STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 20, 2012



SIMBA wazidi kutaka Ligi Kuu yawapigisha kwata maafande wa JKT Ruvu

 

Emannuel Okwi akiwa amembeba mchezaji mwenzake wakishangilia moja ya mabao yao jana

Heka heka za Okwi kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu

 

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba jana wameendeleza makali yao waliyoanza nayo msimu huu baada ya kuitandika timu ya maafande wa JKT Ruvu mabao 2-0 katika mfululizo wa ligi hiyo, mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa.
Simba ambao walicheza mchezo kwa dakika nyingi baada ya mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza cha mchezo, walipata mabao yao kutoka kwa kiungo Amri Kiemba aliyefunga bao la kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga kidude cha pili.
Kadi hiyo ya Okwi ilimfanya kocha mkuu wa Simba, Cirkovic Milovan kuilalamikia, ingawa mazingira ya tukio yanayoonyesha Mganda huyo alistahili kabisa. 
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya pointi 6, magoli matano ya kufunga na wakiwa hawajuruhusu nyavu zao kuguswa. Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa 3 - 0 dhidi ya African Lyon.
Kwa upande mwingine huko jijini Mwanza Azam FC wametoka sare ya kufungana 2-2 na Toto Africa, wakati Tanzania Prisons wametoka 1 - 1 na Coastal Union ya Tanga, huku Coastal wakilalamika kunyimwa bao murua lililofungwa na Atupele Green, wakati mjini Bukoba, Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, na Ruvu Shooting wakiifunga Mgambo JKT 2-1.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea keshokutwa na Jumapili kwa mechi za raundi ya tatu.

No comments:

Post a Comment