STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 20, 2012

MTIBWA SUGAR WALIVYOIGARAGAZA YANGA

Wachezaji wa Moro United wakishangilia baada ya kufunga goli lao la kwanza







MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam jana iliendelea kusuasua kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulambishwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mchezo huo ambao umekuwa na matokeo hasi kwa upande wa timu ya Jangwani ulianza kwa kwa timu kusomana lakini dakika ya 11 ya mchezo akaipatia timu yake ya Mtibwa bao la kuongoza, kabla ya Husseni Javu kuongeza la pili katika dakika ya 45 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na timu zikaenda mapumziko Mtibwa wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Yanga wakafanya mabadiliko kwa kuwaingiza Saimon Msuva na Stephano Mwasika kuchukua nafasi za Frank Domayo na David Luhende lakini haikusadia chochote. Dakika ya 66 akatoka Mbuyu Twitte na kuingia Didier Kavumbangu lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa upande wa vijana wa Jangwani.
Dakika ya 77 ya mchezo Husseni Javu aliiongezea Mtibwa inayonolewa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime bao la tatu kwa kumtungua golikipa Ally Mustapha Barthez.
Yanga ilikuwa ipate bao la kufutia machozi baada ya kupata penati dakika za lala salama na Mganda Hamis Kiiza 'Diego' alishindwa kufunga na kuifanya timu yake ipoteze mechi hiyo kwa mabao 3-0 na kusaliwa na pointi moja iliyopata katika mechi yake ya awali ya ufunguzi dhidi ya maafande wa Prisons ya Mbeya.
Katika mechi hiyo ya awali, kocha wa Yanga, Tom Saintfeit alitoa visingizio kadhaa vilivyofanya washindwe kuwafunga Prisons, kwa matokeo hayo mashabiki wanasubiri kumsikia kocha huyo ataibuka na jambo gani tena baada ya kipigo hicho cha aibu na cha kwanza kwake katika mechi za ligi.

 

Picha:kwa Hisani ya Staikamkali.blogspot.com


 

No comments:

Post a Comment