STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 3, 2016

Kweli imebaki Stori kwa Rich Mavoko (Official Video )

Ngeleja wenzake wapewa kifyagio na Malinzi

http://www.theworldfolio.com/img_db/timthumb.php?src=img_db/old/13226688671.jpg&w=800&z=1
Mhe. Ngeleja
http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/2841132/medRes/1098071/-/un1399/-/Jamal+Malinzi.jpg
Malinzi
MAJUZI Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, walichagua uongozi mpya wa timu yao ya Bunge Sports Club na kama zali, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja akaukwaa Uenyekiti kilaini bila kupingwa, jambo hilo limemvutia sana Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi.
Rais huyo wa TFF amepongeza uongozi wa timu hiyo uliochaguliwa mjini Dodoma, ambapo Ngeleja alitwaa kiti akimrithi Idd Azan ambaye alishindwa kurudi bungeni katika Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa 2015.
Mbali na Ngeleja, wengine waliopewa kifyagio hicho na Malinzi ni Makamu Mwenyekiti, Esther Matiko; Meneja wa Klabu, John Kadutu pamoja Wajumbe Neema Mgaya, Faida Bakari,  Cosato Chumi, Anna Lupembe na Grace Kihwelu.Malinzi amewatakia kila la kheri Bunge Sports Club na kuwaahidi ushirikiano kutoka TFF katika kuendeleza klabu yao na michezo kwa ujumla nchini.

Kwa Buku 5 tu inaiona Stars, VIP nako bwerere Taifa

MSHINDWE wenyewe. Viingilio vya kuliona pambano la kuwania kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mafarao wa Misri zimewekwa hadharani.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio hivyo, ambapo kile cha bei ya chini kabisa ni buku tano tu. (Sh 5,000) wakati cha juu kikiwa ni Sh. 10,000. Mnataka nini tena?!
TFF ni kama kimesikia kilio cha mashabiki wa soka, kwa kutangaza viingilio hivyo katika mchezo huo wa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mwanangu toroka uje kwa sababu tiketi zimeanza kuuzwa mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
TFF imesema watakaolipa Buku 5 watakaa mzunguko wa viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu, wakati wanene wanaotaka kukaa kibosibosi yaani VIP B na C wenyewe watatoboka kiduchu kwa Mwekundu mmoja (Sh. 10,000).
Sasa unajua tiketi zenyewe zinapatikana wapi, wala usikonde ukienda Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam utapata, pale  Ukumbi wa Burudani Mbagala Dar Live, Vituo cha mafuta cha Oilcom - Ubungo na Buguruni (Buguruni Shell) na Ofisi za Ukumbi wa burudani Bilicanas, nako utapata.
Halafu hata kesho Jumamosi Juni 4, 2016 tiketi zitauzwa kwenye vituo hivyo na vingine vya Mwenge, Mnazi Mmoja, Makumbusho, Chang’ombe na Mgahawa wa Brake Point ulioko mkabala makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Unangoja nini mwanangu, changamka bhana!

Maskini Muhammad Ali! Alazwa tena hospitalini

https://i.ytimg.com/vi/C_fEIVwjrew/maxresdefault.jpg
Muhammad Ali katika moja ya mapambano yake akimuadhibu mpinzani wake aliyelala sakafuni.
UNAMKUMBUKA Bingwa wa Dunia wa Masumbwi uzani wa juu wa zamani Muhammad Ali? Ni hivi. Jamaa huyo aliyewatetemesha mabondia wenzake amelazwa hospitalini kufuatia maambikizi ya mapafu.
Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa katika hali wastani alipolazwa hospitalini.
Hata hivyo familia yake ilipendekeza alazwe hospitali kama tahadhari kwa sababu mbali na maambukizi hayo Ali anaugua kiharusi.
Bondia huyo alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu mchezo huo wa ngumi za kulipwa.
Mara ya mwisho bondia huyo mkongwe alipolazwa hospitalini ilikuwa ni Januari mwaka uliopita baada ya kupatwa maambukizi ya njia ya mkojo.
Msemaji wa familia yake hata hivyo hakuwaambia wanahabari alikolazwa wala alilazwa lini.
Chanzo: BBC Swahili

