STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 21, 2013

Ratiba Ya Kagame kuanikwa leo

 
RATIBA ya mashindano ya 39 ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame ambayo yatafanyika kuanzia Juni 18 hadi Julai 2 mwaka huu, inatarajiwa kutangazwa leo jijini Dafur, Sudan imeelezwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye, jumla ya timu 13 zimethibitisha kushiriki michuano hiyo ya kila mwaka.
Musonye alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika miji ya Al Fasher na Kadugli iliyoko Gordofan Kusini ambapo maandalizi yake yamekamilika.
"Viongozi wa serikali ya Sudan walioko Khartoum na magavana wa Darfur Kaskazini na Gordofan Kusini wamesema kila kitu kinachohusika kuelekea mashindano hayo kwenye miji hiyo miwili kimekamilika," alisema Musonye katika taarifa yake.
Aliutaja uwanja wa Al Fasher utaweza kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano baada ya Chama cha Soka cha Sudan (SFA) na CECAFA kujiridhisha kwamba amani ipo eneo hilo.
Aliongeza kuwa Gordofan Kusini ambao wamesaidiwa maandalizi ya gavana, Ahmed Mohammed Haruna, ndiyo watakuwa wenyeji wa mechi ya ufunguzi kwenye uwanja wao unaochukua mashabiki 40,000.
Naye Mweka Hazina wa SFA, Osama Atelamanan, amesema kwamba Sudan wako tayari kuwa wenyeji wa mashindano hayo na wamejipanga kuandaa michuano iliyobora mwaka huu kuliko michuano iliyopita.
Alizitaja timu 13 zitakazochuana kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Yanga ni pamoja na El Merreikh, Al Shandy, Al Hilal Kadugli (Sudan), Al Nasr (Sudani Kusini), Simba (Bara), Tusker (Kenya), Elman (Somalia), Ports (Djibouti), Falcon (Zanzibar), APR (Rwanda), Vitalo (Burundi) na Express ya Uganda.
Mwaka huu katika mashindano hayo ya kila mwaka hakutakuwa na timu mwalika licha ya Lupopo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutuma maombi mapema.

Chanzo:NIPASHE

No comments:

Post a Comment