STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 22, 2014

Soka la Kongo lamduwaza nyota wa Coastal Union

Danny Lyanga akiwa uzi wa FC Lupopo
Danny Lyanga alipokuwa akifanya vitu vyake na Coastal
Danny Lyanga akipiga danadana
 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Coastal Union, Danny Lyanga anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema ameshangazwa na utofauti kubwa uliopo baina ya soka la Tanzania na la nchi hiyo.
Aidha mchezaji huyo amewahimiza wachezaji wenzake waliopo nchini wapambane ili watoke nje badala ya kuridhika kucheza nyumbani akidai kitendo cha kucheza nje ya nchi kitasaidia kupanua upeo wao katika mchezo huo na kulisaidia taifa.
Akizungumza na MICHARAZO, Lyanga aliyepanda na Coastal katika Ligi Kuu msimu wa 2011-2012, alisema kwa kipindi kifupi tangu awe nchini humo na kuichezea timu yake amestaajabishwa na mfumo wa ligi ya nchini hiyo na namna klabu zilivyowekezwa katika mchezo huo.
Lyanga alisema uwekezaji mkubwa uliofanywa na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kongo, imefanya ligi hiyo kuwa ngumu na yenye ushindani na pengine ndiyo maana timu zao zinatisha barani Afrika.
"Kaka kweli tembea uone, huku soka lao linatofautiana sana na huko nyumbani, ligi ina ushindani wachezaji wanajitambua na kujituma na hata mfumo wao unafanya vikaze msuli kweli kweli jambo ambalo linafanya bligi yao kubwa bora," alisema.
Mshambuliaji huyo wa pembeni alisema kwa sasa timu yao ya Fc Lupopo inakamata nafasi ya tano (kabla ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Lubumbashi, walikuwa wamecheza mechi saba wakishindwa tatu, kutoka sare tatu na kupoteza moja, huku yeye akisaidia kutoa pasi ya mabao manne katika mechi tatu alizochezeshwa mpaka sasa.
Lyanga alisema kwa namna alivyofumbuliwa macho anadhani ni muda muafaka kwa wachezaji wa Tanzania kujibidiisha kutoka nje ya nchi badala ya kuridhika na soka la nyumbani na kuwataka pia viongozi kutowabania wanaopata nafasi ili kutoa nafasi ya kuwa na nyota watakaokuwa msaada mkubwa kwa taifa kama inavuonufaika kwa sasa kwa Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto na Thomas Ulimwengu.

No comments:

Post a Comment