STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 20, 2012

  NDOA YANGU 'KUMFUFUA' KANUMBA

KAVA LA MOJA YA FILAMU MBILI ZA MAREHEMU STEVEN KANUMBA ALIZOICHEZEA KABLA YA KUFARIKI APRIL MWAKA HUU AMBAYO INATARAJIWA KUINGIZWA SOKONI HIVI KARIBUNI

Tegete achekelea sare za Oljoro, Azam


KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Toto Africans, John Tegete amedai kufurahishwa na vijana wake walivyopigana kiume katika mechi zao mbili za awali za ligi kuu dhidi ya JKT Oljoro na Azam na kuambulia sare tupu.
Toto iliyokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani katika mechi zote mbili, ilianza kwa sare ya bao 1-1 kwa bao la 'jioni' sawa na ilivyokuwa katika pambano lao la pili dhidi ya Azam waliotoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2 lililochezwa jana jijini Mwanza.
Tegete alisema namna wachezaji wake walivyopigana katika kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha mabao katika mechi hizo zimemfanya aamini msimu huu utakuwa wa mafanikio kwa timu yake.
Hata hivyo Tegete alisema Toto ilistahili ushindi katika mechi hiyo kama sio uzembe uliofanywa na vijana wake na kuwaruhusu Oljoro kujipatia bao la kuongoza ambalo lilikuwa likielekea kuizamisha Toto nyumbani kabla ya kusawazishwa baadae.
"Kwa kweli nimefurahishwa na namna vijana wangu walivyocheza hasa kwa kurudisha bao tulilokuwa tumefungwa, japo sijaridhishwa na bao liloruhusiwa nao na kuwafanya maafande wale kututangulia," alisema.
Juu ya mechi ya Azam alisema timu yake ilicheza vema kipindi cha kwanza kabla ya kuzidiwa maarifa kipindi cha pili, ila wachezaji walijituma na kuepuka kipigo cha mabao 2-1 kilichokuwa ikionekana dhahiri kwa mashabiki waliuofutiuka CCM Kirumba.
Tegete alisema kwa sasa akili zao zipo kwenye pambano lao la ugenini dhidi ya Coastal Union litakalochezwa Jumamosi, mjini Tanga.
Toto itavaana na Coastal ambayo imetoka mjini Mbeya ilipolazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons Mbeya, huku uongozi wa timu ya Tanga wakilalamika kunyimwa bao la dhahiri lililofungwa na Atupele Green ambalo kama sio mwamuzi lingewapa ushindi wao wa pili mfululizo baada ya ule ya awali wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT.

TAMASHA LA MUZIKI LA DANSI KUFANYIKA DAR


IJUE HISTORIA YA NGUMI ZA KULIPWA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ECAPBF) ULIVYOANZA MWAKA 1983‏



LEO tumeona ni vyema kuwakumbsha Watanzania na wapenzi wa ngumi kwa ujumja ili kuweka kumbukumbu sahihi za taarifa  kuhusu masuala ya ngumi za kulipwa na ambazo tunafurahi kuwa zimeanza kutolewa na bwana Yasin Abdallah (Ustaadh), tungependa pia kuwapa maelezo sahihi kuhusu ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa Afrika ya Mashariki na Kati.

Ubingwa huu umekuwa unapigiwa kelele na baadhi ya watu ambao wana malengo ya kuharibu taswira nzima ya nguni za kulipwa na kuturudisha nyuma kwenye enzi za vurugu zilizowahi kutokea hapo nyuma.

Ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati ulianzishwa mwaka 1983 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Mpaka kufikia wakati huo (1983) ni nchi ya Tanzania pekee iliyokuwa imeshaanzisha ngumi za kulipwa katika ardhi yake ambapo Kenya na Uganda zilikuwa bado hazijaanzisha ngumi za kulipwa nchini mwao japokuwa zilikuwa na mabondia kadhaa waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa katika nchi za Ulaya na Asia.

