STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 21, 2013

Makundi ya Kagame Cup 2013 yapangwa

Wachezaji wa Yanga wakishangilia katika baadhi ya mechi zao za mwaka jana za Kagame ilipocheza Dar

 MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga ya Tanzania imepangwa kundi l;a C pamoja na timu za Express ya Uganda, Vital'O ya Burundi na As Port ya Djibout, huku watani zao Simba wakiwekwa kundi A na El Merreikh ya Sudan na APR ya Rwanda.

Mbali na APR na Merreikh, kundi hilo A lina timu ya Elman ya Somalia, wakati kundi B l;ina timu za El Hilal ya Sudan, Ahli Shandi ya Sudan, Al Nasir Juba ya Sudan Kusini, Tusker Kenya na Super Falcon ya Zanzibar.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao na kumalizika mwanzoni mwa Julai, ambapo jumla ya timu 13 zitachuana katika kinyang'anyiro hicho.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:
Kundi A: El Merreikh (Sudan), Simba (Tanzania), Elman (Somalia) na APR (Rwanda).
Kundi B: El Hilal (Sudan), Ahli Shandi (Sudan), Al Nasri Juba (S.Sudan), Tusker (Kenya) na Super Falcon (Zanzibar)
Kunci C: Yanga (Tanzania), Express FC (Uganda), Vitalo (Burundi) na AS Port (Djibouti).

MKALI WA RHYMES  PROF. JAY AAMUA KUMFUATA SUGU CHADEMA

 Wanachama wapya wa Chadema, Joseph Haule maarufu Professa Jay (katikati)  na mwenzake Levison Kasulwa maarufu Kwa Mapacha, wakifurahia mara baada ya kupokea kadi zao za wanachama ikiwa ni kujiunga na Chama hicho mjini Dodoma huku wakionyesha alama yan chama hicho . Hafla hiyo iliyofanyika mjini Dodoma jana ilihudhuriwa na wabunge kadha wa CHADEMA.Kushoto ni Mbunge wa Mbeya  Mjini JosephMbiliny leo

Prof Jay akiionyesha kadi aliyokabidhiwa kwa kujiunga na CHADEMA akiwa na Wabunge wa chama hicho, Josepj Mbilinyi 'Sugu' na John Mnyika.

KICHANGA CHA MIAKA MIWILI CHAFANYIWA UKATILI WA KUTISHA

Mtoto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba  yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha


Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu 

Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana

Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza


Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

Mama wa mlezi wa Joshua akiingia numbani kwake na kutushangaa tumekuja fuatanini kwake

Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo

Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo

Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua

Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema  yeye huwa analala na joshua chumbani kwake 

Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo

Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni



Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo




Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo



Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika  mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
 Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora  pamoja na huduma nyingine.
.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye  Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
 Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
  
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa  wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya  Inyala Kata ya Iyunga  jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo  wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.
Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo


