STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 10, 2014

Mpiga Drums Extra Bongo awashtua Wajumbe Bunge la Katiba

Mpogoro Machine akikaanga chipa mazoezi ya Extra Bongo
MPIGA dramu wa bendi ya Extra Bongo 'Wana Kimbembe', Wenceslaus Chitalula 'Mpogoro Machine', amewaomba Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kufanya kile walizotumwa na wananchi.
Mwanamuziki huyo alisema malumbano na muda unaopotezwa na wajumbe hao kwenye bunge hilo mjini Dodoma ni kutowatendea haki wananchi wanaosubiri kuona wanawasaidia kupata Katiba Mpya.
Mpogoro alisema anashindwa kufahamu iweje tangu wajumbe hao wakutane Dodoma karibu mwezi mzima unafika sasa wameshindwa kupata muafaka ili mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba uanze.
Alisema ni lazima wajumbe hao watambue kuwa wameteuliwa na Rais na kutumwa na wananchi kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Mpya yenye kukidhi matakwa ya watanzania hivyo wafanye kazi yao.
"Malumbano yanayoendelea kwenye Bunge kiasi cha kushindwa kufanya kile walichotumwa kwa hakika ni kutomtendea haki Rais na wananchi waliowatuma kwenda kuipatia nchi katiba mpya,' alisema.
Kumekuwa na malumbano ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo na kusababisha kila mara kuahirishwa kuanza kazi inayosubiriwa kwa hamu na watanzania kitu ambacho kimezua lawama kila kona ya nchi.

TFF yaiomba radhi serikali, ila yaapa kufa na 'wahuni' Taifa

 http://3.bp.blogspot.com/-uLJKC9Kh5w0/UxHRLrp8meI/AAAAAAAFQak/HMg_Zc49ioI/s1600/8.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-45k2Q8Cnb_k/UxHRMVidWtI/AAAAAAAFQas/SmWcYaFMmEM/s1600/9.jpgSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limelaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
TFF  imeiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 1, mwaka huu.
Imesema uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya Sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
“Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine,”imesema taarifa ya TFF.
Kwa mujibu wa Serikali, viti 10 viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao na TFF imekubali kubeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa na ndiyo walioomba idhini ya kutumika uwanja huo kwenye mechi hiyo.
“Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu,”.
“Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi,”imesema taarifa ya TFF.

Japanese anogewa ughaibuni

Japanese kikazi zaidi

Amina Ngaluma 'Japanese' akifurahia maisha Ughaibuni
MUIMBAJI nyota wa zamani wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound, African Revolution 'Wana Tamtam', Amina Ngaluma 'Japanese' amesema hana mpango wa kurejea nchini kwa sasa kutokea ughaibuni anakofanya shughuli zake za muziki na bendi ya Jambo Survivors kwa madai muziki wa Tanzania umejaa 'wizi mtupu'.
Akizungumza na MICHARAZO kutoka Thailand walipoweka maskani yao ya kudumu, Ngaluma alisema haoni ya sababu ya kurudi nyumbani kwa sasa wakati maisha yamemnyookea ughaibuni akiwa na bendi hiyo inayopiga muziki asilia na iliyoweka maskani ya kudumu nchini humo.
"Kwa kweli sifikirii kurudi nyumbani leo wala kesho, hii ni kutokana na kuona tofauti kubwa ya kuthaminika kwa wanamuziki kati ya huko na hapa tulipo tukiendeleza makamuzi na bendi ya Jambo Survivors," alisema Japanese aliyetamba na wimbo wa 'Mgumba II'.
Ngaluma alisema muziki wa Tanzania umeshindwa kuwanufaisha wanamuziki wake kutokana na kuwapo kwa unyonyaji kuanzia kwa wamiliki wa bendi mpaka wadau wanaousimamia kama wasambazaji na hata wananchi wanaowaibia wasanii kazi zao bila kujali wala kuwahurumia wanavyovuja jasho lao.

