STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 13, 2013

Messi, baba yake matatani wakihutumiwa kukwepa kodi

http://www.channelstv.com/home/wp-content/uploads/2013/06/messi_father.jpg
Messi na baba yake

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Muargentina Lionel Messi na baba yake Jorge wanatuhumiwa na Mamlaka ya Kodi ya Hispania kukwepa kodi na kuikosesha serikali ya nchi hiyo mapato ya zaidi ya euro milioni nne (Sh. Bilioni 8.5).
Mwanasoka huyo bora wa mwaka wa Dunia na baba yake wanadaiwa kuficha sehemu ya mapato yao halisi ya miaka ya 2006, 2007, 2008 na 2009, kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka mjini Catalonia.  Msemaji wa Barca hakuwa tayari kuzungumzia tuhuma hizo
Messi, ambaye atafikisha miaka 26 mwezi huu, ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi duniani, akiwa na mshahara wa zaidi ya dola za Marekani milioni 20 kwa mwaka (Sh. bilioni 32), kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Mbali na mshahara mnono anaolipwa na Barca, Messi pia huingiza takriban dola za Marekani milioni 21 kwa mwaka (Sh. bilioni 33) kutokana na udhamini wa makampuni kadhaa yakiwamo ya Adidas, PepsiCo na P&G; na anakamata nafasi ya 10 katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaoongoza kwa kuingiza fedha nyingi duniani.

No comments:

Post a Comment