Zuberi Mussa katika mwonekano wa picha tofauti
tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.
Zuberi Mussa (katikati), akiwa katika
picha ya pamoja na Mwandishi Dotto Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya
(kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo na Mashaka Mhando wa Gazeti la
Majira, walipokwenda kumjulia hali kijjiini kwao.
Na Dotto Mwaibale, Tanga
Zuberi Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo
mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni
mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali.
Kikubwa kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa
ambao bado haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa
ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili wakati wa kuongea
naye hautaelewana naye kutokana na matamushi yake ambayo hayafahamiki yanayoonesha
kama mtu aliyechanganyikiwa.
Kutokana na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika
matibabu hasa Hospitalini, Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake
kwa waganga wa jadi.
Wakati Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani
Korogwe mkoani Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema Amir kwa
kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi
ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es Salaam, hawezi kufanya
chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika inaumiza na kusikitisha.
Ndugu wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni
tulionao wa kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika
kipindi kigumu.
Binafsi nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita
nilishitushwa na hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza
alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.
Zuberi alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali
ambayo si ya kawaida zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea
naye hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi pamoja
na mke wake kipenzi Rehema Amir anaweza
kuwasiliana na Dotto Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na
kaka yake.
No comments:
Post a Comment