Noma! Ronaldo ndiye mchezaji tajiri duniani

NYOTA wa Ureno anayeichezea Real Madrid, Cristiano Ronaldo ndiye mwanasoka tajiri kuliko wote duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, nahodha huyo watimu ya taifa ya Ureno ndiye kinara katika orodha hiyo iliyotangazwa leo.
Mkali huyo amerithi nafasi hiyo ya kwanza iliyokuwa ikishikiliwa na David Beckham kwa muda mrefu kabla hajastaafu soka msimu uliopita. 
Ronaldo ambaye alisaini mkataba mnono zaidi na Real Madrid miezi kadhaa iliyopita amempita mshindani wake Lionel Messi na mwanasoka anayelipwa zaidi kimshahara Wayne Rooney.
Samuel Eto'o ndiye Mwaafrika pekee aliyeingia kwenye listi ya wanasoka matajiri zaidi duniani.
Hii ndiyo orodha kamili:
1. Cristiano Ronaldo £122m
2. Lionel Messi £120.5m
3. Samuel Eto'o £70m
4. Wayne Rooney £69m
5. Kaka £67.5m
6. The Neymar family £66m
7. Ronaldinho £64m
8. Zlatan Ibrahimovic £57m
9. Gianluigi Buffon £52m
10.Thierry Henry £47m
SOURCE: Goal.

Ronaldo azidi kuipaisha Real Madrid

High flying: Cristiano Ronaldo hurdles Levante's goalkeeper Keylor Navas
Ronaldo akiwajibika uwanjani
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo usiku wa jana alisaidia timu yake kuzidi kujichimbia kileleni baada ya kufunga moja ya mabao yaliyoisaidia Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Levante.
Real Madrid imefikisha pointi 67 na kuwakimbia Atletico Madrid wenye pointi 64 timu zote zikiwa zimecheza mechi 29.
Ronaldo alifunga bao hilo katika dakika ya 11 akiunganisha kona ya Angel Di Maria kabla ya kumtengenezea pande zote Marcelo aliyefunga bao la pili.
Bao la tatu la vinara hao lilitiwa kimiani na Karabellas dakika ya 81.
Katika mchezo huo Levente walipata pigo baada ya David Navarro kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea vibaya Ronaldo katika dakika ya 49.
Barcelona ambayo juzi ilikandikwa na vibonde Real Valledolid ipo katia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 63 na kutishia amani utetezi wa taji lake la La Liga msimu huu.

Maskini Yanga yakwama Misri, matuta yawatoa Afrika

LICHA ya kutolewa, lakini Yanga inastahili pongezi kwa kupigana kiume mbele ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Al Ahly baada ya kung'olewa kwa mikwaju ya penati katika pambano la marudiano lililochezwa usiku wa jana.
Yanga ilipambana kwa dakika 90 na kujikuta wakilala kwa bao 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 na hivyo kuingia kwenye hatua ya upigaji wa penati ambapo ilionekana dhahiri walikuwa wakielekea kufuzu baada ya Deo Munishi Dida kudaka penati mbili za Wamisri.
Dida aliyeonyesha ushupavu mkubwa alidaka penati za Saed Mowaeb na Hossan Ashour huku zile za Abdalllah Said, Gedo, Mahmoud Trezeguet na Mohamed Nagieb zilimpita.
Hata hivyo Oscar Joshua alikosa penati naye na baadaye Bahanuzi aliyekuwa akimalizia mikwaju ya penati tano tano, alipaisha mkwaju wake wakati wachezaji wenzake wakijiandaa kushangilia kuwavua ubingwa Al Ahly na kuongezwa penati moja moja.
Katika hatua hiyo Mbuyi Twite alilizamisha jahazi la Yanga baada ya kukosa mkwaju wake na kuwafanya mabingwa watetezi hao kufuzu hatua ya pili na kutarajia kukutana na waarabu wenzao kutola Libya, Al Ahli Benghazi.
Kwa wastani Yanga ilikuwa imejiandaa kuweka rekodi kwa soka la uhakika na umakini mkubwa iliyooonyesdha katika mchezo huo kwa kuwabana wenyeji wao kwenye uwanja wa  Border Guard mjini Alexandria.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare ya kutofungana  kabla ya wenyeji kupata bao dakika za jioni baada ya mabeki wa Yanga kujichanganya kuokoa mpira uliokwamishwa na  Sayed Moawad. dakika ya 71.
Ndipo ikaja hatua ya kupigiana penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa matokeo hayo yaliyofanya timu hizo kuwa nguvu sawa kwani Yanga ilishinda bao 1-0 nyumbani wiki iliyopita na zikaja penati na Yanga wakapata penati zao kupitia nahodha Nadir Cannavaro, Emmanuel Okwi na Didier Kavumbagu.
Kung'olewa kwa Yanga kumehitimisha safari ya timu za Tanzania kwenye michuano ya kimataifa baada ya awali Azam, KMKM na Chuoni kung'oka raundi ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.