STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 22, 2014

Tanzania yaongeza idadi ya waamuzi wa FIFA

http://2.bp.blogspot.com/-Uvl9thwPjXs/UmQg2dG5y6I/AAAAAAAAI8U/3weLwxnUtIk/s1600/DSC_0823.jpg
SHIRIKISHO la soka Duniani, FIFA limetoa orodha mpya ya waamuzi linaowatambua ambapo katika orodha hiyo kuna jumla ya marefa 18 wa Tanzania, miongoni mwao 11 ni wapya na saba wa zamani. 
Waamuzi wapya wa kati kutoka Tanzania ni Mfaume Ali Nassor kutoka Zanzibar pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro.
Pia wamo waamuzi watatu wa kike ambao ni Florentina Zabron, Jonesia Rukyaa pamoja na Sofia Ismail. 
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wanaume ni Frank John Komba na Soud Idd Lila, kwa upande wa wanawake ni Kudura Omary Maurice, Hellen Joseph Mduma, Dalila Jafari Mtwana na Grace Mawala. Waamuzi wa zamani wa Tanzania kwenye orodha ya FIFA, kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha Waziri, kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Fernand Chacha, John Longino Kanyenye, Ali Kinduli na Samuel Hudson Mpenzu.

CAF yatoa ratiba, Azam kuanza na Wasudan, Yanga na maafande wa Botswana, KMKM wapewa pia Wasudan, Polisi kucheza na Wagabon

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/DSC021662.jpg
Yanga
http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/08/AZAM-FC.jpg
Azam watakaoanza na El Merreikh ya Sudan
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), imetangaza ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Azam wamepangwa kuanza na El Merreikh ya Sudan, wakati Yanga wakitupiwa maafande wa Jeshi kutoka Botswana.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Azam ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwakani itaanzia nyumbani kabla ya kuwafuata Wasudan hao kwao katika mechi ya marudiano.
Wenyewe Yanga ambao mwaka huu ilishiriki Ligi ya Mabingwa na kung'olewa raundi ya pili na waliokuwa mabingwa watetezi, Al Ahly, imepangwa kuanzia pia nyumbani katika Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF IX ya Botswana inayomilikiwa na Jeshi la nchi hiyo.
Wawakilishi wengine wa Zanzibar, mabingwa KMKM wataanzia ugenini kwa kuumana na Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika na wawakilishi wa Kombe la Shirikisho, Polisi wataanza ugenini dhidi ya CF Mounana ya Gabon.
Mechi za awali za michuano hiyo zitaanza kuchezwa kati ya Februari 13-15 na zile za marudiano zitakuwa Machi 28-Machi 1.
Ratiba kamili ya michuano hiyo Ligi ya Mabingwa ipo hivi;
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/CAF.png


Rais amfuta kazi Prof Tibaijuka, Prof Muhongo awekwa kiporo

Rais Jakaye Kikwete akizungumza jioni ya leo
http://annatibaijuka.org/wp-content/uploads/2013/06/9.jpg
Prof Tibaijuka aliyetenguliwa uteuzi wake kisa fedha za James Rugemalila
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete amevunja ukimya leo wakati akizungumza na Wazee wa jiji la Da es Salaam na kugusia baadhi ya mambop ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania likiwamo  Sakata la akaunti ya Tegeta ESCROW.
Katika hutoba yake ya zaidi ya saa 2 Rais Kikkwete aliweka bayana juu ya kumfuta kazi  Prof, Anna Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyuma na Maendeleo ya Makazi, huku akimweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.
Rais  KIkwete alisema kuwa kosa kubwa alilofanya Tibaijuka ni kuruhusu fedha alizopewa na Jamea Rugemalila, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya VIP Engeneering kama msaada kwa shule yake kuingia moja kwa moja kwenye akaunti yake kitu amabcho ni kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma.
Prof. Tibaijuka amekiri mwenyewe mara kadhaa kupokea kiasi cha Bil. 1.6 katika akaunti yake, lakini akijitetea ni kwa ajili ya Shule anazomiliki na hiviu karibuni alinukuliwa akidai hatajiuzulu kwa vile hata Rais Kikwete atamshangaa na pia yeye na JK wanajuana kitambo tangu wakisoma wote Chuo Kikuu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Rais ni kwamba wamemshauri kuwapisha wamteue mwingine kushika nafasi yake kwa kukiuka miiko ya Maadili kwa maana nyepesi ni kwamba amemfuta kazi.
Prof Tibaijuka amekumbwa na sekeseke hilo kutokana na kukubali fedha alizopewa na Rugemalila kama msaada kwa shule yake kuingia kwenye akaunti yake.
Aidha Rais Kikwete  amesema kuwa fedha katika akaunti ya ESCROW ni za IPTL na sio za TANESCO (Umma) huku na kuhusu Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mh. Raisi amesema kuwa suala lake linawekwa kiporo kwa bado ucchunguzi juu ya suala hilo unaendelea kufanyiwa kazi.
Pia aliweka bayana namna alivyofurahishwa na uzalendo ulioonyeshwa na Wabunge bila kujali itikikadi zao za vyama na kuwapongeza.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akihutubia Wazee wa jiji la Da es Salaam. Sakata la akaunti ya ESCROW leo limeingia katika sura mpya baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kumvua rasmi madaraka Prof, Anna Tibaijuka. Akizungumza leo na wazee wa Dar es Salaam Raisi Kikwete alisema kuwa kosa kubwa alilofannya Tibaijuka ni kuruhusu fedha alizopewa na Rugemalila kama msaada kwa shule yake kuingia moja kwa moja kwenye akaunti yake kitu amabcho ni kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma. Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa akishikilia wadhifa wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi amekumbwa na sekeseke hilo kutokana na kukubali fedha alizopewa na Rugemalila kama msaada kwa shule yake kuingia kwenye akaunti yake jambo lililozua mjadala mkubwa sana miongoni mwa raia wa Tanzania huku wakihoji kwa nini iwe hivyo. Hivi karibuni Prof. Tibaijuka aliutangazia umma wa Tanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwa hawezi kujiuzulu kwa kuwa yeye hana kosa lolote katika sakata hilo huku akisisitiza kuwa akijiuzulu hata Raisi mwenyewe atashangaa uamuzi wake. Prof. Tibaijuka aliendelea kusisitiza kuwa endapo angejiuzulu asingeitendea haki dhana ya mwanamke kuchakalika na maendeleo has kwa jamii za Kitanzania. Katika hatua nyingine Mh Raisi amesema kuwa fedha katika akaunti ya ESCROW ni za IPTL na sio za TANESCO (Umma) huku na kuhusu Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mh. Raisi amesema kuwa suala lake linawekwa kiporo kwa bado ucchunguzi juu ya suala hilo unaendelea kufanyiwa kazi.

