STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 28, 2014

Dokii ajiandaa kutoka na mbili mpya

NYOTA wa filamu aliye muimbaji pia, Ummy Wenceslaus 'Dokii' amekamilisha nyimbo mbili mpya ' Hakuna Kama Mwanamke' na 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Dokii alisema nyimbo hizo alizozipiga katika mondoko ya Afro Reggae na Afro Dance, zimerekodiwa katika studio mbili tofauti.
Dokii alisema wimbo wa 'Hakuna Kama Mwanamke' amerekodia katika studio za Recho Records chini ya mtayarishaji aitwayo Shivo na huo mwingine umetengenezwa chini ya studio za Akhenato Records chini ya Lil Ghetto.
"Nimekamilisha nyimbo mbili kwa mpigo na mojawapo nitauachia hadharani hivi karibuni ikiwa ni ujio mpya wa Dokii," alisema muigizaji huyo aliyeanzia kutamba kwenye michezo ya runinga kabla ya kujikita kwenye muziki na filamu.
Dokii alisema wimbo aliopanga kuutanguliza hewani ni 'Hakuna Kama Mwanamke' kabla ya 'Nampenda Dereva wa Bodaboda' kufuata ila alidai lolote linaweza kutokea kwa wimbo wowote kuutangulia mwingine.
Kazi hizo mpya zinakuja baada ya Dokii kutamba na 'Obama Welcome Tanzania' na 'No One Like Obama'.

No comments:

Post a Comment