STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 8, 2016

Man City kumekucha! Yaingia vita ya kumwania Aubameyang

https://i.guim.co.uk/img/media/aa83556e4ff4a53c273d8fc73c14e1e6bd7105d7/0_80_3000_1800/master/3000.jpg?w=620&q=85&auto=format&sharp=10&s=53bd60055f2d7d1fab6d5d30c9526dd8KLABU ya Manchester City inadaiwa ipo mbioni kuingia kwenye orodha ya timu zinazomwania straika wa Borussia Dortmund ma Mchezaji Bora wa Afrika 2015, Pierre-Emerick Aubameyang.
City wana matumaini ya kumsana nyota huyo wa kimataifa wa Gabon mwenye umri wa miaka 26 katika kipindi hiki cha kiangazi. Aubameyang anatajwa kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora Ulaya baada ya kuonyesha kiwango kikubwa Dortmund akifunga mabao 39 katika mashindano yote msimu uliopita.
Meneja mpya wa klabu hiyo, Pep Guardiola anafahamu vyema kipaji cha Aubameyang na ameona kuwa anaweza kumfaa katika mipango yake ya baadae. City wanadaiwa kuwa tayari kumsaidia Guardiola katika usajili kwa kujiandaa kuvunja rekodi ya usajili kwa kumleta nyota huyo Etihad.

Leseni za klabu zimeanza kutolewa na TFF, mshindwe ninyi

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/04/Rais-wa-Shirikisho-la-Mpira-wa-Miguu-Jamal-Malinzi-akioneshwa-kukerwa-na-waamuzi-kuuza-mechi.jpg
Rais wa TFF, Malinzi
NA ALFRED LUCAS
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za Leseni za Klabu (Club Licensing) za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.
Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya Juni 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatuamia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema.
Tayari TFF imeteua Kamati ya Leseni ya Klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.
Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.
Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.
Kwa klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala (administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.

Serengeti Boys kambini kuisubiri Shelisheli

http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/2016/03/21/serengeti%20boys.jpg?itok=F-SUOdMWNA ALFRED LUCAS
TIMU ya soka ya taifa ya vijana U17 'Serengeti Boys' inataingia kambini Juni 13, 2016 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba  ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Haishangazi nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani zimeulizia uwezekano wa timu hii kutembelea nchi zao kwa michezo ya kirafiki.
Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.

Rais Obama ayakosa mazishi ya Muhammad Ali

http://cdn-mf1.heartyhosting.com/sites/mensfitness.com/files/styles/photo_gallery_full/public/ali_rotator.jpg?itok=CnLNStFo
Muhammad Ali enzi za uhai wake
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/06/382dab0f0ef23504d829de029e0e543f-702x336.jpgMWILI wa bingwa mara wa tatu wa Dunia kwa uzito wa juu, Muhammad Ali unatarajiwa kuzikwa keshokutwa Ijumaa, lakini cha kusikitisha ni kwamba hatazikwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
Muingiliano wa mazishi hao wa shujaa huyo na mwanaharakati wa kuwatetea watu weusi kupitia ngumi, kiasi kwamba leo Marekani inaongozwa na Rais mwenye asili ya Afrika na yale ya mahafali za binti wa Obama ndio sababu ya Obama kukosa mazishi hao.
Viongozi kadhaa kutoka sehemu mbalimbali duniani watakuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji watakaohudhuria mazishi hayo huko Louisville, Kentucky ambako Ali alizaliwa mwaka 1942.
Ikulu ya Marekani imesema kuwa Obama na mkewe Michelle wanatarajiwa kuwa katika mahafali ya binti yao Malia huko Washington, DC.
Ali alifariki dunia wiki iliyopita hospitalini huko Phoenix, Arizona akiwa na umri wa miaka 74.
Hata hivyo familia ya Obama inatarajia kutuma barua kwa familia ya Ali ambayo itawasilishwa na mshauri mwandamizi wa Ikulu Valerie Jarrett ambaye anamfahamu Ali.
Msemaji wa familia ya Ali, Bob Gunnell amesema Obama alizungumza na mjane wa Ali, Lonnie katika simu kumpa pole kwa kifo hicho cha mumewe. Miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Mfalme Abdullah wa Jordan.

