STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 13, 2013

Diamond, Prezzo kupimana ubavu usiku wa Matumaini

http://2.bp.blogspot.com/-tw2IRWQDrBo/UNM-97kIDUI/AAAAAAAAdRM/T1mHIisYZmw/s1600/392094_297471396942428_1613192750_n.jpg
Diamond

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3vx4abHtyX1-Nnz3uOuykRQ2t985fo7olqXsyYWCIr_uib_UtglZEdk13BxNUrSIjiwsfcFebiKI1LqIcEjAxZOv4uEt7pkNV45jiIHg0_-PMtO1b379OwMQv50Yya-jeECtnk3YsrI3c/s1600/Prezzo+(Kenya).jpg
Prezzo

MSANII nyota wa Bongofleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond, atakuwa na fursa ya kuthibitisha makali yake dhidi ya nyota wa kizazi kipya wa Kenya, Jackson Makini a.k.a CMB Prezzo wakati wawili hao watakapopanda katika jukwaa moja kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu.
Mratibu wa tamasha hilo Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, alisema mpambano huo unatarajiwa kutegua kitendawili cha nani mkali kati ya wasanii hao kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema Diamond ambaye ana tuzo ya Msanii Bora wa Kiume ya Kilimanjaro, ataonyeshana ubavu na mkali Prezzo ambaye ana mashabiki wengi nchini Kenya, hivyo mpambano unatarajiwa kuwa mkali.
Abby alisema Prezzo ambaye ni mshiriki wa Big Brother msimu uliopita, alimwambia kuwa anatarajia kuona umati mkubwa wa mashabiki wake ukimuunga mkono siku hiyo kwa kuwa ndiyo mara yake ya kwanza kufanya shoo katika uwanja huo unaobeba zaidi ya mashabiki 60,000.
Aliongeza pia kwamba kutakuwa na mpambano utakaohusisha Kenya na Tanzania kwa upande wa ngumi ambapo mabondia kutoka nchi hizo mbili watazichapa.
Mabondia Patrick Amonte atatunishiana msuli na Thomas Mashali wakati Shadrack Machanje yeye atazichapa na Francis Miyeyusho.
Ukiachana na ngumi, pia bendi za Msondo Ngoma, Jahazi Modern Taarab na Sikinde zitakuwapo siku hiyo.
TMK Halisi na Wanaume Family watawafundisha mashabiki wao staili mpya za uchezaji, alisema.
“Hii itakuwa vita kali sana kwa kuwa ukiangalia stejini Diamond atapambana na mkali kutoka Kenya, huku kwenye ngumi nako kupo hivyohivyo ambako ni Wakenya vs Watanzania, hivyo patakuwa hapatoshi Julai 7.
“Sehemu ya mapato kama kawaida tutapeleka kwenye mfuko wa elimu kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.”



No comments:

Post a Comment