Mabondia wa Kenya waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa nje ya nchi yao wakati huo walikuwa ni pamoja na Steven Muchoki na mdogo wake Michael Irungu, waliokuwa wanapigana ngumi nchini Denmark chini ya Promota maarufu Mogens Palle. 

Mabondia wengine wa Kenya waliokuwa wanapigana ngumi za kulipwa nje ya Kenya walikuwa ni pamoja na Modesti Napunyi Oduor, Isayah Ikoni na Philip Warwinge waliokuwa wanazipiga nchini Japan.

Aidha mabondia wa Uganda waliokuwa wanacheza ngumi nje ya nchi yao waliongozwa na Ayub Kalule, John Odhiambo, Mustapha Waisaja, John Mugabi (The Beast), John Rubin Byaruhanga na Cuban Businge ambao wote pia walikuwa chini ya promota maarufu Mogens Palle wa Denmark.

Kwa upande Tanzania bondia pekee aliyekuwa anacheza ngumi za kukipwa nje ya nchi wakati huo alikuwa Gerald Isaac (Tanzania’s Devil kama wapenzi wa ngumi na vyombo vya habari vya Marekani walivyokuwa wanamwita kwa ajili ya ukali wake kwenye masumbwi ulingoni) aliyekuwa anazichapa nchini Marekani.

Tarehe 18 mwezi wa Juni liliandaliwa pambano la kwanza la aina yake kwa ubingwa mpya kabisa wa Afrika ya Mashariki na Kati lililofanyika katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa jijini Nairobi (Kenyatta International Conference Center, KICC).

Waandaji wa mpambano huo walikuwa ni pamoja na DS Njoroge wa kampuni maarufu ya ngumi wakati huo DS Boxing Promotions ya jijini Nairobi nchini Kenya, Joe Akech ambaye wakati huo alikuwa ndiye Meneja Mkuu wa Kanda wa shirika la ndege la Marekani, Pan American Airlines (Pan Am) na David Attan na mkewe Linda Brown Attan wa kampuni ya Davlin Boxing Promotions ambaye baadaye alikuja kuwa Promoter wa bondia Onesmo Ngowi. 

Joe Akechi alikuja kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Kenya (KPBC) na Meya wa Jiji la Nairobi.

Mpambamno huo wa kugombea mkanda wa Bantamweight uliwakutanisha mabondia wawili ambao walikuwa wanatamba sana katika nchi zao katika miaka ya 1980!.

Bondia Onesmo Alfred Ngowi (Piston Mover) wa Tanzania alikuwa ameshawapiga mabondia wote waliokuwa tishio kwenye uzito wake wa bantamweight wakiwa ni pamoja na Musa Mwabata, Sasi Sarungi, Ali Mohammed, Antoni Nyembela, Pius Lwandalla na David Migeke.

Kwa upande wa Kenya Modest Napunyi Oduor (Babaa) alikuwa ndiye bondia aliyekuwa anatamba sana kwa wakati huo na ndio tu alikuwa anatokea nchini Japan alikokuwa anapigana ngumi za kulipwa.

Wawili hao (Ngowi na Oduor) walikutana katika mpambano wa kwanza kabisa wa Afrika ya Mashariki na Kati tarehe 18 Juni 1983 katika ukumbi wa Kenyatta International Conference Center (KICC) na kugombea mkanda wa kwanza wa Afrika ya Mashariki na Kati.

Katika mpambano huo mabondia wengine kutoka Kenya (Steven Muchoki, Athumani, na Michael Irungu) Uganda (Cuban Businge) Tanzania (Clement Chacha, Emmanuel Kimaro na Fidel Haynes) nao walipanda ulingoni kusindikiza pambano hilo la kihistoria ambalo lilianzisha ngumi za kulipwa katika nchi za Kenya na Uganda kwa mara ya kwanza.

Mwamuzi wa mpambano huo wa ubingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati alikuwa Emmanuel Mlundwa wa Tanzania wakati huo akiwa ndiye Rais wa Boxing Union of Tanzania (BUT) iliyokuja kubadili jina na kuwa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) mwaka 2000.

