STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 10, 2014

Mpiga Drums Extra Bongo awashtua Wajumbe Bunge la Katiba

Mpogoro Machine akikaanga chipa mazoezi ya Extra Bongo
MPIGA dramu wa bendi ya Extra Bongo 'Wana Kimbembe', Wenceslaus Chitalula 'Mpogoro Machine', amewaomba Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kufanya kile walizotumwa na wananchi.
Mwanamuziki huyo alisema malumbano na muda unaopotezwa na wajumbe hao kwenye bunge hilo mjini Dodoma ni kutowatendea haki wananchi wanaosubiri kuona wanawasaidia kupata Katiba Mpya.
Mpogoro alisema anashindwa kufahamu iweje tangu wajumbe hao wakutane Dodoma karibu mwezi mzima unafika sasa wameshindwa kupata muafaka ili mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba uanze.
Alisema ni lazima wajumbe hao watambue kuwa wameteuliwa na Rais na kutumwa na wananchi kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Mpya yenye kukidhi matakwa ya watanzania hivyo wafanye kazi yao.
"Malumbano yanayoendelea kwenye Bunge kiasi cha kushindwa kufanya kile walichotumwa kwa hakika ni kutomtendea haki Rais na wananchi waliowatuma kwenda kuipatia nchi katiba mpya,' alisema.
Kumekuwa na malumbano ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo na kusababisha kila mara kuahirishwa kuanza kazi inayosubiriwa kwa hamu na watanzania kitu ambacho kimezua lawama kila kona ya nchi.

No comments:

Post a Comment