Jose Mourinho aanza mambo Man United

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/styles/article_large/public/thumbnails/image/2016/06/08/13/eric-bailly-2.jpg
Eric Bailly
MBONA mtamkoma. Kocha Mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho ameanza makeke yake baada ya klabu yake kumnasa beki wa Villarreal, Eric Bailly.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na United kwa ada ya Pauni Milioni 30 na kupewa mkataba wa miaka minne.
Akihojiwa Bailly amesema ndoto zake zimetimia za kujiunga na United na kucheza soka katika kiwango cha juu kama siku zote alivyotaka iwe.
Kocha Mourinho amesema Bailly ana nafasi kubwa ya kuja kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.
Bailly alijiunga na Villarreal kwa kitita cha Pauni Milioni 4.4 Januari mwaka 2015 na kucheza katika kila mechi wakati Ivory Coast ikishinda taji la Mataifa ya Afrika wiki chache baadae.
Huo unakuwa usajili wa kwanza wa Mourinho toka atue Old Trafford huku pia wakitajwa kumwania pia mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic.

Malinzi amlilia Stephen Keshi aliyefariki leo

http://stargist.com/wp-content/uploads/2014/05/Stephen-Keshi-Stargist.jpg
Keshi enzi za uhai wake
NAHODHA na Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi amefariki dunia ghafla leo Jumatano na kuleta mshtuko mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini humo na kwingineko Afrika.
Nchini Tanzania  Rais wa Shirikisho la Soka(TFF), Jamal Malinzi naye ni miongoni mwa walioshtushwa na kifo hicho na kuweka bayana alivyopokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo0 wa Keshi (54) na kutuma salamu zake za pole. Rais Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), Amaju Pinnick, familia ya marehemu Keshi pamoja na ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata kuwa nahodha wa kikosi cha Taifa Nigeria ‘Super Eagles’.
Katika rambirambi ambazo zimefika pia katika Ofisi za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Rais Malinzi amesema kuwa japo Keshi ametangulia mbele za haki, mchango wake kwenye soka hautasahaulika kwani atabaki kuwa alama ya maendeleo ya mchezo wa soka.

Benteke ambeep Klopp, atasepa kama atamzingua

http://i3.mirror.co.uk/incoming/article6908832.ece/ALTERNATES/s615b/Liverpool-vs-Bordeaux-Europa-League-Group-Stage.jpg
Benteke
ANAONDOKA. Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke amesema anataka kubakia Liverpool, lakini amekiri anaweza kuangalia mahali pengine kama hatakuwepo katika mipango ijayo ya Kocha Jurgen Klopp.
Strika huyo aliyepo na kikosi chao kwenye fainali za Kombe la Ulaya Euro 2016, alijiunga na Liverpool akitokea Aston Villa kwa kitita cha Pauni Milioni 32.5 kiangazi mwaka jana.
Mkataba wake ulikuwa wa miaka mitano lakini amekuwa akishindwa kuonyesha cheche zake Anfield tangu Kocha Klopp alipomrithi Branden Rodgers.
Nyota huyo bado anapenda kuendelea kubakia hapo, lakini kama atakuwa nje ya mipango ya Klopp anaweza kuangalia mahali pengine atakapoweza kupata nafasi ya kucheza.
Akihojiwa Benteke amesema akiwa na umri wa miaka 25 sasa sio kwamba ni mkubwa sana au mdogo lakini muhimu ni kupata muda mwingi wa kucheza.

