STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 22, 2014

Polisi yawasaka waliohusika na kifo cha Aisha Madinda



Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake.
KIMENUKA! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

Aisha Madinda akiwa na Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka.
  Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, zilidai kwamba jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.

  “Aisha alipofikishwa Mwananyamala alikuwa ameshafariki dunia. Sasa waliokuwa naye wanajua aliyehusika kwa namna yoyote ile lazima wakamatwe,” kilisema chanzo cha ndani cha jeshi hilo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake
Ili kupata undani wa ishu hiyo, Jumamosi iliyopita Ijumaa Wikienda lilizungumza na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Camilius Wambura ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza majibu hayajatoka hivyo ni mapema kuyazungumzia. Madai kwamba kuna mtu mmoja amekamatwa si ya kweli.”
Aisha (35) alizikwa Ijumaa iliyopita huko Kigamboni, Dar, baada ya kukutwa na umauti wa kutatanisha Jumatano ya wiki iliyopita.
GPL

No comments:

Post a Comment