STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 3, 2015

VUMBI LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI HII

Kagera Sugar
JKT Ruvu
Ruvu Shooting
Ndanda FC itaialika Mbeya City

Coastal wanawakaribisha vibonde Prisons-Mbeya

Simba watakuwa Shinyanga kujiuliza kwa Kagera Sugar
VUMBI la Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo sita. Minne ikichezwa kesho Jumamosi na miwili siku ya Jumapili.
Simba wanaopigana kuingia kwenye Mbili Bora wapo ugenini kukabiliana na Kagera Sugar katika mechi ya kisasi itakayochezwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Kagera iliyotoka kuifumua Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 juzi kwenye uwanja huo, imeapa kuishikisha adabu Simba ikitaka kufuata nyayo za Stand United.
Stand iliitambia Simba kwa kuilaza bao 1-0 katika mechi baina yao iliyochezwa Februari mwaka huu.
Hata hivyo Simba kupitia Msemaji wakem, Haji Manara ametamba kuwa kikosi chao kipo kamili kutoa kichapo kesho Jumamosi.
Mbali na mechi hiyo pia kesho kuna michezo miwili mitatu jijini Tanga Coastal Union watawakaribisha maafande wa Magereza, Prisons-Mbeya kwenye Uwanja wa Mkwakwani. 
Ndanda wenyewe watakuwa nyumbani mjini Mtwara kuwakaribisha Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona na maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatini huko Mlandizi, Pwani.
Jumapili Stand United watakuwa nyumbani kuialika Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage na Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Msimamo wa Ligi hiyo unaonyesha kuwa Yanga waliopo ugenini nchinio Zimbabwe wanaongoza wakiwa na pointi 40 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 36 na Simba wanakamata nafasi ya tatu na pointi zao 32 kisha Kagera Sugar wenye pointi 28.
 MSIMAMO WA LIGI ULIVYO KWA SASA:                      P     W      D    L    F      A     Pts
1. Yanga        19    12    04   03  28    11    40
2. Azam FC    18    10    06   02  25    12    36
3. Simba        20    08    08   04  25    14    32
4. Kagera       20    07    07   06  18    18    28
5. Coastal      20    05    09   06  14    14    24
6. JKT Ruvu   20    06    06   08   16    19    24
7. Mgambo    19    07    03   09   13    19    24
8. Mtibwa      19    05    08   06   19    19    23
9. Mbeya City 19   05    08   06    14    16    23
10.Ruvu        18    05    08   05    12    16    23
11. Ndanda    20   06    05   09    17    23    23
12. Stand       19   05    06   08    14    23    21
13. Polisi Moro20   04    09   07    13    17    21
14. Prisons     18   02    11   05    13    20    17

No comments:

Post a Comment