Miaka 21 baadaye mwaka yaani 2004, Kamisheni za Ngumi za Kulipwa za Kenya (Kenya Professional Boxing Commission, UPBC), Uganda (Uganda Professional Boxing Commission, UPBC na Tanzania Professional Boxing Commission, TPBC zilikutana mjini Moshi na kuunda rasmi Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika Mashariki na Kati (East & Central Africa Professional Boxing Federation au ECAPBF.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Marais wa Kamisheni hizo tatu Celestino Mindra (UPBC) Memba Muriuki (KPBC) na Onesmo Ngowi (TPBC) uliweka uongozi mpya wa Shirikisho la ECAPBF kama ifuatavyo:

Onesmo Ngowi (Tanzania) – Rais
Celestino Midra (Uganda) - Makamu wa Kwanza wa Rais
Memba Muriuki (Kenya) - Makamu wa Pili wa Rais
Shaaban Ogola (Kenya) Katibu Mkuu wa ECAPBF
Nemes Kaviehe (Tanzania) Mweka Hazina Mkuu wa ECAPBF
Paul Chiwa (Uganda) Afisa Uhusiano na habari Mkuu wa ECAPBF
Imetolewa na:
Uongozi
ECAPB

CHELSEA, BARCA, MAN UTD ZATAKATA ULAYA

Shinji Kagawa akiwajibika katikam pambano lao dhidi ya Galatasaray

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia moja ya mabao yao



















WAKATI mabingwa watetezi Chelsea ya Uingereza ikianza kwa sare ya 2-2 kwenye mbio za kuwania Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndugu zao wa Manchester United walianza ligi yab makundi kwa ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Galatasaray.

Nao vinara wa Ligi ya Hispania, Barcelona waliponea chupuchupu na kufanikiwa kuibuka mshdini wa mabao 3-2 dhidi ya Spartak Moscow, ilihali wanafainali za mwaka jana, Bayern Munich iliipata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Valencia.

Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo ni kama ifuatavyo;


19 September
Shakhtar Donetsk2 - 0FC Nordsjaelland
HH Mkhitaryan (43)
HH Mkhitaryan (75)

Donbass ArenaAttendance (51624)
Teams | Report
19 September
Chelsea2 - 2Juventus
EdSJ Oscar (30)
EdSJ Oscar (32)

A Vidal (37)
F Quagliarella (79)
Stamford BridgeAttendance (40918)
Teams | Report

19 September
Bayern Munich2 - 1Valencia
B Schweinsteiger (37)
T Kroos (75)

N Haedo Valdez (90)
Allianz ArenaAttendance (65374)
Teams
19 September
Lille1 - 3BATE
A Chedjou (59)
A Volodko (5)
V Rodionov (19)
E Olekhnovich (42)
Lille MetropoleAttendance (43215)
Teams | Report

19 September
Barcelona3 - 2Spartak Moscow
CH Tello (13)
LA Messi (70)
LA Messi (79)

d Dani Alves (og 29)
BM Romulo (57)
Camp NouAttendance (82241)
Teams | Report
19 September
Celtic0 - 0Benfica
Celtic Park
Teams | Report

19 September
Man Utd1 - 0Galatasaray
M Carrick (6)
Old TraffordAttendance (74653)
Teams | Report
19 September
Braga0 - 2CFR Cluj-Napoca

R Bastos (18)
R Bastos (33)
Estadio AXAAttendance (24000)