Picha na Mbeya yetu 

Aggrey Morris azikatisha tamaa zinazomwania adai ang'oki Azam


Aggrey Morris
BEKI mahiri wa Azam anayeichezea pia timu ya taifa (Taifa Stars), Aggrey Morris, amezikata maini klabu zinazodaiwa kumnyemelea ili zimsajili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kusema wazi kuwa, haendi kokote zaidi ya kubaki Azam.
Aidha beki huyo kutoka Zanzibar, alikiri kwamba ligi iliyomalizika wikiendi ilikuwa ngumu na kudai kufurahishwa na namna Azam ilivyozipeleka puta Simba na Yanga kiasi cha kuonekana kama ingetwaa ubingwa msimu huu kabla ya kuteleza.
Akizungumza na MICHARAZO Morris alisema pamoja na kutajwa kuwindwa na klabu kadhaa nchini ili kumsajili, ukweli ni kwamba klabu hizo zinajisumbua bure kwa sababu hana mpango wa kuihama Azam kwa sasa.
Beki huyo wa kati alisema bado ana mkataba na Azam na anauheshimu vilivyo, kadhalika analo deni kubwa kwa klabu hiyo hasa kwa soka la kimataifa hivyo hafikirii kuondoka kirahisi kama inavyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Ukweli mimi siendi kokote, mimi ni mchezaji wa Azam nitaendelea kuwa mchezaji wa Azam mpaka mwisho wa mkataba wangu, ni klabu ninayoipenda na ninayoona nina deni kubwa ambalo napaswa kulipwa hasa kwa michuano ya kimataifa," alisema.
Morris ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Azam walioshindwa kuitumikia klabu hiyo katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo klabu hiyo iliishia kwenye 16 Bora, kutokana na kusimamishwa na uongozi wao kwa tuhuma za Rushwa.
Hata hivyo Morris na wachezaji wenzake, Said Murad, Erasto Nyoni na kipa Deo Munishi 'Dida' walisafishwa na Taasisi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kurejeshwa klabu mwishoni mwa msimu.
Juu ya msimu ulioisha, Morris alisema ulikuwa mgumu na wenye ushindani, huku akidai kufurahishwa na jinsi Azam ilivyozikimbiza Simba na Yanga kiasi cha kukaribia kutwaa ubingwa kabla ya kuteleza na kuiachia Yanga inyakue taji la 24 kilaini.
"Ligi ilikuwa ngumu na huenda msimu ujao ikawa ngumu zaidi kutokana na timu kuonyesha kuimarika kila uchao na hasa kupewa nafasi kwa wachezaji vijana," alisema.

Matokeo Kidato cha Sita:Sifuri kibao zafutwa kimyakimya

http://laivu.com/habari/files/2013/02/kawambwa1.jpg
Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi Dk Shukuru Kawambwa


MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.


“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.


 "Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa.

" Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika na wanafunzi wapya, yaani kama wanaanza kidato cha kwanza wawe wanapewa mitihani ya kupimwa kwa kuzingatia alama mpya na waendelee nazo hadi mitihano yao ya mwisho.

“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato cha tano mara wanapoanza shule, kila mitihani wanayopewa isahihishwe na kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka NECTA.


Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya alama, alama mpya zilizokuwa zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34 hadi sifuri; badala ya alama hiyo F kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia 35 tofauti na awali, yaani alama 21.


Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita tofauti na muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa kidato cha nne ambapo matokeo yalitangazwa na kisha kufutwa ili kuyapanga upya kwa kutumia alama za zamani.


Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema; “Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa kuandaa matokeo ya kidato cha sita unaendelea, siwezi kusema lini hasa utakamilika lakini nina uhakika ni katika muda muafaka.”


Kuhusu matokeo ya kidato cha sita kucheleweshwa kutokana kupangwa upya ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana na matumizi ya alama mpya za kufaulu, Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa kuzingatia alama za zamani) yamekuja wakati mchakato wa kuandaa matokeo ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa kufuata maagizo hayo.”


Hata hivyo, hakuweka bayana kama matokeo ya awali kabla ya maagizo ya Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia alama za zamani yamewafanya wanafunzi wengi kufeli na badala yake akasema; “Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato wa matokeo hayo haukuwa umefika mwisho. Takwimu rasmi hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si sahihi kusema rasmi walifeli.”


Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa matokeo yanayotarajiwa ya kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi 50,000 wamepata unafuu katika matokeo yao tofauti na awali.


Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yaliyotangazwa Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani huo walifaulu.


Katika matokeo hayo idadi ya wasichana waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi 80,686 na idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361.


Katika matokeo hayo watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni 15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903 lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo itabadilika kwa sababu ya alama kuongezwa kwa watahiniwa hao wa mwaka 2012.


Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja na vituko walivyofanya baadhi ya wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani na kutokana na makosa hayo, watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao.


Source: Raia Mwema.

