STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 22, 2014

Shamsa aota makubwa zaidi 2015

MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Shamsa Ford amesema anatamani mafanikio makubwa zaidi katika mwaka ujao kuliko aliyoyapata ndani ya 2014 hasa kupitia kazi yake ya 'Chausiku'.
Shamsa, alisema ingawa kila kitu hupangwa na Mungu, lakini anaamini mwaka 2015 unaweza kuwa wa neema zaidi kwake kutokana na kutarajia kuufungua na kazi mpya iitwayo 'Mama Muuza'.
"Mama Muuza ndiyo nitakayofungua nayo mwaka, ila naomba Mungu na ninatamani sana niwe na mafanikio zaidi 2015 kuliko niliyoyapata mwaka huu. Niseme ukweli 'Chausiku' imenibeba sana kama ilivyokuwa kwa 'Hukumu ya Ndoa Yangu'," alisema Shamsa.
Muigizaji huyo alisema katika filamu hiyo ijayo ameigiza na nyota mbalimbali akiwamo Haji Adamu maarufu kama Baba Haji na ni moja ya filamu iliyobeba maisha halisi ya Watanzania hasa wa uswahili kama ilivyokuwa katika Chausiku ambayo  aliigiza kama 'chakaramu' ambaye analiliwa penzi na mtoto wa tajiri.
Cha ajabu pamoja na umapepe wake na utemi wake mtaani katika kusaka madeni yake, kumbe alikuwa 'mpya' katika katika mapenzi kitu kilichomfanya kijana aliyelilia penzi lake kustaajabu.

No comments:

Post a Comment