lakini tatizo kubwa linatarajiwa kuwa mshahara wake, kwani mshambuliaji huyo hayuko tayari kuchukua chini ya kiasi cha paundi milioni 5.2 kabla ya kuondoka. 
Hata hivyo, Spurs sasa wako tayari kulipa asilimia fulani ya mshahara wa Adebayor msimu ujao ili kuhakikisha anaondoka klabu kwao. 
Adebayor anatarajia kuingia miezi 12 ya mwisho katika mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na anatarajiwa kuwekwa sokoni kwa mkopo au kwa dili la moja kwa moja.
Kabla ya kuchemesha mshambuliaji huyo alikuwan tegemeo White Hart Lane kwa kufunga mabao muhimu, hata hivyo kazi hiyo kwa sasa inafanywa na Harry Kane.

Jennifer Mgendi andaa Tamasha la Kumshukuru Mungu

 
MIAKA 20 si mchezo, hasa katika huduma ya uimbaji. Ndivyo ambavyo mwanadada mkali wa muziki wa Injili, Jennifer Mgendi amepanga kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kufikisha umri huo katika huduma hiyo na kulihubiri Neno kwa njia ya nyimbo.
Jennifer alisema anatarajia kufanya Tamasha la Shukrani ya Miaka 20 ya Uimbaji wake siku ya uzinduzi wa video ya albamu yake mpya ya 'Wema ni Akiba'.
Muimbaji huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu, alisema uzinduzi huo utakaoenda na tamasha hilo utafanyika June 28 katika Kanisa la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) lililopo Tabata Shule, Dar es Salaam.
Jennifer alisema ni wajibu wake kumshukuru Mungu kwa wema aliyomfanyia katika miaka hiyo 20 akiwa ametoa albamu nane, mpya ikiwa ni 'Wema ni Akiba' aliyoiachia wiki iliyopita ikiwa na nyimbo saba.
Miongoni mwa nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni; 'Nakugonja' alioimba na Mchungaji Abiudi Misholi na 'Wema ni Akiba' ambao unasumbua hewani tangu auachie mapema mwaka huu.
"Ni lazima nimshukuru Mungu kwa ukarimu na wema wake alionifanyia kuweza kumudu ndani ya huduma ya uimbaji kwa miaka 20 nikiwa nimetoa albamu nane na filamu kadhaa," alisema Jennifer.

VUMBI LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI HII

Kagera Sugar
JKT Ruvu
Ruvu Shooting
Ndanda FC itaialika Mbeya City

Coastal wanawakaribisha vibonde Prisons-Mbeya

Simba watakuwa Shinyanga kujiuliza kwa Kagera Sugar
VUMBI la Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo sita. Minne ikichezwa kesho Jumamosi na miwili siku ya Jumapili.
Simba wanaopigana kuingia kwenye Mbili Bora wapo ugenini kukabiliana na Kagera Sugar katika mechi ya kisasi itakayochezwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Kagera iliyotoka kuifumua Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 juzi kwenye uwanja huo, imeapa kuishikisha adabu Simba ikitaka kufuata nyayo za Stand United.
Stand iliitambia Simba kwa kuilaza bao 1-0 katika mechi baina yao iliyochezwa Februari mwaka huu.
Hata hivyo Simba kupitia Msemaji wakem, Haji Manara ametamba kuwa kikosi chao kipo kamili kutoa kichapo kesho Jumamosi.
Mbali na mechi hiyo pia kesho kuna michezo miwili mitatu jijini Tanga Coastal Union watawakaribisha maafande wa Magereza, Prisons-Mbeya kwenye Uwanja wa Mkwakwani. 
Ndanda wenyewe watakuwa nyumbani mjini Mtwara kuwakaribisha Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona na maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatini huko Mlandizi, Pwani.
Jumapili Stand United watakuwa nyumbani kuialika Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage na Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Msimamo wa Ligi hiyo unaonyesha kuwa Yanga waliopo ugenini nchinio Zimbabwe wanaongoza wakiwa na pointi 40 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 36 na Simba wanakamata nafasi ya tatu na pointi zao 32 kisha Kagera Sugar wenye pointi 28.
 MSIMAMO WA LIGI ULIVYO KWA SASA:                      P     W      D    L    F      A     Pts
1. Yanga        19    12    04   03  28    11    40
2. Azam FC    18    10    06   02  25    12    36
3. Simba        20    08    08   04  25    14    32
4. Kagera       20    07    07   06  18    18    28
5. Coastal      20    05    09   06  14    14    24
6. JKT Ruvu   20    06    06   08   16    19    24
7. Mgambo    19    07    03   09   13    19    24
8. Mtibwa      19    05    08   06   19    19    23
9. Mbeya City 19   05    08   06    14    16    23
10.Ruvu        18    05    08   05    12    16    23
11. Ndanda    20   06    05   09    17    23    23
12. Stand       19   05    06   08    14    23    21
13. Polisi Moro20   04    09   07    13    17    21
14. Prisons     18   02    11   05    13    20    17

