STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, October 16, 2014

Nigeria yazinduka, Ivory Coast hoi, Cameroon wanusa AFCON 2015

http://images.performgroup.com/di/library/Goal_Nigeria/e0/cf/nigeria-vs-sudan-abuja_1ro9umbg2xq9b1qgpib297xiqm.jpg?t=349299433&w=940
Nigeria walipoisulubu Sudan mjini Abuja
http://www.goal-news.com/wp-content/uploads/2014/10/Asamoah-Gyan-Ghana-e1413339163729.jpg
Ghana wakishangilia moja ya mabao yao
http://nilsenreport.ca/wp-content/uploads/2014/06/Ivory-Coast-World-Cup-tea-010.jpg
Ivory Coast iliyokufa kwa DR Congo
http://www.goolfm.net/wp-content/uploads/2014/10/s64.jpg
Cameroon walionusa fainali za AFCON 2015

MABINGWA watetezi wa Kombe la Afrika, Nigeria imelipiza kisasi kwa Sudan kwa kuilaza mabao 3-1, wakati Ivory Coast ikifumuliwa mabao 4-3, huku Uganda ikigawa pointi tena kwa Togo kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye mechi za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Nigeria mabyo ilitoka kupigwa mabao 2-0 na Sudan kwenye mechi iliyochezwa wikiendi iliyopita, ikiwa mjini Abuja waliwakomalia wapinzani wao na kupata ushindi huo muhimu na kufufua matumaini yao ya kwenda kutetea taji hilo Morocco kwa mabao ya Ahmed Mussa aliyefunga mawili dakika ya 48 na 90 na jingine la Aaron Olanare.
Bao la kufutia machozi la Sudan lilifungwa na Mohammed Salah Ibrahim dakika ya 56.
Katika mechi nyingine za mashindano hao Ghana ilipata ushindi mnono nyumbani dhidi ya Guinea waliotoka nao sare siku chache zilizopita.
Mabao ya washindi yalifungwa na Asamoh Gyan aliyefunga dakika ya 16 kabla ya Ander Ayew 'Pele' kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 58 na Agyemang-Badu kufunga la tatu dakika za jioni, huku wapinzani wao wakipata bao kupitia kwa Mohammed Yattara.
Uganda ikiwa mjini Lome Togo, ilishinda kulip[a kisasi kwa wenyeji wao kwa kukubali tena kicvhapo cha bao 1-0 na kuzidi kuwaweka pabaya katika mbio za kwenda Morocco.
Bao lililoiangamiza Uganda The Cranes lilifungwa na Serge Akakpo dakika ya 70 na kuifanya Togo kupanda hadi nafasi ya pili katika kundi hilo la E ikiwa na pointi 6, ikishusha Uganda inayosaliwa na pointi zake nne.
Katika mechi za kundi F, Zambia iliendeleza ubabe kwa kuinyuka Niger mabao 3-0 katika pambano lililiochezwa mjini Lusaka kupitia mabao ya Rainford Kalaba, Emmanuel Mayuka na Kenned Mweene aliyefungwa kwa penatui.
Nayo Misri ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana wakirejea ushindi kama huo walioupata katika mechi iliyopita siku chache zilizopita wakiwa ugenini.
Mabao ya washindi yalifungwa na Amr Gamal na Mohammed Salah, huku Cameroon ikizinduka na kuinyuka Sierra Leone kwa mabao 2-0 kupitia mabao ya mapema ya Leonard Kweuke na Stephane Mbia na kuifanya tuimu hiyo inuse fainali hizo za mwakani kwa kufikisha pointi 10 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo walikung'utwa mabao 4-3 na DR Congo katika mechi iliyosisimua.
Magoli ya DR Congo yalifungwa na Neeskens Keban dk ya 21, Junior Kabananga dk ya 35 na Jeremy Bokila dakika ya 36 na 89 huku magoli ya wageni waliocheza pungufu baada ya kumpoteza Yannick Kessie aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47, yalipachikwa wavuni na Mwanasoka Bora wa Afrika Yaya Toure na Solomon Kalou aliyefunga mawili.

No comments:

Post a Comment