MICHAEL WAMBURA AWEKA PINGAMIZI UCHAGUZI MKUU DRFA

MICHAEL RICHARD WAMBURA
P.O. BOX 22557,
TEL. 0713/0754/O787 326 485
DAR ES SALAAM.
September  15, 2012
Mr A. Ndolanga
MWENYEKITI,
KAMATI YA Uchaguzi ya DRFA
CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU- DSM(DRFA)
YAH: PINGAMIZI JUU YA KAMATI YA UCHAGUZI , WAPIGA KURA, NA WAGOMBEA   KATIKA  UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU CHA DAR-ES-SALAAM(DRFA) ULIOPANGWA KUFANYIKA OCT ,2012
Nimelazimika  kuleta maombi ya pingamizi langu  mbele yako na kamati yako kuhusiana na uchaguzi tajwa hapo juu  wa DRFA kutokana na uvunjifu wa kanuni, maagizo na Katiba ya TFF sambamba na katiba ya DRFA na sheria za nchi katika mchakato mzima wa kuelekea katika uchaguzi huo , malalamiko yangu ambayo sehemu kubwa ni ya kisheria na kikatiba malalamiko yangu  ni  kama ifuatavyo.
  1. Uundwaji wa kamati ya chaguzi ya DRFA umevunja kanuni ya uchaguzi wa wanachama wa TFF (TFF MEMEBERS STANDARD ELECTROL CODE) Ibara ya 3(2) inakataza mtu mmoja kuwa mjumbe wa kamati mbili za uchaguzi za   wanachama wa TFF au wanachama washiriki wa TFF “The members of the  Committee  shall under no circumstances be member of the executive body of TFF or Executive body of the Association or Executive of other TFF member Association or the Elections Committee of the other member association of TFF or Executive body /Elections Committee of a subordinate”  kwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Muidin Ndolanga Pia Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya FRAT(taifa ambao wote ni wanachama wa TFF basi uhalali wake wa kuwa m/kiti wa kamati ya Uchaguzi wa DRFA unakuwa haupo kwa kuwa unavunja kanuni za uchaguzi  , kwa maana hiyo naomba tamko la kuwa mchakato mzima  wa uchaguzi ufutwe na kuanza upya kwa kuwa haukufuata taratibu na kanuni husika .
  2. Katiba ya DRFA toleo la 2008 ibara ya  1(6) inatamka kuwa “DRFA itaheshimu  Katiba, Kanuni Maagizo na Maamuzi ya TFF na  kuhakikisha  kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake”  TFF kupitia barua yake kumbukumbu TFF/ADM/EC/36 ya tarehe 22/7/2011 yenye kichwa cha habari “ Katiba za Wanachama na Wanachama wao”  kwenda kwa  makatibu ambapo iliagiza kufanyika mabadiliko katiba zao ili ziendane kikamilifu  na katiba ya mfano ya TFF  aidha TFF kupitia barua yake ya  tarehe 12/12/2012 yenye kumbukumbu TFF/TECH?GC11/115 kwenda kwa makatibu wa wilaya ikikumbushia  kurekebisha katiba zao ili ziendane na Katiba ya mfano ya TFF, Kwa kuwa Katiba za wanachama wa DRFA na DRFA  hazijafanyiwa marekebisho na wahusika ni wazi hawajatekeleza maagizo ya TFF hivyo  kwenda kinyume na Katiba ya TFF 12(d)(e) & (n) na Ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi za TFF na Wanachama wake. Na hata kama marekebisho yamefanyika ni wazi hayatakuwa yamezingatia matakwa ya kisheria na maamuzi ya TFF kwani katiba hiyo haijapitishwa na kamati ya sheria, Katiba na hadhi za wachezaji kama maagizo ya awali ya TFF yalivyo agiza.
  3. KUKIUKWA KWA KATIBA YA DRFA
Marekebisho ya Katiba yanayodaiwa kufanywa  hayakuzingatia katiba ya DRFA  “kazi mojawapo ya Mkutano mkuu wa DRFA ni kufanya na kupitisha marekebisho ya katiba” kwa kuwa marekebisho hayajapitishwa na mkutano mkuu wa DRFA” kama katiba inavyo elekeza basi marekebisho hayo ni batili kwa mujibu wa katiba ya DRFA