Didier Kavumbagu anukia Mbeya City

Didier Kavumbagu (kulia) akiwa na nyota wenzake wa Azam FC
NYOTA wa timu ya Taifa ya Burundi ‘Intamba Mu rugamba’ Didier Kavumbagu anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kutangazwa kujiunga na kikosi cha Mbeya City Fc ya jijini Mbeya kinachoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara muda wowote kuanzia sasa.
Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe, mchana huu ameidokeza mtandao wa mbeyacityfc.com kuwa mazungumzo ya kumnasa nyota huyo wa timu ya taifa ya Burundi aliyekuwa akicheza kwenye kikosi cha Azam Fc ya jijini Dar es Salaam msimu uliomalizika yako kwenye hatua nzuri na tayari wakala wa mchezaji huyo amekwishaainisha yale yote muhimu yanayohitaji kwa ajili ya kuipata huduma yake likiwemo suala la kipengele cha kumruhusu kwenda kufanya majaribio nje ya nchi endapo yatapatikana.
“Tulianza mchakato wa kumpata Kavumbagu mapema kabisa, baada ya kukwama kwenye dirisha dogo Januari mwaka huu, tulikubaliana kuwa hitimisho litakuwa kwenye majira haya ya kiangazi, tayari nimezungumza na wakala wake, tuko kwenye hatua za mwisho kwa sababu ameshaanishia yale yote yanayohitajika, kwa maana hiyo basi, endepo tutamalizia vizuri hatua iliyobaki, muda wowote kuanzia sasa tunaweza kumtangaza kama mchezaji wetu," alisema Kimbe.
Akiendelea zaidi Kimbe alisema kuwa, Kavumbagu ni moja ya nyota walio kwenye orodha ya kocha Kinnah Phiri aliyoomba wasajiliwe ili kuiimarisha timu kwenye eneo la ushambuliaji akilenga kuwa wachezaji wenye uwezo wa kufunga kufuatia tatizo la umaliziaji lililoikuba City  kwenye michezo kadhaa ya mzunguko wa pili wa ligi  licha ya kucheza vizuri kwenye maeneo mengine.
“Tunayo majina  kadhaa ambayo kocha wetu ameomba wasajiliwe kulingana na mahitaji aliyonayo, Kavumbagu anaweza kuwa  wa kwanza kati yao,wengine watafuata kwa mujibu wa taratibu zetu, tunataka kufanya usajili makini ili kuimarisha timu na hatimaye tuwe na kikosi kitakachotupatia matokeo mazuri msimu ujao  hii ni baada ya mapito msimu uliopita”.
Kavumbagu  alianza kuichezea timu ya taifa ya Burundi mwaka 2009 na alikuwa mmoja wa nyota waliokiwakilisha kikosi hicho  kwenye michezo ya kutafuta kufuzu Kombe la Mataifa Afrika 2012 na kufunga mabao 2.
Kwa upande  mwingine   Kimbe  amedokeza kuhusu nyota ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha City msimu ujao, na kusema kuwa  ni vizuri kuendelea kusubiri  kwa sababu muda si mrefu  taarifa  juu ya hilo itatolewa.

Simba kweli imepania yasajili nyota wapya kimyakimya

Wachezaji wa Simba wakishanglia moja ya mabao yao katika ligi iliyoisha hivi karibuni
http://3.bp.blogspot.com/-Ipu0ia4uDWg/U7A1me4yA1I/AAAAAAABBX4/VGLiaBprUbI/s1600/_FDA0288.JPG
Rais wa Simba, Evans Aveva na Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zakari Hanspoppe
KLABU ya Simba wajanja kwelikweli. Baada ya viongozi wa klabu hiyo kubaini kuwa, wanachama wao wana hasira kwa sababu timu yao haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tangu mwaka 2011-2012, wameamua kufanya yao.
Wakienda na mwendo wa kimya kimya, viongozi hao wamefanya usajili kamambe bila makeke, kitu ambacho wapinzani wao Yanga na Azam ni lazima wakae chonjo kwa ligi ya msimu ujao.
Viongozi wa Simba ambao wanadaiwa wapo mbioni kuleta vifaa vya kimataifa kutoka Zimbabwe na Malawi, wamewanyakua nyota kadhaa wa klabu mbalimbali za Ligi Kuu Bara wakiwamo kutoka Mtibwa Sugar na Mwadui FC.
Wachezaji hao wameshasaini na kupewa mikataba yao, licha ya kwamba zile mbwembwe ambazo zimezoeleka kipindi kama hiki kwa klabu hiyo katika usajili zimewekwa kando ili kuhakikisha wachezaji wanaowataka wanawatia mkononi.
Micharazo inayo majina ya wachezaji wanne wapya waliosainiwa Msimbazi akiwamo kiungo mmoja fundi, ambaye katika ligi iliyomalizika alifanya yake akiifungia mara kadhaa Mtibwa mabao muhimu.

Kazi hiyo inafanywa kwa ushirikiano mkubwa baina ya matajiri wa Simba na Kamati ya usajili ya klabu hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Zakaria Hanspoppe kwa mapendekezo ya kocha Jackson Mayanja na Benchi lake la Ufundi.
Mkali mwingine ni kiberenge kilichowahi kutamba Azam Fc, huku beki aliyekuwa akiwindwa na timu hiyo kutoka Mwadui, Idd Mobby ikielezwa amepotezewa, kwa sababu analetwa fundi mmoja toka Malawi atakayechukua nafasi ya Juuko Murshid.