STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 3, 2015

Kiongozi Simba ainyima Simba ubingwa

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/Kikosi-cha-Simba1.jpg
Kikosi cha Simba
SIMBA iwe bingwa, nani kasema? Labda kama itakomalia kuwania nafasi ya pili, ili kupata nafasi ya uwakilishi wa michuano ya kimataifa mwakani.
Katibu Mwenezi wa zamani wa Simba, Said 'Seydou' Rubeya, aliliambia MICHARAZO kuwa, kwa Simba hii ni ngumu kuweza kutwaa ubingwa.
Seydou alisema kuwa, ni kweli Simba inafanya vema baada ya kusuasua mwanzoni mwa msimu, lakini haiwezi kurejesha taji ililolitema msimu wa 2012-2013 kwa watani zao Yanga na Azam kulinyakua msimu uliopita.
"Simba haina safu ya ushambuliaji, inamtegemea Emmanuel Okwi pekee yake, hilo ni jambo linaloiangusha timu, japo kocha Goran Kopunovic ameibadilisha mno timu kwa kipindi kifupi," alisema Seydou.
"Kwa nafasi ya pili inawezekana kama wachezaji watapambana kiume, ila kwa ubingwa siyo rahisi kwa Simba hii, ni lazima tujipange vema kwa msimu ujao ili turejeshe makali yetu za zamani," aliongeza.
Seydou aliyejiweka kando kwa masuala ya michezo, tangu aondoke uongozini  chini ya Mwenyekiti wake Hassan Dalali 'Field Marshal', aliwataka wachezaji wa Simba kuacha 'utoto' uwanjani kuisaidia timu.
Alisema baadhi ya chipukizi waliong'ara msimu uliopita wamebweteka na mara nyingi wamekuwa wakifanya utoto dimbani unaoigharimu Simba na kuwataka kuamka ili kuisaidia timu kurejesha heshima yake.

No comments:

Post a Comment