STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 28, 2014

Tanzia! Muimbaji Issa Nundu afariki, kuzikwa leo Moshi

Issa Nundu wa tatu toka kulia akiwa na wanamuziki wenzake wa Marquiz
MUIMBAJI nyota wa zamani aliyewahi kuzifanyia kazi bendi kadhaa zikiwamo Orchestra Marquis, MK Group, Makassy, Le Capital Wazee Sugu amefariki katika hospitali ya KCMC Moshi.
Issa ambaye alianza kuugua muda mrefu na kukutwa na tatizo la kusinyaa ubongo, aliamua kurudi kwao Kongo, lakini alipofika Kigoma alizidiwa na kulazwa huko ambako alihamishiwa KCMC Moshi kwa matibabu zaidi. 
Issa ambaye jina lake halisi ni Jackson Issa Nundu atazikwa Moshi leo Jumanne ikiwa taratibu zote zitakamilika. 
Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa,
Mungu Aiweke Roho ya Marehemu Issa Nundu Mahali Pema. Ameen

Dokii ajiandaa kutoka na mbili mpya

NYOTA wa filamu aliye muimbaji pia, Ummy Wenceslaus 'Dokii' amekamilisha nyimbo mbili mpya ' Hakuna Kama Mwanamke' na 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Dokii alisema nyimbo hizo alizozipiga katika mondoko ya Afro Reggae na Afro Dance, zimerekodiwa katika studio mbili tofauti.
Dokii alisema wimbo wa 'Hakuna Kama Mwanamke' amerekodia katika studio za Recho Records chini ya mtayarishaji aitwayo Shivo na huo mwingine umetengenezwa chini ya studio za Akhenato Records chini ya Lil Ghetto.
"Nimekamilisha nyimbo mbili kwa mpigo na mojawapo nitauachia hadharani hivi karibuni ikiwa ni ujio mpya wa Dokii," alisema muigizaji huyo aliyeanzia kutamba kwenye michezo ya runinga kabla ya kujikita kwenye muziki na filamu.
Dokii alisema wimbo aliopanga kuutanguliza hewani ni 'Hakuna Kama Mwanamke' kabla ya 'Nampenda Dereva wa Bodaboda' kufuata ila alidai lolote linaweza kutokea kwa wimbo wowote kuutangulia mwingine.
Kazi hizo mpya zinakuja baada ya Dokii kutamba na 'Obama Welcome Tanzania' na 'No One Like Obama'.

Hii ndiyo orodha ya watakaowania tuzo ya FIFA Ballon d'Or

http://static.guim.co.uk/sys-images/Guardian/Pix/audio/video/2014/1/13/1389648809158/Cristiano-Ronaldo-011.jpg
Mshindi aliyepita wa tuzo ya Mwanasoka Bora Duniani
ORODHA ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora ya Fifa Ballon d'Or imetoka. 
Mchujo wa kupata wachezaji watatu utafanyika mwezi Disemba na mshindi kutangazwa Januari 12 2015.
Orodha yenyewe na timu wanazochezea  ni kama ifuatavyo: Gareth Bale (Wales, Real Madrid), Karim Benzema (France, Real Madrid), Diego Costa (Spain, Chelsea), Thibaut Courtois (Belgium, Chelsea), Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina, Manchester United), Mario Gotze (Germany, Bayern Munich) na Eden Hazard (Belgium, Chelsea).
Wengine ni; Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris St-Germain), Andres Iniesta (Spain, Barcelona), Toni Kroos (Germany, Real Madrid), Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich), Javier Mascherano (Argentina, Barcelona) na Lionel Messi (Argentina, Barcelona).
Pia wamo Thomas Muller (Germany, Bayern Munich), Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich), Neymar (Brazil, Barcelona), Paul Pogba (France, Juventus), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid), Arjen Robben (Netherlands, Bayern Munich), James Rodriguez (Colombia, Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Germany, Bayern Munich), Yaya Toure (Ivory Coast, Manchester City).