STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 3, 2015

Jennifer Mgendi andaa Tamasha la Kumshukuru Mungu

 
MIAKA 20 si mchezo, hasa katika huduma ya uimbaji. Ndivyo ambavyo mwanadada mkali wa muziki wa Injili, Jennifer Mgendi amepanga kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kufikisha umri huo katika huduma hiyo na kulihubiri Neno kwa njia ya nyimbo.
Jennifer alisema anatarajia kufanya Tamasha la Shukrani ya Miaka 20 ya Uimbaji wake siku ya uzinduzi wa video ya albamu yake mpya ya 'Wema ni Akiba'.
Muimbaji huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu, alisema uzinduzi huo utakaoenda na tamasha hilo utafanyika June 28 katika Kanisa la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) lililopo Tabata Shule, Dar es Salaam.
Jennifer alisema ni wajibu wake kumshukuru Mungu kwa wema aliyomfanyia katika miaka hiyo 20 akiwa ametoa albamu nane, mpya ikiwa ni 'Wema ni Akiba' aliyoiachia wiki iliyopita ikiwa na nyimbo saba.
Miongoni mwa nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni; 'Nakugonja' alioimba na Mchungaji Abiudi Misholi na 'Wema ni Akiba' ambao unasumbua hewani tangu auachie mapema mwaka huu.
"Ni lazima nimshukuru Mungu kwa ukarimu na wema wake alionifanyia kuweza kumudu ndani ya huduma ya uimbaji kwa miaka 20 nikiwa nimetoa albamu nane na filamu kadhaa," alisema Jennifer.

No comments:

Post a Comment