Kiongozi Simba ainyima Simba ubingwa

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/Kikosi-cha-Simba1.jpg
Kikosi cha Simba
SIMBA iwe bingwa, nani kasema? Labda kama itakomalia kuwania nafasi ya pili, ili kupata nafasi ya uwakilishi wa michuano ya kimataifa mwakani.
Katibu Mwenezi wa zamani wa Simba, Said 'Seydou' Rubeya, aliliambia MICHARAZO kuwa, kwa Simba hii ni ngumu kuweza kutwaa ubingwa.
Seydou alisema kuwa, ni kweli Simba inafanya vema baada ya kusuasua mwanzoni mwa msimu, lakini haiwezi kurejesha taji ililolitema msimu wa 2012-2013 kwa watani zao Yanga na Azam kulinyakua msimu uliopita.
"Simba haina safu ya ushambuliaji, inamtegemea Emmanuel Okwi pekee yake, hilo ni jambo linaloiangusha timu, japo kocha Goran Kopunovic ameibadilisha mno timu kwa kipindi kifupi," alisema Seydou.
"Kwa nafasi ya pili inawezekana kama wachezaji watapambana kiume, ila kwa ubingwa siyo rahisi kwa Simba hii, ni lazima tujipange vema kwa msimu ujao ili turejeshe makali yetu za zamani," aliongeza.
Seydou aliyejiweka kando kwa masuala ya michezo, tangu aondoke uongozini  chini ya Mwenyekiti wake Hassan Dalali 'Field Marshal', aliwataka wachezaji wa Simba kuacha 'utoto' uwanjani kuisaidia timu.
Alisema baadhi ya chipukizi waliong'ara msimu uliopita wamebweteka na mara nyingi wamekuwa wakifanya utoto dimbani unaoigharimu Simba na kuwataka kuamka ili kuisaidia timu kurejesha heshima yake.

Owino ajiweka sokoni kiaina


AMEJIWEKA sokoni. Beki wa kimataifa wa Simba, Joseph Owino amesema bado hajaamua hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Akiwa ni mmoja wa nyota wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu, Owino alisema itategemea kama abaki Simba au arejee kwao Uganda.
Akaweka bayana kwamba kama itajitokeza klabu itakayompa ofa nzuri atabaki Tanzania ili kuendelea kucheza katika Ligi Kuu.
"Itategemea hapo baadaye, ila ikitokea klabu ikanipa ofa nzuri nitabaki Bongo," alisema beki huyo aliyeichezea Azam.
Kwa muda mrefu sasa, Owino amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Goran Kopunovic.
Mbali na Owino wengine wanaomaliza mikataba Msimbazi ni; Said Ndemla, William Lucian 'Gallas', kipa Ivo Mapunda, Nassor Masoud 'Chollo', Ibrahim Twaha 'Messi' na Abdallah Seseme ambaye baba yake mzazi amefichua kuwa hawezi kubaki Simba kwa vile klabu tatu za Mwadui, Kagera Sugar na Coastal Union zinamtaka na zimeanza kuzungumza naye.