|
Waombolezaji wakifukia kaburi ya marehemu Suzuki wakati wa mazishi yake jana kwenye makaburi ya Magomeni Kagera |
|
Mwili wa marehemu Suzuki ulipokuwa ukihifadhiwa jana |
|
Mwili wa Suzuki ukihifadhiwa katika makaburi ya Kagera |
|
Waombolezaji wakiwa makini kufuatilia mazishi ya Suzuki |
|
Baadhi ya woambolezaji walioshiriki mazishi ya Suzuki |
|
Suzuki Sauti ya Marehemu enzi za uhai wake |
MWILI wa mwanamuziki nyota wa zamani wa bendi za Tabora Jazz, Mikumi Sound, Levent Musica na Extra Bongo, Suleiman Ramadhan 'Suzuki' au Sauti ya Malaika hatimaye umepumzishw akatika mazishi yaliyofanyika jana jioni kwenye makaburi yaliyopo eneo la Kagera.
Mwili huo ulizikwa saa 10:30 mara baada ya kuswaliwa kwenye Msikiti wa Rahman Kagera Mikoroshini na kusindikizwa na wanamuziki wenzake wachache na waumini wengine ambao wlaifurika kumhifadhi muimbaji huyo aliyefariki usiku wa juzi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.
MICHARAZO iliwashuhudia wanamuziki wachache waliojitokeza kumsindikiza mwenzao huku baadhi ya waliokuwa mabosi wake wa zamani wakiwa wameingia mitini.
Miongoni mwa wanamuziki walioshiriki mazishi hayo mwanzo mwishoni ni Ramadhan Mhoza 'Pentagone', Athanas Montanabe, Adam Mbombole, Frank Kaba 'Kaba Tano' Redock Sura ya Mauzo, Hosea Mgohachi, dansa wa zamani wa Chino Loketo, Bob Kissa na wengine.
Aidha kulikuwa na wasanii wengine mbalimbali wa muziki ambao walishiriki kumsindikiza mwenzao, huku majina makubwa ya wasanii ambao waliwahi kufanya kazi na marehemu Suzuki wakiwa wameingia mitini.
No comments:
Post a Comment