STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, October 16, 2014

Paul Scholes ampigia 'salute' Jack Welshere

http://i1.mirror.co.uk/incoming/article2168562.ece/alternates/s2197/England-v-Scotland-International-Friendly.jpg
Jack Welshere
KIUNGO nyota wa zamani wa England aliyewahi kutamba na klabu ya Manchester United, Paul Scholes anaamini kwamba Jack Wilshere ameongezeka ubora na sasa ndiye mchezaji bora zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya England.
Welshere, 22, ambaye alicheza kwa dakiia zote 180 za mechi mbili za timu ya taifa ya England za kuwania kufuzu kwa fainali za Euro 2016 ambazo walishinda dhidi ya San Marino na Estonia, alipata kukosolewa na gwiji huyo wa Manchester United kwa kushindwa kuongezeka ubora tangu alipoingia katima kikosi cha kwanza cha Arsenal.
Lakini Scholes sasa amemsifu Wilshere, ambaye alipewa jukumu la kucheza katikati ya kiungo na kocha Roy Hodgson, na gwiji huyo wa Man U mwenye umri wa miaka 39 amefurahishwa na pasi zilizokuwa zikitolewa na kiungo huyo.
“Nadhani Jack Wilshere alikuwa na mechi mbili nzuri sana za England wiki iliyopita,” Scholes aliandika kwenye gazeti la Independent. “Naweza kwenda hatua moja mbele na kusema kwamba, kwa sasa, Wilshere ndiye mchezaji bora wa England.
“Amebadilika na ameongeza kitu katika uchezaji wake. Alikuwa ni mtu wa pasi fupi tu, lakini sasa anaweza kupiga pasi ndefu pia.”

No comments:

Post a Comment