  1. Kwa kuwa wilaya wanachama wa DRFA hawakufuata kanani za Uchaguzi  za TFF na  Wanachama wake, kumepelekea baadhi ya viongozi waliochaguliwa  kutokuwa na sifa ikiwemo ya Elimu isiyopungua kidato cha Nne ikiambatana na  Cheti cha Matokeo  kama ilivyoagizwa na TFF katika barua yake kwa wanachama  wake  na wilaya, kwa kuwa viongozi hao wa wilaya wanakosa sifa ya kuwa viongozi ni wazi pia wanakosa sifa ya kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, itakumbukwa katika Uchaguzi wa Chama cha mpira Mkoa Mara(FAM) ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Nd Lyato) alikuwepo ambapo Nd MAGOTI ambaye alikuwa Katibu wa Chama cha mpira Wilaya  ya Bunda aliondolewa  katika kugombea  na hakurusiwa kupiga kura baada ya kuonekana hakuwa na sifa ya kuwa Katibu wa wilaya kutokana na tatizo la Elimu halikadhalika Katibu wa Wilaya ya Serengeti Ombeni Magati nae aliondolewa katika kugombea ujumbe wa kamati ya Utendaji na pia hakuruhusiwa kupiga kura na  nafasi walizokuwa wanazishikilia kutangazwa kuwa ziko wazi, hivyo ni matumaini yangu hata katika DRFA na wanachama wake mkondo utafuata huo huo.
  2. kiongozi anaemaliza muda wake atakuwa na haki ya kutetea nafasi yake ili mradi awe na sifa kwa mujibu wa Katiba na kanuni za DRFA na TFF , itakumbukwa kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba Mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Mzee Hasan Dalali aliondolewa kugombea kwa sababu ya kukosa sifa ya Elimu ya kidato cha nne  huku Mwenykiti wa sasa wa DRFA ndugu Amin (AKA Bakhresa) na Nd Damas Ndumbaru wakiwa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyotekeleza na kuzingatia Kanuni za uchaguzi za TFF, aidha Nd A. Bulembo nae aliondolewa kwa vigezo hivyo hivyo katika uchaguzi wa timu Villa Squad ya DSM, kanuni haikuishia hapo iliendelea mpaka kwa timu ya Coastal Union  ya Tanga, kwa misingi hiyo ni wazi kamati hii haitafumbia macho kwenye hili la DRFA.
Aidha ninapenda kuikumbusha kamati yako kuwa Kamati ta uchaguzi ya TFF hivi karibuni ilisitisha chaguzi za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kutokana na dosari za Vyeti vya elimu kwa wagombea kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF
6.0    PINGAMIZI KWA MGOMBEA AMIN MOHAMED SALIM (AKA BAKHRESA
6.1        Mgombea mtajwa hapo juu ni mmoja wa wagombea ambae  jina lake limetajwa kupitishwa kugombea nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi wa DRFA, Katiba ya DRFA ibara ya 29(3) inamtaka  mgombea  kuwa na sifa zilizo ainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Elimu ya kidato cha Nne, aidha ibara ya 9 ya kanuni za Uchaguzi wa wanachama wa TFF inatamka ibara ya 9(2) amboyo ina tamka wazi kuwa mgombea yoyote lazima awe na  Elimu ya kidato cha nne inayo ambatana na cheti cha matokeo any person contesting any position “ Must have minimum academic qualification of form Four and holder of a certificate of ordinary Secondary Education” . Kwa kuzingatia maelezo na sifa za kanuni za uchaguzi wa wanachama wa TFF, Katiba na maagizo mbalimbali ya TFF na katiba ya DRFA Mgombea  mtajwa  Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA)   anakosa sifa ya kuwa mgombea Mwenyekiti wa DRFA kwa kuwa hana Elimu ya Kidato cha Nne kinachoambatana na cheti cha matokeo hivyo jina lake liondolewe katika orodha ya wagombea waliopitishwa kugombea uongozi wa  DRFA.
6.2        Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA)  hana sifa ya
 kugombea  kwa mujibu wa ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa  TFF “The person contesting any position in the association must have integrity and the capacity of performing  fulfilling and implementing Association obligations and objectives”  kwa sababu zifuatazo:
1.   20/01/1993 aligombea uongozi kwa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya FAT. Alijaza form ya maombi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutoa maelezo ya uongo ya kuwa ana elimu ya kidato cha nne na kutoa kiapo huku akijua maelezo yake ni ya uongo ANNEXED “A” Aidha pamoja na form hiyo Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA aliasilisha cheti cha kugushi kuwa amemaliza kidato cha Nne katika shule ya sekondari Tambaza (school living Certificate)mwaka  1974  huku akijua kuwa Hasemi ukweli  ANNEXED “B”
