STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, October 16, 2014

Algeria yafuzu Fainali za AFCON 2015 yaitungua Malawi 3-0

Algeria prove why they are the top ranked side in AfricaTIMU ya taifa ya Algeria imeweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza kufuzu katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco baada ya kupata ushindi murua wa mabao 3-0 dhidi ya Malawi katika mechi za kundi D.
Vijana wa kocha Christian Gourcuff wameweka rekodi ya kushinda mechi zake zote mpaka sasa kukiwa kumesaliwa mechi mbili kabla ya mechi za makundi kumalizika.
Mabao ya washindi hao waliong'olewa kwenye raundi ya pili ya Fainali za Kombe la Dunia za 2014 na waliokuja kuwa Mabingwa wapya, Ujerumani yaliwekwa kimiani naYasine Brahimi  dakika ya pili, Riyad Mahrez dk ya 45 na Islam Slimani Dk ya 55.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo kundi B lilishuhudiwa Ethiopia ikiwa ugenini mjini Bamako iliicharaza wenyeji Mali kwa mabao 3-2 na kujiweka pazuri kabla ya mechi mbili za mwisho dhidi ya Algeria na Malawi.
Bakary Sako alianza kufungua milango ya pambano hilo kwa kuwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 31 kabla ya wageni kurejesha na kuongeza la pili kupitia kwa wachezaji wao Oumed Oukri na Getaneh Kebede na Mali kuchomoa na kufanya matokeo kuwa 2-2 kwa bao la Mustapha Yatabare dakika dakika ya 69.

Bao la ushindi la Ethiopia lilifungwa na Abebaw Butako Bune, huku Angola ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lesotho katika mechi ya Kundi C.
Bastos alianza kuwaandikia wenyeji bao dakika ya pili kabla ya Ary Papel kuongeza la pili dakika ya 33 na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa 2-0 na kwenye kipindi cha pili Tsoanelo Koetle alijifunga katika dakika ya 47 na Love akapigilia msumari wa mwisho kw akuifungia Palancas Negras bao dakika ya 57.
nazo timu za Burkina Faso na Gabon zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 Jonathan Pitroipa akiifungia Burkinabe na wageni kuchomoa kupitia kwa Malick Evouna dakika ya 76.
Cape Verde waliendelea kuweka ugumu katika Kundi F baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Msumbiji kwa bao la Heldon katika dakika ya 75 na kuifanya wenyeji kufikisha pointi 9, huku Msumbiji wakisalia kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 5 sawa na Zambia walioshinda nyumbani mabao 3-0 dhidi ya Niger.
Nayo timu ya Tunisia ilifuata nyayo za majirani zao Misri walioishinda Botswana kwa mabao 2-0 nyumbani baada ya kuilaza Senegal bao 1-0 bao lilifungwa 'jioni' na Ferjani Sassi na kuifanya Tunisia kuongoza msimamo wa kundi hilo wakiwa na pointi 10 wakifuatiwa na Senegal wanaokamata nafasi ya pili wamiwa na pointi saba wakiitangulia Misri wenye pointi 6 wakiwa nafasi ya tatu.

Breaking Newz! Nigeria yamtimua Stephen Keshi, Amodu amrithi

http://ynaija.com/wp-content/uploads/2013/10/Nigerias-coach-Stephen-Ke-011.jpg
Stephen Keshi akiwa amebebwa alipotwaa ubingwa wa Afrika
https://thetbjoshuafanclub.files.wordpress.com/2009/12/amodu1.jpg
Shaibu Amodu anayemrithi Keshi kartika Super Eagles

SHIRIKISHO la Soka la Nigeria, NFF, kimetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha Mkuu wa Super Eagles, Stephen Keshi ikiwa ni saa chache tangu aiongoze timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Sudan katika mechi ya kuwania Fainali za Kombe la Afrika za 2015.
Kocha za zamani wa timu hiyo Shaibu Amodu ndiye aliyepewa mikoba ya kuuiongoza Super Eagles katika mechi zilizosalia za kundi lake.
Keshi, nyota wa zamani wa timu hiyo amekuwa kocha wa Nigeria tangu mwaka 2011 na alifanikiwa  kuipeleka Super Eagles kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kuishia nao raundi ya pili na inaelezwa tangu fainali hizo hakuwa na mkataba wowote licha ya kuendelea kuinoa timu hiyo aliyoipa ubingwa wa Afrika fainali za mwaka jana zilizofanyika nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa NFF, maamuzi ya kutimuliwa kwa Keshi yamekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo kukutana jana.
"Kwa manufaa ya soka la Nigeria na kiu kubwa ya kushiriki fainali za mwaka 2015 kamati imeamua kuachana na Keshi na benchi lake lote la ufundi," taarifa ya NFF ilisomeka hivyo.
Badala ya keshi NFF imemtaja Amodu aliyewahi kuinoa timu hiyo katika vipindi vinne tofauti mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2008-2010.
Vipindi vingine ambayo Shaibu Amodu aliwahi kuiongoza timu hiyo ni mwaka 1994-95, 1998-99, 2001-2002, Mei Mwaka jana alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Soka nchini humo kabla ya kupata kazi kama hiyo katika klabu na kutema nafasi yake hadi alipoitwa leo na NFF kuwa Kocha Mkuu kwa mara ya tano.

