STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 3, 2016

Manji amkimbiza Alloyce Komba Kamati ya Uchaguzi ya TFF

Alloyce Komba

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi  ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Aloyce Komba, amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi wa klabu Yanga uliopangwa kufanyika Juni 25 , mwaka huu.
Hatua hii imekuja baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kumtuhumu kumhujumu hivyo anakaa pembeni kupisha uchunguzi
Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Komba alisema Manji anasema nahusika kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili akate  jina lake na tuhuma hizi kwake ni nzito ukizingatia taaluma yake ya sheria.
“Manji ananituhumu mimi kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili nikate jina lake, tuhuma hizi kwangu ni nzito ukizingatia taaluma yangu ya sheria, sitaki kuwa chanzo cha mgogoro Yanga”, alisema Komba
Pia Komba alisema wanasheria nguli Said El Maamry, Alex Mgongolwa,  Mapande na baadhi ya wabunge ni watu anaowaheshimu na wamemshauri juu ya suala hili hivyo kwa busara ameamua kukaa pembeni uchaguzi ufanyike.
 “Sauti zinazosemwa sizitambui, sizijui, halafu najiuliza  wanapanga kwa manufaa ya nani? Kwanini Manji katishika kuchukua fomu TFF wakati ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza Yanga?”, alihoji Komba.
Komba alisema alitegemea Manji angemrahisishia kazi lakini matokeo yake anachafuka kwa vitu ambavyo si vya kweli.
Mchakato wa uchaguzi TFF unaendelea chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Domina Mideli, ingawa uongozi wa Yanga nao unaendesha zoezi lao makao makuu kabla ya kufanya uchaguzi wao Juni 11.

No comments:

Post a Comment