Copy and WIN :##############

Shamsa aota makubwa zaidi 2015

MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Shamsa Ford amesema anatamani mafanikio makubwa zaidi katika mwaka ujao kuliko aliyoyapata ndani ya 2014 hasa kupitia kazi yake ya 'Chausiku'.
Shamsa, alisema ingawa kila kitu hupangwa na Mungu, lakini anaamini mwaka 2015 unaweza kuwa wa neema zaidi kwake kutokana na kutarajia kuufungua na kazi mpya iitwayo 'Mama Muuza'.
"Mama Muuza ndiyo nitakayofungua nayo mwaka, ila naomba Mungu na ninatamani sana niwe na mafanikio zaidi 2015 kuliko niliyoyapata mwaka huu. Niseme ukweli 'Chausiku' imenibeba sana kama ilivyokuwa kwa 'Hukumu ya Ndoa Yangu'," alisema Shamsa.
Muigizaji huyo alisema katika filamu hiyo ijayo ameigiza na nyota mbalimbali akiwamo Haji Adamu maarufu kama Baba Haji na ni moja ya filamu iliyobeba maisha halisi ya Watanzania hasa wa uswahili kama ilivyokuwa katika Chausiku ambayo  aliigiza kama 'chakaramu' ambaye analiliwa penzi na mtoto wa tajiri.
Cha ajabu pamoja na umapepe wake na utemi wake mtaani katika kusaka madeni yake, kumbe alikuwa 'mpya' katika katika mapenzi kitu kilichomfanya kijana aliyelilia penzi lake kustaajabu.

Sadiki Momba kuwania ubingwa wa WBO Ghana

http://4.bp.blogspot.com/-LLzmWHII6N4/UkitFkI0rJI/AAAAAAAADl0/8mVm6RcEU2s/s1600/IMG_6645.JPG
Momba (Kushoto) akiwa katika moja na mapambano yake ya ngumi nchini
BONDIA Sadiki Momba ameondoka nchini kwenda Ghana kwa ajili ya kupanda ulingoni siku ya Krismasi kuwania ubingwa wa WBO-Mabara dhidi ya mwenyeji wake, Emmanuel Tagoe.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST, Anthony Rutta, Momba aliondoka nchini juzi Jumamosi kwa Ndege ya Shirika la Kenya Airways na atapanda ulingoni kwenye uwanja wa michezo wa Accra, mjini Accra siku za Desemba 26.
Rutta alisema pambano hilo la uzani wa Light (lightweight) litakuwa la raundi 12 na litakuwa nafasi nyingine kwa Mtanzania huyo kulipa kisasi kilichomkuta bondia mwenzake mapema mwezi huu Allan Kamote alioyepigwa kwa KO katika kuwania ubingwa wa dunia wa WBO.
"Baada ya Allan Kamote kupigwa kwa KO na George Ashie Desemba 5, safari hii PST imempeleka Sadiki MOmba kupigana na Mghana Emmanuel Tagoe kuwania ubingwa wa Mabara wa WBO pambano litakalochezwa mjini Accra, Ghana DEsemba 26," alisema Rutta.
Kwa muda mrefu mabondia wa Tanzania wamekuwa hawafanyi vizuri kila wanapoenda kupambana nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikizua maswali mengi, japo mamlaka zinazosimamia ngumi hizo zimekuwa zikijitetea kuwa inatokana na maandalizi duni.