6.3              Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) huku akijua hasemi ukweli mwaka 1994/Dec/17 Katika form yake  ya kuomba uongozi FAT alieleza ya kuwa Amehitimu Darasa la Nane(STDVIII)  mwaka 1965 na mwaka huo huo akawa mchezaji wa Cosmopolitan akipingana na barua  aliyoiwasilisha mwaka 2000 kutoka  Wizara ya elimu ya Serekali ya mapinduzi Zanzibar ANNEXED “C” inayosema  kuwa Amemaliza miaka 8 ya mafunzo katika shule ya Msingi Darajani 1965 uhalali wa barua  hiyo unatia shaka hivyo inahitaji kuhakikiwa uhalisia wake.
6.4              Mwaka 2005 Ndugu AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA)   alifunguliwa  jarada la mashtaka ya kugushi maandishi na Nd OPIYO jalada CD/RB/6236/05 na CD/IR/2707/05  la kosa la kugushi vyeti jambo ambalo mlalamikaji yuko tayari kuwaslisha ushahidi mbele ya kamati yako
7.0   PINGAMIZI DHIDI YA WAPIGA KURA WAFUATAO
1.   ABEID MZIBA –KINONDONI
2.   SALEH NDONGA-TEMEKE
3.   PETER MUHINZI- TEMEKE
4.   DAUDI KANUTI- ILALA
5.   GUNGULUGWA TAMBAZA-ILALA
6.   Na wengine
Majina niliyo yataja hapo juu ni wajumbe na wanawakilishi wilaya zao katika mkutano mkuu wa DRFA, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF , maagizo mbalimbali ya TFF, katiba za mfano zilizotolewa na TFF pamoja Katiba  ya DRFA nilio wataja hapo juu wanakosa sifa za kuwakilisha wilaya katika mkutano mkuu wa DRFA kwa kukosa  Elimu ya Kidato cha Nne kinachoambatana na cheti cha matokeo.
Naomba kamati yako itamke kuwa viongozi hao walichaguliwa kimakosa bila kuzingatia kanuni za uchaguzi za TFF hivyo nafasi zao zitangazwe ziko wazi ili wapatikane watu wenye sifa za kikanuni kugombea, pia wasiruhusiwe kushiriki kupiga kura katika Uchaguzi wa DRFA, aidha ninapenda ufahamu jambo kama hili lilifanyika katika Uchaguzi wa Mkoa wa Mara(FAM) ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF taifa ilishiriki na ilitoa mwongozo na kusimamia utekelezaji wake.
Kwa kuzingatia Maelezo hayo hapo, Ninawasilisha pingamizi langu lenye sehemu tatu(3)   pamoja na nakala za maagizo mbali mbali ya TFF kwa wanachama wake:
8.0    Kwa kuzingatia Maelozo hayo hapo, Ninawasilisha katika maombi ya dharura  kama ifuatavyo:
(a)  Tamko kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila  kufuata  kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ivunjwe na kuundwa upya.
(b)  Tamko kuwa Mchakato mzima wa uchaguzi uanze upya mara baada ya Kamati mpya kuundwa.
(c)  Tamko katiba ya DRFA ina kinzana na katiba Kanuni na Maelekezo  ya TFF hivyo ifanyiwe   marekebisho. yanayostahili kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine.
(d)  Tamko la kufanyika kwa Uhakiki wa sifa za viongozi wa wanachama na wanachama washiriki wa DRFA ili kuridhia matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba za Mfano za wiliya zilizotolewa na TFF.
(e)  Tamko kuwa kuiruka kamati ya sheria na Katiba ya TFF  katika kuipitisha katiba ya DRFA ni ukiukwaji wa maagizo ya TFF
(f)   Jina  la Mgombea Nd AMIN MOHAMED SALIM (BAKHRESA) liondolewa kwenye orodha ya wagombea
(g)  Wapiga kura wote wasio na sifa ambao wamegombea waondolewe kwenye orodha ya wagombea.
(h)  Jambo au uwamuzi mwegine wowote ambao kamati itaona unafaa kwa maendeleo DRFA na taifa kwa Ujumla
………………………………….
MICHAEL RICHARD WAMBURA
MLALAMIKAJI/MPINGAJI
15th Sept, 2012
CC:Nd L.C Tenga Rais shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF)
CC: Nd  D. Lyatto  M/kiti Kamati ya Uchaguzi ya –TFF
CC: A Mgongolwa - Mwenyekiti-kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi
       za wachezaji