FAINALI ZA VODACOM MIC KING KUFANYIKA  J'MOSI

Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni DJ John Dilinga (JD), Prodyuza Ally Baucha na Prodyuza Tudd Thomas.
Kutoka kushoto waliokaa ni msanii Stamina, DJ John Dilinga, Abdallah Mrisho, Ally Baucha na Tudd Thomas katika picha ya pamoja na washiriki wa The Vodacom Mic King waliosimama nyuma.
Wakali wa MIC wanaowania gari wakiwa katika pozi na gari hilo.
Wanahabari wakichukua baadhi ya matukio.
…Wakimsikiliza Abdallah Mrisho.
Hawa ndiyo wakali tisa wanaowania gari aina ya Toyota Funcargo (New Model).
Uongozi wa Dar Live Co. Ltd leo umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la Usiku wa Hip Hop na fainali za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama ‘The Vodacom Mic King’ kwa wanahabari. Tamasha hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. Jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Mbali na zawadi ya gari, mshindi wa kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi. Majaji katika shindano hili ni mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na Prodyuza Ally Baucha.
Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao ni Fid Q, Joh Makini, Stamina, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na shoo kali kutoka kundi la Wakali Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya vizuri mwaka 2012/13. Kutakuwa na Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.
(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)

Friends Rangers na wenzao kuchujana RCL Wikiendi


Na Boniface Wambura
LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele.

Timu zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Siku hiyo hiyo Uwanja wa Azam ulioko Chamazi utatumika kwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga wakati Jumapili (Mei 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Machava FC ya Kilimanjaro na Mpwapwa Stars ya Dodoma itakayochezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Stand United ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida katika mechi itakayochezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Polisi Jamii ya Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana siku hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi. Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu wakati timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

Wabunge nusura wachapane makofi

Wabunge Anna Kilango (kulia) na Tundu Lissu aliyeshikiliwa wakitupiana maneno

BAADA ya Bunge kuahirishwa jana, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.

 
Maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.
 
Hata hivyo wawili hao walimalizana kiutu uzima, japo awali ilidaiwa ilikuwa mshikemshike kama sio kuamuliwa wangeweza kuchapana makofi hadharani.

Liunda kuwatathimini waamuzi mechi ya FIFA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUOM9IRMZijo63-gOG0Myp2_FetrrPAa1FMIGgam1cJJeCV3Zw9RJxhccBlTqfqv1BugkRqtKZpQeEqBNDPehsoBY_0JHLwIcpdrPLMoLPcJYFT2o3h3y1-9g6SWu_adMOBBokNV6MFCU/s1600/liunda.JPG
Leslei Liunda

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.

Mechi hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Verzea mjini Praia.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa Mauritania.

Real Madrid yathibitisha kuacha na Mourinho

 
Kocha Jose Mourinho

KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa kocha wake, Jose Mourinho ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu na kuwa nafasi kubwa ya kurejea Stanford Bridge kuinoa Chelsea.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyomnukuu Rais wao, Florentino Perez wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, kuwa Mourinho hatafukuzwa klabuni hapo.

Perez akasema kuwa, wamekubaliana na Mreno huyo kumaliza mkataba wao na hivuyo kuondoka Real Madrid mwishoni wa msimu huu.

Pia Rais huyo aliweka bayana kwamba hawajaanza kufanya mazungumzo na kocha yeyote kwa ajili ya kuziba nafasi ya Mreno huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa mbioni kurejea Chelsea.

Kwa taarifa hiyo ya klabu yake ya sasa ya kuachana naye ni wazi njia ya kurejea Uingereza imekuwa nyepesi tofauti na ilivyotarajiwa na kwamba mwenyewe amekuwa akisisitiza anatamani kurudi nchini humo kutokana na mazingira aliyokuwa nayo Madrid.

Kocha huyo amekuwa na msimu mbaya kwa mwaka huu baada ya timu yake kutoambulia taji lolote ikishindwa kufuzu fainali za Ligi ya Ulaya inayochezwa Jumamosi kwa kung'olewa na Borrusia Dortmund kwenye Nusu fainali, kufungwa Fainali ya Kombe la Mfalme na kushindwa kutetea taji kwa mahasimu wao Barcelona.