Mkwasa aahidi raha Taifa, tunasubiri nini twendeni uwanjani

Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa

TWENDENI Taifa kesho Jumamosi, kwani Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameahidi kuifanyizia Mafarao wa Misri katika pambano lao la kuwania Afcon 2017.
Stars kesho inashuka dimbani kucheza na Misri ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-0 iliyopata kwenye mchezo wa awali uliochezwa mji wa Alexandria, katika ufunguzi wa mechi za Kundi G.
Stars  inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu AFCON ya mwakani wakati Misri wao sare itawafanya wafikishe pointi nane ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye kundi lao.
Endapo Tanzania itashinda mchezo huo itafikisha pointi nne kwani hadi sasa ina pointi moja baada ya sare ya 0-0 na Nigeria nyumbani huku ikibakisha mchezo wa marudiano na Nigeria ugenini baadaye Septemba mwaka huu..
Kundi hili baada ya kujitoa kwa Chad limebaki na timu tatu ambazo ni Misri wenye pointi saba, Nigeria pointi nne na Tanzania yenye inashika mkia ikiwa na  pointi moja lakini Misri na Nigeria zimebakiza mchezo mmoja mmoja, wakati Tanzania ina faida ya mechi mbilim huu wa leo na mwingine ni dhidi ya Nigeria utakaochezwa Septemba.
Akizungumza na Wanahabari Kocha Mkwasa alisema mchezo wa keshoni  mgumu kwani ni sawa na fainali hivyo wanahitaji kushinda ili kujiweka pazuri kwani Misri wanakuja wakihitaji sare.
“Wachezaji wako vizuri, wako kwenye morali nzuri na tumefanya mazoezi na wachezaji wote 26 na mimi nimefanya marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo dhidi ya Kenya na kinachosubiriwa ni dakika 90 tu”, alisema Mkwasa.
Pia Mkwasa alisema anatambua Misri ni timu nzuri kwani waliifunga Tanzania mabao 3-0 kwao na anajua wanakuja kucheza mfumo wa kujilinda kuliko kushambulia kama ilivyo desturi kwa timu za kiarabu lakini wao wamejiandaa kushambulia.
“Tuna deni kubwa kwa watanzania hivyo tunajua tunatakiwa kupata matokeo mazuri ili kuwapa faraja na kufufua matumaini ya kwenda AFCON hivyo tutashambulia sana”, alisema Mkwasa
Mkwasa aliwashukia watu wanaojiita wachambuzi wa soka akisema wamekuwa wakiwavunja moyo wachezaji na kuwataka waangalie namna wanavyofanya uchambuzi kwani wanawakatisha tamaa wachezaji na kuwaasa uchambuzi mzuri ni ule ambao unafanywa baada ya mchezo.

Manji amkimbiza Alloyce Komba Kamati ya Uchaguzi ya TFF

Alloyce Komba

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi  ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Aloyce Komba, amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi wa klabu Yanga uliopangwa kufanyika Juni 25 , mwaka huu.
Hatua hii imekuja baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kumtuhumu kumhujumu hivyo anakaa pembeni kupisha uchunguzi
Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Komba alisema Manji anasema nahusika kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili akate  jina lake na tuhuma hizi kwake ni nzito ukizingatia taaluma yake ya sheria.
“Manji ananituhumu mimi kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili nikate jina lake, tuhuma hizi kwangu ni nzito ukizingatia taaluma yangu ya sheria, sitaki kuwa chanzo cha mgogoro Yanga”, alisema Komba
Pia Komba alisema wanasheria nguli Said El Maamry, Alex Mgongolwa,  Mapande na baadhi ya wabunge ni watu anaowaheshimu na wamemshauri juu ya suala hili hivyo kwa busara ameamua kukaa pembeni uchaguzi ufanyike.
 “Sauti zinazosemwa sizitambui, sizijui, halafu najiuliza  wanapanga kwa manufaa ya nani? Kwanini Manji katishika kuchukua fomu TFF wakati ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza Yanga?”, alihoji Komba.
Komba alisema alitegemea Manji angemrahisishia kazi lakini matokeo yake anachafuka kwa vitu ambavyo si vya kweli.
Mchakato wa uchaguzi TFF unaendelea chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Domina Mideli, ingawa uongozi wa Yanga nao unaendesha zoezi lao makao makuu kabla ya kufanya uchaguzi wao Juni 11.

UEFA Euro Cup 2016 itakuwa tamu si mchezo


http://www.uefa.com/MultimediaFiles/Photo/competitions/General/02/35/95/19/2359519_w2.jpg 
http://i4.irishmirror.ie/incoming/article7002411.ece/ALTERNATES/s1200/Screen-Shot-2015-12-12-at-185759.png 
http://e2.365dm.com/16/05/768x432/marcus-rashford-england_3476376.jpg?20160531141444
Rashford
http://talksport.com/sites/default/files/tscouk_old_image/cristiano-ronaldo_2.jpg
Ronaldo atafanya nini safari hii huko Ufaransa

MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 'UEFA Euro 2016' itaanza wiki ijayo nchini Ufaransa kwa kushuhudiwa nyota wa nchi mbalimbali barani humo wakionyeshana kazi mpaka Julai 10 atakapopatikana bingwa wake.
Hispania ndio watetezi wa taji hilo ikilishikilia kwa mihula miwili mfululizo tangu mwaka 2008 na kutetea mwaka 2012.
Michuano hiyo itafanyika huku kukiwa na rekodi kadhaa ambazo zinahitajiwa kuvunjwa ikiwamo ya mchezaji alitefunga mabao mengi katika fainali moja, iliyowekwa na aliyekuwa nyota wa Ufaransa, Michel Platini mwaka 1984.
Katika michuano hiyo Platini aliyekuwa Rais wa Uefa kabla ya kufungiwa na FIFA kwa tuhuma za kifisadi, alifunga mabao 9, huku pia akitupia hat-trick mbili ikiwa ni rekodi tena zilizofululiza, mbali na bao la mapema la michuano la dakika 18.