BANGO KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, TFF !

Release No. 149
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 19, 2012
KLABU LIGI KUU, WADHAMINI VODACOM KUTETA
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zimekubaliana kukutana na mdhamini (kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kuzungumzia kipengele cha mkataba wa ligi hiyo kinachozuia kampuni nyingine za mawasiliano kudhamini timu zinazocheza Ligi Kuu.
Maazimio hayo yalifikiwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika kikao kati ya klabu hizo na Kamati ya Ligi kilichofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wallace Karia.
Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.
Maazimio mengine ya kikao hicho ni TFF kuiandikia barua African Lyon ambayo itaipeleka kwa mdhamini wake (Zantel) ikielezea hatua hiyo ili kusimamisha udhamini huo wakati ikisubiri matokeo ya mazungumzo kati ya klabu hizo na mdhamini wa Ligi Kuu juu ya kipengele cha kuzuia washindani wa Vodacom.
Katika mkutano huo, watendaji wawili wa Kamati ya Ligi ambayo iko katika kipindi cha mpito kuelekea kuundwa kwa Bodi ya Ligi walitambulishwa kwa klabu hizo. Watendaji hao ni Silas Mwakibinga ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na Joel Balisidya ambaye ni Ofisa wa Ligi (LO).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MTIBWA SUGAR WALIVYOIGARAGAZA YANGA

Wachezaji wa Moro United wakishangilia baada ya kufunga goli lao la kwanza







MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam jana iliendelea kusuasua kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulambishwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mchezo huo ambao umekuwa na matokeo hasi kwa upande wa timu ya Jangwani ulianza kwa kwa timu kusomana lakini dakika ya 11 ya mchezo akaipatia timu yake ya Mtibwa bao la kuongoza, kabla ya Husseni Javu kuongeza la pili katika dakika ya 45 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na timu zikaenda mapumziko Mtibwa wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Yanga wakafanya mabadiliko kwa kuwaingiza Saimon Msuva na Stephano Mwasika kuchukua nafasi za Frank Domayo na David Luhende lakini haikusadia chochote. Dakika ya 66 akatoka Mbuyu Twitte na kuingia Didier Kavumbangu lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa upande wa vijana wa Jangwani.
Dakika ya 77 ya mchezo Husseni Javu aliiongezea Mtibwa inayonolewa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime bao la tatu kwa kumtungua golikipa Ally Mustapha Barthez.
Yanga ilikuwa ipate bao la kufutia machozi baada ya kupata penati dakika za lala salama na Mganda Hamis Kiiza 'Diego' alishindwa kufunga na kuifanya timu yake ipoteze mechi hiyo kwa mabao 3-0 na kusaliwa na pointi moja iliyopata katika mechi yake ya awali ya ufunguzi dhidi ya maafande wa Prisons ya Mbeya.
Katika mechi hiyo ya awali, kocha wa Yanga, Tom Saintfeit alitoa visingizio kadhaa vilivyofanya washindwe kuwafunga Prisons, kwa matokeo hayo mashabiki wanasubiri kumsikia kocha huyo ataibuka na jambo gani tena baada ya kipigo hicho cha aibu na cha kwanza kwake katika mechi za ligi.