Maafa makubwa Misri! Bomu lalipuliwa Mahakamani jiji Cairo

An injured man arrives at the Helal hosp 
BOMU lililotengenezwa kienyeji huko Cairo, Misri limelipuka karibu na mahakama kuu siku ya Jumanne tarehe 14 mwaka huu na kujeruhi watu 12 ambapo gari na maduka yaliliyokuwa karibu ya eneo hilo la tukio yameharibika.
Haikufahamika vizuri kama lengo lilikuwa ni la kumuua mtu mmoja au kufanya tu uharibifu kwa sababu hii ni mara ya pili tukio kama hili limetokea huko Cairo chini ya mwezi mmoja.
Ripoti zinasema bomu ambalo lililipuka mwezi uliopita karibu na wizara ya mambo ya nje lililoua polisi watatu, lilisababisha uhalifu mkubwa ambao haukutokea kwa muda mrefu mjini Cairo.
Shambulizi hilo la bomu lilianzishwa na kundi la Jeshi la Kiislamu liitwalo Ajnad Misr ambapo inasemekana ongezeko la mashambulizi ya majeshi ya Kiislamu yamezidi kwenye nchi hiyo toka mkuu wa jeshi aitwae Abdel Fattah al-Sisi ampindue Rais Mohamed Morsi mwaka jana baada ya wananchi kupinga utawala wake.
Baada ya kumpindua Rais Mohamed Morsi mkuu huyo wa jeshi Abdel Fattah alivunja udugu wa Kiislamu uliokuwa chini ya Mohamed Morsi ambapo serikali ililitangaza kuwa ni kundi la kigaidi.

Kocha Hispania aanza kuaga, kutema timu baada ya Euro Cup

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/10/01/1412176952043_wps_10_Spain_s_head_coach_Vicent.jpg
Kocha Del Bosque
KOCHA wa Hispania, Vicente Del Bosque amesema ataachia ngazi ya kukinoa kikosi hicho cha timu ya taifa baada ya michuano ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa.
Del Bosque (63), ameshuhudiwa akipata mafanikio ya dhahabu kwa umri wake huo katika soka la Hispania, baada ya kushinda Kombe la Dunia  2010 na michuano ya Ulaya (Euro 2012) katika historia ya jina lake kwenye timu ya taifa.
Hata hivyo, Hispania ilianza kudorora katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Slovakia ilichokipata Alhamisi ni cha kwanza katika mechi 36 za kuwania kufuzu kuanzia 2006 -- kimemfanya Del Bosque kuanza kukosolewa kwa mara ya kwanza tangu alipotwaa mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka 2008 kutoka kwa Aragones.
Baada ya kutolewa kwenye Kombe la Dunia, kocha huyo mkuu wa Hispania, Del Bosque alionekana kuzama zaidi katika vipaji vya timu ya taifa ya makinda kwa kuviandaa kwa ajili ya Euro 2016. Tayari Del Bosque ameiongoza Hispania katika michuano mikubwa ya kimatifa mitatu na kushinda miwili tangu alipoanza kuinoa 2008.
"Nadhani Euro 2016 itakuwa michuano yangu ya mwisho kama kocha mkuu wa Hispania," aliiambia  Redio Nacional de Espana.
"Tutaona nini kitatokea wakati tutakapokwenda Ufaransa. Kinadharia, hii ni michuano yangu ya mwisho."
Del Bosque si mtu pekee ambaye yupo katika presha kubwa katika kikosi hicho cha 'La Roja', pia kipa wa Real Madrid, Iker Casillas amepoteza nafasi yake ambayo imetwaliwa na mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea wakati  walipoibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg Jumapili.
Casillas (33), amekuwa akikosolewa na vyombo vya habari vya Hispania kutokana na kiwango chake katika Kombe la Dunia na dhidi ya Slovakia, huku pia uwezo wake ndani ya klabu ukizua mjadala, jambo linalomfanya kipa wa kimataifa wa Costa Rica Keylor Navas kuanza kuivizia nafasi yake.

