STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 3, 2015

Owino ajiweka sokoni kiaina


AMEJIWEKA sokoni. Beki wa kimataifa wa Simba, Joseph Owino amesema bado hajaamua hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Akiwa ni mmoja wa nyota wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu, Owino alisema itategemea kama abaki Simba au arejee kwao Uganda.
Akaweka bayana kwamba kama itajitokeza klabu itakayompa ofa nzuri atabaki Tanzania ili kuendelea kucheza katika Ligi Kuu.
"Itategemea hapo baadaye, ila ikitokea klabu ikanipa ofa nzuri nitabaki Bongo," alisema beki huyo aliyeichezea Azam.
Kwa muda mrefu sasa, Owino amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Goran Kopunovic.
Mbali na Owino wengine wanaomaliza mikataba Msimbazi ni; Said Ndemla, William Lucian 'Gallas', kipa Ivo Mapunda, Nassor Masoud 'Chollo', Ibrahim Twaha 'Messi' na Abdallah Seseme ambaye baba yake mzazi amefichua kuwa hawezi kubaki Simba kwa vile klabu tatu za Mwadui, Kagera Sugar na Coastal Union zinamtaka na zimeanza kuzungumza naye.

No comments:

Post a Comment