STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 13, 2013

BREAKING NEWS: MSANII LANGA KILEO AFARIKI DUNIA


HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa nyota wa zamani wa Coca Coca Pop Stars na mkali wa miondoko ya Hop Hop, Langa Kileo (Pichani) amefariki dunia.
Habari hizo zinadai  kuwa msanii huyo alikumbwa na Malaria kali sana hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana na kukumbwa na mauti.
Tunaendelea kufuatilia kujua ukweli na kama ni kweli tunamuomba Mungu aipokee roho ya marehemu na tunatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa msanii huyo ambaye hivi juzi tu alinukuliwa akiwa mbioni kuachia video ya wimbo wake mpya wa 'Rafiki wa Kweli' baada ya kupona katika janga la matumizi ya dawa za kulevya.

Fabregas azikata maini Man Utd, Arsenal

Cesc Fabregas

KIUNGO Cesc Fabregas amevunja ukimya na kusema kwamba hana mpango wa kuondoka Nou Camp, licha ya tetesi za kuwaniwa na mabingwa wa England, Manchester Utd na klabu yake ya zamani Arsenal.
Fabrega, 26, amesema licha ya tetesi hizo mipango yake ni kusalia Barcelona kipindi hiki cha majira ya Joto.
Alisema "Siku zote nimekuwa zikisema najisikia furaha kuwepo Barca. Wanaosema naondoka hawanijui na wala hawajazungumza nami,"
Akaongeza hakuna aliyezumnguza na wakala wale kwa sababu anajua namna gani sipendi azungumze na watu wengine kuhusu mimi.
Nyota huyo wa Hispania alisema huwa hapendi mambo yake binafsi kuwaambia wengine na hata hilo analopakaziwa sasa la kutaka kurejea Ligi Kuu ya England hajaiambia hata familia yake.
"Iwapo mtu mmoja amesema lolo kuhusu hilo amekosea, nataka kuendelea kucheza Barca, hivi ndivyo ilivyo," alisema Fabregas alikyehama Arsenal kutoa Barcelona Agosti 2011 kwa kitita cha Paundi Mil 30.

TFF yawafungia waamuzi watatu, kisa...!





Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungia miezi mitatu waamuzi watatu walioshindwa kuchezesha mechi namba 32 ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Mpwapwa Stars ya Dodoma na Machava FC ya Kilimanjaro iliyokuwa ichezwe Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

TFF kupitia Kamati yake ya Waamuzi iliyokutana katika kikao chake cha Juni 12 mwaka huu kupitia taarifa mbalimbali za waamuzi wa RCL ilibaini makosa yaliyofanywa na baadhi ya waamuzi na kuyatolea uamuzi.

Waamuzi hao waliofungiwa ambao wanatoka mkoani Singida ni Jilili Abdallah, Amani Mwaipaja na Theofil Tegamisho. Wamefungiwa kwa kutoripoti katika kituo walichopangiwa (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma) na kutoa taarifa ya uongo kwa kushirikiana na Kamishna wa mechi hiyo.

Kanuni iliyotumika kuwafungia ni ya 28 kifungu (d) na (g) ya Ligi za TFF, na adhabu hiyo imeanza Juni 13 mwaka huu. Waamuzi hao pamoja na kamishna badala ya kwenda Uwanja wa Jamhuri, wao walikwenda kwenye Uwanja wa Mgambo ulioko Mpwapwa na kuandika ripoti iliyoonesha kuwa timu ya Machava FC haikufika uwanjani wakati wakijua kuwa mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa katika Uwanja wa Jamhuri.


Mhe Sugu, Sir Nature kumpiga tafu Anaconda Nyumbani Lounge

Jide katika pozi
MMOJA wa waasisi wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini-ChADEMA, Mhe. Joseph Mbilinyi, Sir Juma Nature na Komandoo Hamza Kalala ni baadhi ya watakaomsindikiza onyesho la Lady Jaydee 'Anaconda' katika maadhimisho ya miaka 13 tangu ajitose kwenye fani hiyo.
Onyesho hilo la Anaconda maarufu kama Binti Machozi a.k.a Comandoo litafanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge kuanzia saa 3 usiku ambapo mwanadada huyo ameanika hadharani mipango mizima ya onyesho lake hilo.
Kwa mujibu Jide kupitia akaunti yake ya Twitter ni kwamba kesho atapigwa tafu na Mh Sugu, mmoja wa watu waliomuibua kisanii.
Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani, na pia uwepo wa Sugu.
” Miaka 13 ya Lady JayDee, Ijumaa ya kesho shughuli inaanza rasmi saa 3:00 usiku...Ukiskia paaaa ujue show imeisha

1. Prof Jay 2. Juma Nature 3. Grace Matata 4. Hamza Kalala 5. Wakazi na ugeni wa Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU

Nyimbo zote unazozipenda zitalia tar 14 June, pale Nyumbani Lounge sababu yaaaaa sababu yaaaaaa ?????????”
Sidhani kama utaikosa hafla hiyo ambayo itatumika pia kusimikwa rasmi kwa Jide jina la 'Komandoo' na mkongwe Hamza Kalala.