Soka la Kongo lamduwaza nyota wa Coastal Union

Danny Lyanga akiwa uzi wa FC Lupopo
Danny Lyanga alipokuwa akifanya vitu vyake na Coastal
Danny Lyanga akipiga danadana
 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Coastal Union, Danny Lyanga anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema ameshangazwa na utofauti kubwa uliopo baina ya soka la Tanzania na la nchi hiyo.
Aidha mchezaji huyo amewahimiza wachezaji wenzake waliopo nchini wapambane ili watoke nje badala ya kuridhika kucheza nyumbani akidai kitendo cha kucheza nje ya nchi kitasaidia kupanua upeo wao katika mchezo huo na kulisaidia taifa.
Akizungumza na MICHARAZO, Lyanga aliyepanda na Coastal katika Ligi Kuu msimu wa 2011-2012, alisema kwa kipindi kifupi tangu awe nchini humo na kuichezea timu yake amestaajabishwa na mfumo wa ligi ya nchini hiyo na namna klabu zilivyowekezwa katika mchezo huo.
Lyanga alisema uwekezaji mkubwa uliofanywa na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kongo, imefanya ligi hiyo kuwa ngumu na yenye ushindani na pengine ndiyo maana timu zao zinatisha barani Afrika.
"Kaka kweli tembea uone, huku soka lao linatofautiana sana na huko nyumbani, ligi ina ushindani wachezaji wanajitambua na kujituma na hata mfumo wao unafanya vikaze msuli kweli kweli jambo ambalo linafanya bligi yao kubwa bora," alisema.
Mshambuliaji huyo wa pembeni alisema kwa sasa timu yao ya Fc Lupopo inakamata nafasi ya tano (kabla ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Lubumbashi, walikuwa wamecheza mechi saba wakishindwa tatu, kutoka sare tatu na kupoteza moja, huku yeye akisaidia kutoa pasi ya mabao manne katika mechi tatu alizochezeshwa mpaka sasa.
Lyanga alisema kwa namna alivyofumbuliwa macho anadhani ni muda muafaka kwa wachezaji wa Tanzania kujibidiisha kutoka nje ya nchi badala ya kuridhika na soka la nyumbani na kuwataka pia viongozi kutowabania wanaopata nafasi ili kutoa nafasi ya kuwa na nyota watakaokuwa msaada mkubwa kwa taifa kama inavuonufaika kwa sasa kwa Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto na Thomas Ulimwengu.

Sherehe za SHIWATA zaota mbaya, kisa...Sikukuu

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib 'Teacher'
SHEREHE za miaka 10 ya kuanzishwa kwa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) zilizokuwa zifanyike Desemba 25, jijini Dar es Salaam zimeahirishwa.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema kuwa kuahirishwa kwa sherehe hizo kumetokana na wanachama wengi ambao walitakiwa kukabidhiwa nyumba zao kuwa katika sherehe za Krismas nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kuahirishwa huko kumesababisha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga Veterani lililokuwa lichezwe Desemba 25 kwenye uwanja wa Azam, Charambe mpaka litakapotangazwa tena.
Mwenyekiti Taalib alisema sababu nyingine ya kuahirishwa kwa sherehe hizo ni kutokana na maombi ya mgeni rasmi ambaye hakumtaja kuwa yuko nje ya nchi kikazi ambaye aliomba ahudhurie tamasha hilo la kihistoria.
Nyumba ambazo zitakabidhiwa ni 38 ambazo zimejengwa na kukamilika ambako wanachama hao walichangia ujenzi kwa kutoa fedha kidogo kidogo kupitia benki na kuchangua aina ya nyumba anayoitaka kutokana na kiasi alizochangia.
Ili kuwapatia makazi ya bei nadfuu wanachama wake SHIWATA inajenga nyumba za sh. 631,000, sh. 1,500,000, sh. 3,800,000 na sh. 6,400,000 ambazo mwanachama anagaiwa kila mwezi Juni na Desemba kila mwaka.
Alisema katika makabidhiano hayo wamiliki wa nyumba hizo pia watakabidhiwa vyeti maalum vya kumaliki nyumba zao katika sherehe kubwa itakayofanyika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga. Mpaka sasa SHIWATA ina wanachama 8,000.

Polisi yawasaka waliohusika na kifo cha Aisha MadindaMwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake.
KIMENUKA! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

Aisha Madinda akiwa na Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka.
  Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, zilidai kwamba jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.

  “Aisha alipofikishwa Mwananyamala alikuwa ameshafariki dunia. Sasa waliokuwa naye wanajua aliyehusika kwa namna yoyote ile lazima wakamatwe,” kilisema chanzo cha ndani cha jeshi hilo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake
Ili kupata undani wa ishu hiyo, Jumamosi iliyopita Ijumaa Wikienda lilizungumza na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza majibu hayajatoka hivyo ni mapema kuyazungumzia. Madai kwamba kuna mtu mmoja amekamatwa si ya kweli.”
Aisha (35) alizikwa Ijumaa iliyopita huko Kigamboni, Dar, baada ya kukutwa na umauti wa kutatanisha Jumatano ya wiki iliyopita.
GPL