MRISHO NGASSA HATIMAYE ARUDI RASMI JANGWANI

Mrisho Ngassa akiongea na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada y akutambulishwa rasmi jana.
KATIBU
Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha
rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea
katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa
miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngassa
amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya
kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3
uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye
mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema
anashukuru kwa Ngassa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji
anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa
akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya
juu.
Kwa
kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika
timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa
kusema kuwa Ngassa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha
Ngassa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya
Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua
wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na
kunishangilia pia.
Nimeamua
kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee
wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa
moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo
kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngassa
anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya
kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)

Mrisho Ngasa akikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga na katibu mkuu Lawrence Mwalusako.
CHANZO;www.youngafricans.com
No comments:
Post a Comment