Ivory Coast wakitarajia kutua leo, tiketi za pambano la Stars kuanza kuuzwa kesho

Wanaume wa Tanzania watakawakabili Tembo wa Ivory Coast Jumapili Taifa
Na Boniface Wambura
WAKATI timu ya Ivory Coast inatarajiwa kuwasili leo usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, tiketi kwa ajili ya mechi kati yake na Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa zinaanza kuuzwa kesho mchana (Juni 14 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Vituo vitakavyotumika kwa mauzo hayo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.

Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, sh. 7,000 viti vya rangi ya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Pia viti 100 vilivyo katika sehemu ya Wageni Maalumu (VVIP) vitauzwa kwa sh. 50,000 kila kimoja. Tiketi hizo zitauzwa katika ofisi za TFF, na watakaonunua watapewa kadi maalumu zenye majina yao, majina ambayo pia watayakuta katika vita watakavyokaa. Kwa maana hiyo hakutakuwa pasi maalumu (free pass) za kuingia VVIP.

TFF yampongeza Rais mpya ZFA

Rais wa TFF, Leodger Tenga
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza Rais mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina aliyechaguliwa katika uchaguzo mdogo uliofanyika hivi karibuni.

Amesema ushindi aliopata Faina unaonyesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA walivyo na imani naye katika kuhakikisha maendeleo ya mpira wa miguu visiwani humo.

Rais Tenga amesema ni imani yake kuwa Rais Faina ataendeleza ushirikiano uliopo kati ya TFF na ZFA kwa ajili ya ustawi wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumtakiwa kila kheri katika wadhifa wake huo mpya.

Musonye afichua walijua Tanzania haitashiriki Kagame 2013

http://kigalisports.com/wp-content/uploads/2012/11/Nicholas-Musonye-2-300.jpg
Katibu Mkuu wa Musonye
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholas Musonye amesema kuwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itafanyika nchini Sudan kama ilivyopangwa lakini mwaka huu klabu za Tanzania hazitashiriki katika michuano hiyo.
Akizungumza na NIPASHE kwa simu jana, Musonye alisema kuwa walishajua mapema kwamba Tanzania haiko tayari klabu zake zishiriki katika mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2 nchini Sudan, hivyo wataendelea na timu kutoka mataifa mengine.
"Tulijua mapema kwamba klabu za Tanzania hazitashiriki michuano hii baada ya serikali ya nchi hiyo kuingiwa na hofu ya usalama wa nchi ya Sudan ambako mashindano ya mwaka huu yanafanyika. Tutaendelea na timu ambazo ziko tayari kushiriki," alisema Musonye.
"Hata kama waziri asingesema leo (jana), tulishajua tangu mapema kuwa hawashiriki, lakini watambue kwamba michuano hii ina kanuni zake, ukizikiuka unaadhibiwa, aliongeza Katibu Mkuu huyo." Hata hivyo, Kenya ambayo ilikuwa inawakilishwa na klabu ya Tusker, nayo ilishatuma barua Cecafa kujitoa katika michuano hiyo.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, mwaka huu yamepangwa kuchezwa katika miji miwili ya Kadugli, uliopo Kordofan Kusini na Alfashery, uliopo Darfur Kaskazini, eneo ambalo kwa muda mrefu limekumbwa na vita vya wenyeji.
Juni Mosi mwaka huu akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika kuchangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo, Bernard Membe alisema kuwa hali ya usalama mjini Darfur ni ya wasiwasi kwa sababu watu wanaokwenda huko wanapokewa na vikosi vya magari ya jeshi na huvishwa nguo ambazo hazipenyezi risasi.
Timu tatu za Tanzania wakiwamo mabingwa watetezi wa kombe hilo, Yanga, mabingwa wa mwaka jana, Simba na Super Falcon ya Zanzibar ni miongoni mwa timu 13 zilizotakiwa kushiriki katika michuano hiyo mwaka huu.
Mapema jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema kuwa baada ya kuzungumza na Waziri Membe jana asubuhi Bungeni Mjini Dodoma na kuelezwa kuwa hali ya usalama Darfur ni mbaya, hayuko tayari kupeleka timu yake katika mashindano hayo.
"Nimezungumza na Waziri Membe na Naibu Waziri wa Wizara yenye dhamana na michezo (Amos Makalla) leo (jana). Waziri Membe amesema Sudan si shwari, hivyo klabu ya Simba haitapeleka timu katika michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu. Hilo ndilo tamko rasmi la Simba baada ya kuhakikishiwa na waziri," alisema Rage, ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM).
Hata hivyo, simu ya Waziri Membe ilikuwa haipatikani jana kuzungumzia suala hilo. Tanzania ina kikosi maalum kinachoshiriki kulinda amani nchini Sudan.

