STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 10, 2014

TFF yaiomba radhi serikali, ila yaapa kufa na 'wahuni' Taifa

 http://3.bp.blogspot.com/-uLJKC9Kh5w0/UxHRLrp8meI/AAAAAAAFQak/HMg_Zc49ioI/s1600/8.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-45k2Q8Cnb_k/UxHRMVidWtI/AAAAAAAFQas/SmWcYaFMmEM/s1600/9.jpgSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limelaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
TFF  imeiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 1, mwaka huu.
Imesema uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya Sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
“Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine,”imesema taarifa ya TFF.
Kwa mujibu wa Serikali, viti 10 viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao na TFF imekubali kubeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa na ndiyo walioomba idhini ya kutumika uwanja huo kwenye mechi hiyo.
“Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu,”.
“Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi,”imesema taarifa ya TFF.

No comments:

Post a Comment