Stars yaingia kambini bila akina Samatta


TIMU ya taifa ya soka (Taifa Stars) jana jioni ilianza rasmi kambi yake jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kundi C dhidi ya timu ya taifa ya Morocco (Simba wa Atlasi) itakayopigwa Juni 8 mwaka huu kuwania kufuzu kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazili 2014.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa kikosi kilichoingia kambini jana kinaanza mazoezi rasmi leo jijini Dar es Salaam na kinawakosa washambuliaji wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
"Wachezaji wote walioitwa na kocha (Kim Poulsen) isipokuwa Samatta na Ulimwengu wanaingia kambini ni leo (jana) jioni kuanza kambi ya Stars na kesho (leo) wataanza rasmi mazoezi kabla ya safari ya Ethiopia ambako Stars itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Sudani Juni 2," alisema Wambura.
 Alisema kuwa Samatta na Ulimwengu wameshindwa kuungana na kikosi cha Mdenmark Poulsen kwa sababu bado wanahitaji kwenye kikosi cha TP Mazembe kinachoshiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika na kwamba wataungana na Stars mjini Marrakech, Morocco Juni 3.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machi 24 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars mabyo kwenye kundi hilo imepangwa pia na timu za Ivory Coast na Gambia, ilishinda 3-1.
Ivory Coast ndiyo wanaongoza kundi hilo wakikwa na pointi 7 wakifuatwa na Taifa Stars wenye pointi 6 wakati Morocco wanakamata nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi mbili huku Gambia wakishika mkia baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zote tatuy ambazo kila timu kwenye kundi hilo imeshacheza.

HADIJA SAID NDIYE MISS UTALII TANZANIA KWA MWAKA 2012/2013

MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO  KATIKATI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM KUSHOTO NA MSHINDI WA TATU KULIA THELESIA KILOMO MISS UTALII VYUO VIKUU.
 MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO AKISHWA TAJI LA USHINDI NA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO

 KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO
 KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO ,MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO NA MISS UTALII SINGIDA MWAKOMBO KESSY ALIYESHINDA NAFASI YA TANO

 WASHIDI WA TANO BORA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI MKOA WA TANGA.

Ratiba Ya Kagame kuanikwa leo

 
RATIBA ya mashindano ya 39 ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame ambayo yatafanyika kuanzia Juni 18 hadi Julai 2 mwaka huu, inatarajiwa kutangazwa leo jijini Dafur, Sudan imeelezwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye, jumla ya timu 13 zimethibitisha kushiriki michuano hiyo ya kila mwaka.
Musonye alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika miji ya Al Fasher na Kadugli iliyoko Gordofan Kusini ambapo maandalizi yake yamekamilika.
"Viongozi wa serikali ya Sudan walioko Khartoum na magavana wa Darfur Kaskazini na Gordofan Kusini wamesema kila kitu kinachohusika kuelekea mashindano hayo kwenye miji hiyo miwili kimekamilika," alisema Musonye katika taarifa yake.
Aliutaja uwanja wa Al Fasher utaweza kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano baada ya Chama cha Soka cha Sudan (SFA) na CECAFA kujiridhisha kwamba amani ipo eneo hilo.
Aliongeza kuwa Gordofan Kusini ambao wamesaidiwa maandalizi ya gavana, Ahmed Mohammed Haruna, ndiyo watakuwa wenyeji wa mechi ya ufunguzi kwenye uwanja wao unaochukua mashabiki 40,000.
Naye Mweka Hazina wa SFA, Osama Atelamanan, amesema kwamba Sudan wako tayari kuwa wenyeji wa mashindano hayo na wamejipanga kuandaa michuano iliyobora mwaka huu kuliko michuano iliyopita.
Alizitaja timu 13 zitakazochuana kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Yanga ni pamoja na El Merreikh, Al Shandy, Al Hilal Kadugli (Sudan), Al Nasr (Sudani Kusini), Simba (Bara), Tusker (Kenya), Elman (Somalia), Ports (Djibouti), Falcon (Zanzibar), APR (Rwanda), Vitalo (Burundi) na Express ya Uganda.
Mwaka huu katika mashindano hayo ya kila mwaka hakutakuwa na timu mwalika licha ya Lupopo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutuma maombi mapema.

Chanzo:NIPASHE

MRISHO NGASSA HATIMAYE ARUDI RASMI JANGWANI

Mrisho Ngassa akiongea na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada y akutambulishwa rasmi jana.
KATIBU Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngassa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb  amesema anashukuru kwa Ngassa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu.
Kwa kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa kusema kuwa Ngassa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha Ngassa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na kunishangilia pia.
Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngassa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO  (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)
Mrisho Ngasa akikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga na katibu mkuu Lawrence Mwalusako.
CHANZO;www.youngafricans.com