Paul Scholes ampigia 'salute' Jack Welshere

http://i1.mirror.co.uk/incoming/article2168562.ece/alternates/s2197/England-v-Scotland-International-Friendly.jpg
Jack Welshere
KIUNGO nyota wa zamani wa England aliyewahi kutamba na klabu ya Manchester United, Paul Scholes anaamini kwamba Jack Wilshere ameongezeka ubora na sasa ndiye mchezaji bora zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya England.
Welshere, 22, ambaye alicheza kwa dakiia zote 180 za mechi mbili za timu ya taifa ya England za kuwania kufuzu kwa fainali za Euro 2016 ambazo walishinda dhidi ya San Marino na Estonia, alipata kukosolewa na gwiji huyo wa Manchester United kwa kushindwa kuongezeka ubora tangu alipoingia katima kikosi cha kwanza cha Arsenal.
Lakini Scholes sasa amemsifu Wilshere, ambaye alipewa jukumu la kucheza katikati ya kiungo na kocha Roy Hodgson, na gwiji huyo wa Man U mwenye umri wa miaka 39 amefurahishwa na pasi zilizokuwa zikitolewa na kiungo huyo.
“Nadhani Jack Wilshere alikuwa na mechi mbili nzuri sana za England wiki iliyopita,” Scholes aliandika kwenye gazeti la Independent. “Naweza kwenda hatua moja mbele na kusema kwamba, kwa sasa, Wilshere ndiye mchezaji bora wa England.
“Amebadilika na ameongeza kitu katika uchezaji wake. Alikuwa ni mtu wa pasi fupi tu, lakini sasa anaweza kupiga pasi ndefu pia.”

Hivi ndivyo Suzuki Sauti ya Malaika alivyozikwa jana jijini Dar

https://fbcdn-sphotos-h-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xpf1/v/t34.0-12/10735860_387830028030788_699106094_n.jpg?oh=4a4a71a5e704c6de8d13b86213f578a6&oe=544077E5&__gda__=1413518840_3735b6aa646908122422cde63a7ff273
Waombolezaji wakifukia kaburi ya marehemu Suzuki wakati wa mazishi yake jana kwenye makaburi ya Magomeni Kagera
Mwili wa marehemu Suzuki ulipokuwa ukihifadhiwa jana
Mwili wa Suzuki ukihifadhiwa katika makaburi ya Kagera

Waombolezaji wakiwa makini kufuatilia mazishi ya Suzuki

Baadhi ya woambolezaji walioshiriki mazishi ya Suzuki
http://2.bp.blogspot.com/-kIX-KBZtV84/TyWuKERucVI/AAAAAAAAPSo/YM6VjTOyW4k/s400/P1211580.jpg
Suzuki Sauti ya Marehemu enzi za uhai wake
MWILI wa mwanamuziki nyota wa zamani wa bendi za Tabora Jazz, Mikumi Sound, Levent Musica na Extra Bongo, Suleiman Ramadhan 'Suzuki' au Sauti ya Malaika hatimaye umepumzishw akatika mazishi yaliyofanyika jana jioni kwenye makaburi yaliyopo eneo la Kagera.
Mwili huo ulizikwa saa 10:30 mara baada ya kuswaliwa kwenye Msikiti wa Rahman Kagera Mikoroshini na kusindikizwa na wanamuziki wenzake wachache na waumini wengine ambao wlaifurika kumhifadhi muimbaji huyo aliyefariki usiku wa juzi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.
MICHARAZO iliwashuhudia wanamuziki wachache waliojitokeza kumsindikiza mwenzao huku baadhi ya waliokuwa mabosi wake wa zamani wakiwa wameingia mitini.
Miongoni mwa wanamuziki walioshiriki mazishi hayo mwanzo mwishoni ni Ramadhan Mhoza 'Pentagone', Athanas Montanabe, Adam Mbombole, Frank Kaba 'Kaba Tano' Redock Sura ya Mauzo, Hosea Mgohachi, dansa wa zamani wa Chino Loketo, Bob Kissa na wengine.
Aidha kulikuwa na wasanii wengine mbalimbali wa muziki ambao walishiriki kumsindikiza mwenzao, huku majina makubwa ya wasanii ambao waliwahi kufanya kazi na marehemu Suzuki wakiwa wameingia mitini.

TFF yapangua kiduchu ratiba Ligi Daraja la Kwanza (FDL)

http://2.bp.blogspot.com/-fabjlG96V7c/UoMFV9FO0KI/AAAAAAAAbbk/1avFfd1EY4Y/s640/Wambura1_2_339a2.jpg
MECHI nne za Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho ili kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.


Timu za African Lyon na Kimondo ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


Nayo mechi ya Polisi Dar es Salaam na Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, sasa itachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.


Mechi ya Friends Rangers na Ashanti United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani Pwani, Oktoba 26 mwaka huu, sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28 mwaka huu.

