Kocha Del Bosque |
Del Bosque (63), ameshuhudiwa akipata mafanikio ya dhahabu kwa umri wake huo katika soka la Hispania, baada ya kushinda Kombe la Dunia 2010 na michuano ya Ulaya (Euro 2012) katika historia ya jina lake kwenye timu ya taifa.
Hata hivyo, Hispania ilianza kudorora katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Slovakia ilichokipata Alhamisi ni cha kwanza katika mechi 36 za kuwania kufuzu kuanzia 2006 -- kimemfanya Del Bosque kuanza kukosolewa kwa mara ya kwanza tangu alipotwaa mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka 2008 kutoka kwa Aragones.
Baada ya kutolewa kwenye Kombe la Dunia, kocha huyo mkuu wa Hispania, Del Bosque alionekana kuzama zaidi katika vipaji vya timu ya taifa ya makinda kwa kuviandaa kwa ajili ya Euro 2016. Tayari Del Bosque ameiongoza Hispania katika michuano mikubwa ya kimatifa mitatu na kushinda miwili tangu alipoanza kuinoa 2008.
"Nadhani Euro 2016 itakuwa michuano yangu ya mwisho kama kocha mkuu wa Hispania," aliiambia Redio Nacional de Espana.
"Tutaona nini kitatokea wakati tutakapokwenda Ufaransa. Kinadharia, hii ni michuano yangu ya mwisho."
Del Bosque si mtu pekee ambaye yupo katika presha kubwa katika kikosi hicho cha 'La Roja', pia kipa wa Real Madrid, Iker Casillas amepoteza nafasi yake ambayo imetwaliwa na mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea wakati walipoibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg Jumapili.
Casillas (33), amekuwa akikosolewa na vyombo vya habari vya Hispania kutokana na kiwango chake katika Kombe la Dunia na dhidi ya Slovakia, huku pia uwezo wake ndani ya klabu ukizua mjadala, jambo linalomfanya kipa wa kimataifa wa Costa Rica Keylor Navas kuanza kuivizia nafasi yake.
No comments:
Post a Comment