 

Picha:kwa Hisani ya Staikamkali.blogspot.com


 



SIMBA wazidi kutaka Ligi Kuu yawapigisha kwata maafande wa JKT Ruvu

 

Emannuel Okwi akiwa amembeba mchezaji mwenzake wakishangilia moja ya mabao yao jana

Heka heka za Okwi kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu

 

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba jana wameendeleza makali yao waliyoanza nayo msimu huu baada ya kuitandika timu ya maafande wa JKT Ruvu mabao 2-0 katika mfululizo wa ligi hiyo, mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa.
Simba ambao walicheza mchezo kwa dakika nyingi baada ya mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza cha mchezo, walipata mabao yao kutoka kwa kiungo Amri Kiemba aliyefunga bao la kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga kidude cha pili.
Kadi hiyo ya Okwi ilimfanya kocha mkuu wa Simba, Cirkovic Milovan kuilalamikia, ingawa mazingira ya tukio yanayoonyesha Mganda huyo alistahili kabisa. 
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya pointi 6, magoli matano ya kufunga na wakiwa hawajuruhusu nyavu zao kuguswa. Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa 3 - 0 dhidi ya African Lyon.
Kwa upande mwingine huko jijini Mwanza Azam FC wametoka sare ya kufungana 2-2 na Toto Africa, wakati Tanzania Prisons wametoka 1 - 1 na Coastal Union ya Tanga, huku Coastal wakilalamika kunyimwa bao murua lililofungwa na Atupele Green, wakati mjini Bukoba, Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, na Ruvu Shooting wakiifunga Mgambo JKT 2-1.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea keshokutwa na Jumapili kwa mechi za raundi ya tatu.



HAYA NDIO MABASI MAPYA YA KISASA YA SIMBA NA YANGA WALIYOPEWA NA MDHAMINI WAO

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.
KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager hatimaye inatarajia kukabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga siku ya Ijumaa asubuhi.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja vya ofisi za TBL Ilala.

“Zaidi ya wageni 100 wamealikwa kwenye hafla hii itakayofanyika Ijumaa hapa TBL na kati ya hawa wageni kutakuwa na baadhi ya mashabiki wa timu hizi mbili kwa hivyo tunatarajia makabidhiano ya aina yake,” alisema Kavishe.

Kwa mujibu wa ratiba, baada ya makabidhiano, kila timu itaondoka na basi lake na wachezaji na mashabiki na kupita katika matawi yao kwa msafara maalumu utakaoambatana na burudani mbalimbali huku mashabiki wa timu hizi wakitarajiwa kuyapokea mabasi hayo na kuwashangilia wachezaji wakipita katika matawi.

Msafara wa timu ya Simba ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Vuvuzela lililopo Makao Makuu ya klabu hiyo Kariakoo Mtaa wa Msimbazi kisha utaelekea katika Tawi la Magomeni Mpira Pesa, Ubungo katika kituo cha mabasi na hatimaye Tawi la Wailes Temeke.

Msafara wa Yanga nao ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Ubungo katika kituo cha mabasi na kuelekea katika Tawi la Manzese, Lango la Jiji Magomeni, Buguruni, Mwembe Yanga, Mtoni kwa Aziz Ali, Mkombozi na hatimaye kumalizia katika makao makuu ya Jangwani, Kariakoo.

"Tunawaomba mashabiki wa timu hizi mbili wajitokeze kwa wingi katika matawi yao ili wajionee mabasi haya mapya ambayo ni ya kisasa na pia wapate fursa ya kukutana na wachezaji wa timu zao," alisema Kavishe.

Kilimanjaro Premium Lager imedhamini klabu hizi hivi tangu mwaka 2008.


Source/http://straikamkali.blogspot.com