STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 8, 2016

Simba kweli imepania yasajili nyota wapya kimyakimya

Wachezaji wa Simba wakishanglia moja ya mabao yao katika ligi iliyoisha hivi karibuni
http://3.bp.blogspot.com/-Ipu0ia4uDWg/U7A1me4yA1I/AAAAAAABBX4/VGLiaBprUbI/s1600/_FDA0288.JPG
Rais wa Simba, Evans Aveva na Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zakari Hanspoppe
KLABU ya Simba wajanja kwelikweli. Baada ya viongozi wa klabu hiyo kubaini kuwa, wanachama wao wana hasira kwa sababu timu yao haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tangu mwaka 2011-2012, wameamua kufanya yao.
Wakienda na mwendo wa kimya kimya, viongozi hao wamefanya usajili kamambe bila makeke, kitu ambacho wapinzani wao Yanga na Azam ni lazima wakae chonjo kwa ligi ya msimu ujao.
Viongozi wa Simba ambao wanadaiwa wapo mbioni kuleta vifaa vya kimataifa kutoka Zimbabwe na Malawi, wamewanyakua nyota kadhaa wa klabu mbalimbali za Ligi Kuu Bara wakiwamo kutoka Mtibwa Sugar na Mwadui FC.
Wachezaji hao wameshasaini na kupewa mikataba yao, licha ya kwamba zile mbwembwe ambazo zimezoeleka kipindi kama hiki kwa klabu hiyo katika usajili zimewekwa kando ili kuhakikisha wachezaji wanaowataka wanawatia mkononi.
Micharazo inayo majina ya wachezaji wanne wapya waliosainiwa Msimbazi akiwamo kiungo mmoja fundi, ambaye katika ligi iliyomalizika alifanya yake akiifungia mara kadhaa Mtibwa mabao muhimu.

Kazi hiyo inafanywa kwa ushirikiano mkubwa baina ya matajiri wa Simba na Kamati ya usajili ya klabu hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Zakaria Hanspoppe kwa mapendekezo ya kocha Jackson Mayanja na Benchi lake la Ufundi.
Mkali mwingine ni kiberenge kilichowahi kutamba Azam Fc, huku beki aliyekuwa akiwindwa na timu hiyo kutoka Mwadui, Idd Mobby ikielezwa amepotezewa, kwa sababu analetwa fundi mmoja toka Malawi atakayechukua nafasi ya Juuko Murshid.

No comments:

Post a Comment