Unajua kuwa ni nchi mbili tu za Ujerumani na Hispania ndizo zilizotwaa mara nyingi, zikifanya hivyo mara tatu kila moja, hivyo ni wakati wao wa kuzidiana ujanja au kuzubaa na kukutwa na Ufaransa inayowafukizia ikitwaa mara mbili tangu michuano ilipoasisiwa mwaka 1960.
Pia michuano hiyo ilimpa ujiko Cristiano Ronaldo mwaka 2004 alipokuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza fainali akifanya hivyo mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 na siku 150.
Kwa kifupi kina Marcus Rashford na makinda wenzake wanapaswa kufanya mambo ili kufikia rekodi mbalimbali ambazo zimedumu kwa miaka mingi bila kuvunjwa.

Samatta akimaliza kazi Taifa, kupewa kiwanja chake Mkuranga

Na Rahma Junior
MBWANA Samatta kesho Jumamosi ataiongoza Taifa Stars kuvaana na Misri, kwenye pambano la kuwania kwenda Gabon katika fainali za Afcon 2017, lakini Jumapili atakuwa katika sherehe moja kamambe.
Nahodha huyo wa Stars, atakuwa anakabidhiwa  kiwanja cha ekari tano kilichopo kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib 'Teacher' alisema  jijini Dar es Salaam kuwa maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.
Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao.
Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa.
Taalib alisema mtandao  huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.
Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.
Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya Naibu wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu.
Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.
Wageni wengine walioalikwa kwenye sherehe hizo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi viongozi wa Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii maarufu nchini.

Hivi ndivyo Copa America 2016 itakavyopigwa USA kuanzia leo

http://www.concacaf.com/wp-content/uploads/2015/10/16_CAC_GEN_GGL.jpg
#no.DateTime in ISTMatchScore
104-06-201607:00amUSA vs Colombia--
205-06-201602:30amCosta Rica vs Paraguay--
305-06-201605:00amHaiti vs Peru--
405-06-201607:30amBrazil vs Ecuador--
506-06-201602:30amJamaica vs Venezuela--
606-06-201605:30amMexico vs Uruguay--
707-06-201604:30amPanama vs Bolivia--
807-06-201607:30amArgentina vs Chile--
908-06-201605:30amUSA vs Costa Rica--
1008-06-201608:00amColombia vs Paraguay--
1109-06-201605:00amBrazil vs Haiti--
1209-06-201607:30amEcuador vs Peru--
1310-06-201605:00amUruguay vs Venezuela--
1410-06-201607:30amMexico vs Jamaica--
1511-06-201604:30amChile vs Bolivia--
1611-06-201607:00amArgentina vs Panama--
1712-06-201604:30amUSA vs Paraguay--
1812-06-201606:30amCosta Rica vs Colombia--
1913-06-201604:00amEcuador vs Haiti--
2013-06-201605:00amBrazil vs Peru--
2114-06-201605:30amMexico vs Venezuela--
2214-06-201607:30amUruguay vs Jamaica--
2315-06-201605:30amPanama vs Chile--
2415-06-201607:30amArgentina vs Bolivia--

2016 Copa America Centenario Quarter Final Match

#no.DateTime in ISTMatchScoreWinner
2517-06-201607:00amGroup A1  vs Group B2--
2618-06-201605:30amGroup B1 vs Group A2--
2719-06-201604:30amGroup D1 vs Group C2--
2819-06-201607:30amGroup C1 vs Group D2--

2016 Copa America Centenario Semi Final Match Schedule

#no.DateTime in ISTMatchScoreWinner
2922-06-201606:30amWinner M25 vs Winner M27--
3023-06-201605:30amWinner M26 vs Winner M28--

2016 Copa America Centenario Final Match Schedule

#no.DateTime in ISTMatchScoreWinner
3126-06-201605:30amLooser M29 vs Looser M30--
3227-06-201605:30amWinner M29 vs Winner M30--

Liverpool asikuambie mtu baba'ake imepania si utani!

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2016/05/emre-mor-1463896209-800.jpgKLABU ya Liverpool ambayo ilikaribia kutwaa taji la UEFA Europa League kama sio kuteleza kwa Sevilla ya Hispania, imedaiwa inaongoza mbio za kuwania saini ya chipukizi wa kimataifa wa Uturuki na klabu ya Nordsjaelland, Emre Mor.
Mor mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia Ulaya kwasasa baada ya kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Denmark na kumfanya kuitwa katika kikosi cha Uturuki kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 inayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
Klabu za Manchester United, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam nazo zinatajwa kuwa zinamwania chipukizi huyo anayemudu kiungo mshambuliaji lakini Liverpool ndio inaelezwa kuwa inaongoza mbio hizo.
Dogo huyo amefunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili mechi 13 alizoichezea klabu yake msimu huu.