Pia mechi ya Lipuli na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Uchaguzi mdogo Bodi ya Ligi Nov 15

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/DSC03338.jpgMKUTANO  Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utafanyika Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo moja ya ajenda ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi moja ya uongozi kwenye bodi hiyo.


Nafasi hiyo ya ujumbe kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB iliyokuwa ikishikiliwa na Kazimoto Muzo imebaki wazi baada ya klabu yake ya Pamba ya Mwanza kushuka daraja kutoka la Kwanza hadi la Pili.

Hivyo, wagombea wa nafasi hiyo ni kutoka kwenye klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL). 
Klabu hizo zina nafasi mbili kwenye Kamati ya Uendeshaji ya TPLB ambapo nyingine inashikiliwa na Omari Mwindadi wa klabu ya Mwadui ya Shinyanga.

Nigeria yazinduka, Ivory Coast hoi, Cameroon wanusa AFCON 2015

http://images.performgroup.com/di/library/Goal_Nigeria/e0/cf/nigeria-vs-sudan-abuja_1ro9umbg2xq9b1qgpib297xiqm.jpg?t=349299433&w=940
Nigeria walipoisulubu Sudan mjini Abuja
http://www.goal-news.com/wp-content/uploads/2014/10/Asamoah-Gyan-Ghana-e1413339163729.jpg
Ghana wakishangilia moja ya mabao yao
http://nilsenreport.ca/wp-content/uploads/2014/06/Ivory-Coast-World-Cup-tea-010.jpg
Ivory Coast iliyokufa kwa DR Congo
http://www.goolfm.net/wp-content/uploads/2014/10/s64.jpg
Cameroon walionusa fainali za AFCON 2015

MABINGWA watetezi wa Kombe la Afrika, Nigeria imelipiza kisasi kwa Sudan kwa kuilaza mabao 3-1, wakati Ivory Coast ikifumuliwa mabao 4-3, huku Uganda ikigawa pointi tena kwa Togo kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye mechi za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Nigeria mabyo ilitoka kupigwa mabao 2-0 na Sudan kwenye mechi iliyochezwa wikiendi iliyopita, ikiwa mjini Abuja waliwakomalia wapinzani wao na kupata ushindi huo muhimu na kufufua matumaini yao ya kwenda kutetea taji hilo Morocco kwa mabao ya Ahmed Mussa aliyefunga mawili dakika ya 48 na 90 na jingine la Aaron Olanare.
Bao la kufutia machozi la Sudan lilifungwa na Mohammed Salah Ibrahim dakika ya 56.
Katika mechi nyingine za mashindano hao Ghana ilipata ushindi mnono nyumbani dhidi ya Guinea waliotoka nao sare siku chache zilizopita.
Mabao ya washindi yalifungwa na Asamoh Gyan aliyefunga dakika ya 16 kabla ya Ander Ayew 'Pele' kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 58 na Agyemang-Badu kufunga la tatu dakika za jioni, huku wapinzani wao wakipata bao kupitia kwa Mohammed Yattara.
Uganda ikiwa mjini Lome Togo, ilishinda kulip[a kisasi kwa wenyeji wao kwa kukubali tena kicvhapo cha bao 1-0 na kuzidi kuwaweka pabaya katika mbio za kwenda Morocco.
Bao lililoiangamiza Uganda The Cranes lilifungwa na Serge Akakpo dakika ya 70 na kuifanya Togo kupanda hadi nafasi ya pili katika kundi hilo la E ikiwa na pointi 6, ikishusha Uganda inayosaliwa na pointi zake nne.
Katika mechi za kundi F, Zambia iliendeleza ubabe kwa kuinyuka Niger mabao 3-0 katika pambano lililiochezwa mjini Lusaka kupitia mabao ya Rainford Kalaba, Emmanuel Mayuka na Kenned Mweene aliyefungwa kwa penatui.
Nayo Misri ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana wakirejea ushindi kama huo walioupata katika mechi iliyopita siku chache zilizopita wakiwa ugenini.
Mabao ya washindi yalifungwa na Amr Gamal na Mohammed Salah, huku Cameroon ikizinduka na kuinyuka Sierra Leone kwa mabao 2-0 kupitia mabao ya mapema ya Leonard Kweuke na Stephane Mbia na kuifanya tuimu hiyo inuse fainali hizo za mwakani kwa kufikisha pointi 10 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo walikung'utwa mabao 4-3 na DR Congo katika mechi iliyosisimua.
Magoli ya DR Congo yalifungwa na Neeskens Keban dk ya 21, Junior Kabananga dk ya 35 na Jeremy Bokila dakika ya 36 na 89 huku magoli ya wageni waliocheza pungufu baada ya kumpoteza Yannick Kessie aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47, yalipachikwa wavuni na Mwanasoka Bora wa Afrika Yaya Toure na Solomon Kalou aliyefunga mawili.