STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 3, 2016

Kwa Buku 5 tu inaiona Stars, VIP nako bwerere Taifa

MSHINDWE wenyewe. Viingilio vya kuliona pambano la kuwania kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mafarao wa Misri zimewekwa hadharani.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio hivyo, ambapo kile cha bei ya chini kabisa ni buku tano tu. (Sh 5,000) wakati cha juu kikiwa ni Sh. 10,000. Mnataka nini tena?!
TFF ni kama kimesikia kilio cha mashabiki wa soka, kwa kutangaza viingilio hivyo katika mchezo huo wa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mwanangu toroka uje kwa sababu tiketi zimeanza kuuzwa mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
TFF imesema watakaolipa Buku 5 watakaa mzunguko wa viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu, wakati wanene wanaotaka kukaa kibosibosi yaani VIP B na C wenyewe watatoboka kiduchu kwa Mwekundu mmoja (Sh. 10,000).
Sasa unajua tiketi zenyewe zinapatikana wapi, wala usikonde ukienda Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam utapata, pale  Ukumbi wa Burudani Mbagala Dar Live, Vituo cha mafuta cha Oilcom - Ubungo na Buguruni (Buguruni Shell) na Ofisi za Ukumbi wa burudani Bilicanas, nako utapata.
Halafu hata kesho Jumamosi Juni 4, 2016 tiketi zitauzwa kwenye vituo hivyo na vingine vya Mwenge, Mnazi Mmoja, Makumbusho, Chang’ombe na Mgahawa wa Brake Point ulioko mkabala makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Unangoja nini mwanangu, changamka bhana!

No comments:

Post a Comment