BOMU lililotengenezwa kienyeji huko Cairo, Misri limelipuka karibu na mahakama kuu siku ya Jumanne tarehe 14 mwaka huu na kujeruhi watu 12 ambapo gari na maduka yaliliyokuwa karibu ya eneo hilo la tukio yameharibika.
Haikufahamika vizuri kama lengo lilikuwa ni la kumuua mtu mmoja au
kufanya tu uharibifu kwa sababu hii ni mara ya pili tukio kama hili
limetokea huko Cairo chini ya mwezi mmoja.
Ripoti zinasema bomu ambalo lililipuka mwezi uliopita karibu na
wizara ya mambo ya nje lililoua polisi watatu, lilisababisha uhalifu
mkubwa ambao haukutokea kwa muda mrefu mjini Cairo.
Shambulizi hilo la bomu lilianzishwa na kundi la Jeshi la Kiislamu
liitwalo Ajnad Misr ambapo inasemekana ongezeko la mashambulizi ya
majeshi ya Kiislamu yamezidi kwenye nchi hiyo toka mkuu wa jeshi aitwae
Abdel Fattah al-Sisi ampindue Rais Mohamed Morsi mwaka jana baada ya
wananchi kupinga utawala wake.
Baada ya kumpindua Rais Mohamed Morsi mkuu huyo wa jeshi Abdel Fattah
alivunja udugu wa Kiislamu uliokuwa chini ya Mohamed Morsi ambapo
serikali ililitangaza kuwa ni kundi la kigaidi.
No comments:
Post a Comment