Chanzo:NIPASHE

Diamond, Prezzo kupimana ubavu usiku wa Matumaini

http://2.bp.blogspot.com/-tw2IRWQDrBo/UNM-97kIDUI/AAAAAAAAdRM/T1mHIisYZmw/s1600/392094_297471396942428_1613192750_n.jpg
Diamond

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3vx4abHtyX1-Nnz3uOuykRQ2t985fo7olqXsyYWCIr_uib_UtglZEdk13BxNUrSIjiwsfcFebiKI1LqIcEjAxZOv4uEt7pkNV45jiIHg0_-PMtO1b379OwMQv50Yya-jeECtnk3YsrI3c/s1600/Prezzo+(Kenya).jpg
Prezzo

MSANII nyota wa Bongofleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond, atakuwa na fursa ya kuthibitisha makali yake dhidi ya nyota wa kizazi kipya wa Kenya, Jackson Makini a.k.a CMB Prezzo wakati wawili hao watakapopanda katika jukwaa moja kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu.
Mratibu wa tamasha hilo Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, alisema mpambano huo unatarajiwa kutegua kitendawili cha nani mkali kati ya wasanii hao kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema Diamond ambaye ana tuzo ya Msanii Bora wa Kiume ya Kilimanjaro, ataonyeshana ubavu na mkali Prezzo ambaye ana mashabiki wengi nchini Kenya, hivyo mpambano unatarajiwa kuwa mkali.
Abby alisema Prezzo ambaye ni mshiriki wa Big Brother msimu uliopita, alimwambia kuwa anatarajia kuona umati mkubwa wa mashabiki wake ukimuunga mkono siku hiyo kwa kuwa ndiyo mara yake ya kwanza kufanya shoo katika uwanja huo unaobeba zaidi ya mashabiki 60,000.
Aliongeza pia kwamba kutakuwa na mpambano utakaohusisha Kenya na Tanzania kwa upande wa ngumi ambapo mabondia kutoka nchi hizo mbili watazichapa.
Mabondia Patrick Amonte atatunishiana msuli na Thomas Mashali wakati Shadrack Machanje yeye atazichapa na Francis Miyeyusho.
Ukiachana na ngumi, pia bendi za Msondo Ngoma, Jahazi Modern Taarab na Sikinde zitakuwapo siku hiyo.
TMK Halisi na Wanaume Family watawafundisha mashabiki wao staili mpya za uchezaji, alisema.
“Hii itakuwa vita kali sana kwa kuwa ukiangalia stejini Diamond atapambana na mkali kutoka Kenya, huku kwenye ngumi nako kupo hivyohivyo ambako ni Wakenya vs Watanzania, hivyo patakuwa hapatoshi Julai 7.
“Sehemu ya mapato kama kawaida tutapeleka kwenye mfuko wa elimu kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.”



Messi, baba yake matatani wakihutumiwa kukwepa kodi

http://www.channelstv.com/home/wp-content/uploads/2013/06/messi_father.jpg
Messi na baba yake

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Muargentina Lionel Messi na baba yake Jorge wanatuhumiwa na Mamlaka ya Kodi ya Hispania kukwepa kodi na kuikosesha serikali ya nchi hiyo mapato ya zaidi ya euro milioni nne (Sh. Bilioni 8.5).
Mwanasoka huyo bora wa mwaka wa Dunia na baba yake wanadaiwa kuficha sehemu ya mapato yao halisi ya miaka ya 2006, 2007, 2008 na 2009, kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka mjini Catalonia.  Msemaji wa Barca hakuwa tayari kuzungumzia tuhuma hizo
Messi, ambaye atafikisha miaka 26 mwezi huu, ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi duniani, akiwa na mshahara wa zaidi ya dola za Marekani milioni 20 kwa mwaka (Sh. bilioni 32), kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Mbali na mshahara mnono anaolipwa na Barca, Messi pia huingiza takriban dola za Marekani milioni 21 kwa mwaka (Sh. bilioni 33) kutokana na udhamini wa makampuni kadhaa yakiwamo ya Adidas, PepsiCo na P&G; na anakamata nafasi ya 10 katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaoongoza kwa kuingiza fedha nyingi duniani.

Miaka 13 ya Jide ni kesho Nyumbani Lounge