STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 9, 2013

Aisha Bui akana kukamatwa na 'unga' Brazili, adai yu salama Afrika Kusini


MWANADADA anayetamba kwenye filamu nchini, Aisha Bui amekanusha taarifa kwamba amekamatwa na dawa za kulevya na kufungwa kifungo cha miaka mitano nchini Brazil.

Akizungumza na MICHARAZO kutoka Afrika Kusini, Aisha Bui alisema ameshtushwa na taarifa hizo za kunaswa na 'bwimbwi' Brazili, ilihali yeye yupo Afrika Kusini salama wa salimini.
Aisha alisema angependa kuwafahamisha watanzania kwamba yu salama na wazichukulie taarifa hizo kama uzushi kwa sababu hajawahi na wala hajishughulishi na biashara hiyo ya 'unga'.
Pia mwanadada huyo alitupia ujumbe katika 'wall' yake Facebook akisisitiza suala hilo kwa kuandika;
Dear Friends, Fans n Family Naskia kuna habari flani mbaya zimetolewa na baadhi ya vyombo vya habari, napenda kuwajulisha wote kua hiyo si kweli Mimi ndio kweli niko safari lkn niko salama salmin Hakuna kitu Kama Hicho n namuomba mungu aniepushe na mambo hayo. Niko poa Kabisa n nawapenda wote.
Alipoulizwa kama kuna hatua zozote atakazochukua kwa kuzushiwa tuhuma hizo, Aisha aliyewahi kung'ara katika filamu mbalimbali, alisema hana mpango wa kufanya lolote kwa sababu hataki kugombana na vyombo vya habari, inagwa hakupendezwa na kilichoripotiwa ambacho alidai alikisoma mapema leo.
"Nawapotezea tu sina mda wa kugombana na vyombo vya habari," alisema Aisha Bui, mwanadada aliyewahi kuripotiwa kuolewa na aliyekuwa mfanyabiashara na mdau mkubwa wa muziki nchini, Marehemu Mohammed Mpakanjia.

MSAIDIE MWANAHABARI HUYU MUNGU ATAKULIPA INSHALLAH


 Zuberi Mussa  katika mwonekano wa picha tofauti 
tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.

Zuberi Mussa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Dotto Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya (kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo na Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira, walipokwenda kumjulia hali kijjiini kwao.

Na Dotto Mwaibale, Tanga
Zuberi Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali.
Kikubwa kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa ambao bado haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili wakati wa kuongea naye hautaelewana naye kutokana na matamushi yake ambayo hayafahamiki yanayoonesha  kama mtu aliyechanganyikiwa.
Kutokana na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika matibabu hasa Hospitalini, Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake kwa waganga wa jadi.
Wakati Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani Korogwe mkoani Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema Amir kwa kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es Salaam, hawezi kufanya chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika inaumiza na kusikitisha.
Ndugu wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni tulionao wa kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika kipindi kigumu.
Binafsi nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita nilishitushwa na hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.
Zuberi alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali ambayo si ya kawaida zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea naye hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi pamoja na mke wake kipenzi  Rehema Amir anaweza kuwasiliana na Dotto Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na kaka yake.
Ndugu wanahabari wenzangu  na mtu mmoja mmoja, Taasisi yoyote, shirika lolote, Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya, Wafanyabiashara, Makampuni mbalimbali na vyama vya michezo  hima tujitoe kimasomaso kumsaidia mpiga naji mwenzetu Zuberi Mussa na mke wake waondoke katika matibabu ya jadi wanayopata badala yake wapelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya zao kwani kutoa ni moyo na si utajiri.